Shocking: Video inayomuonesha P Diddy akimpiga vibaya mpenzi wake Cassie yawekwa hadharani

Shocking: Video inayomuonesha P Diddy akimpiga vibaya mpenzi wake Cassie yawekwa hadharani

Skendo inayomuandama msanii maarufu wa miondoko ya HipHop wa nchini Marekani, Puff Daddy a.k. P Didy, inazidi kupamba moto baada ya CNN kupandisha mitandaoni video inayomuonesha akimpiga vibaya mpenzi wake wa zamani, Cassie Ventura.

Video hiyo ilinaswa kwenye moja ya hoteli waliyoenda kwa mapumziko mwaka 2016.

View attachment 2992915


----------------
Kipande cha video kilichonaswa kupitia kamera za CCTV kimeweka hadharani kupitia Kituo cha CNN kikimuonesha nguli wa Muziki wa Hip Hop, Sean "Diddy" Combs akimshambulia aliyekuwa mpenzi wake, Casandra "Cassie" Ventura hotelini Machi 5, 2016.

Baada ya video hiyo kuwekwa mtandaoni, Cassie hajatoa tamko lolote lakini Mwanasheria wake amenukuliwa akisema “Hizo ni baadhi ya tabia za Combs" wakati Mwanasheria wa Diddy hajatoa jibu

CNN imeeleza video hiyo ilirekodiwa katika moja ya Hoteli ya Los Angeles, Marekani, Cassie anaonekana akitoka chumbani kuelekea kwenye lifti kisha Diddy akiwa na taulo pekee anamfuata na kuanza kumpiga, anamvuta kwa kumburuza huku akionekana kutoa maneno kama anamfokea.

Mwendelezo wa video unaonesha Diddy anampiga mwenza wake huyo akiwa chini kisha anakusanya mizigo aliyokuwa nayo Cassie na kuondoka nayo.

Ofisi ya Mwanasheria wa Los Angeles imeeleza “Ikiwa ni tukio la Mwaka 2016 hatutaweza kushtaki kwa kuwa ni shambulio lililotokea nje ya muda unaostahili kufunguliwa mashtaka."

Inadaiwa kuwa Diddy alinunua video hiyo ya hotelini kwa Dola 50,000 alipobaini amenaswa kwenye kamera kwa wakati huo.
Mbona yupo mkupiga hewa tu!

Wewe mleta mada umemuona anampiga mtu katika video hiyo?
 
Aisee kwa jinsi US ilivyo, huyu career yake imeishia hapo, yaani hii haina mjadala.
Pdidy hana jipya tena. Its Over.... CCTV inaonyesha ilikuwa ni 2016 march, issue ya 2016 inakuja kumkaanga miaka 8 baadae, mazingira inaonekana walikuwa hotelini, sasa nashangaa ilikuaje waliokuwa wamiliki wa hio hotel walishindwa kutoa hizo video kwenye vyombo vya habari kipindi hiko, sijui walipewa pesa, noma mzee.

Kweli msomali ni msomali tu, nasikia ni jamii ya watu kukumaliza ukimzingua ni dk 0.

Hapo tegemea maandamano
Mkuu hujamalizia kusoma naona
Imeandikwa hapo mwisho jamaa alitoa $50,000 kuinunua hiyo clip wakati huo
Lakini wajanja wamevujisha tu
 
Hiyo mbona kawaida, wangapi wanapigana kwenye ndoa/mahusiano yao? Vile vile tutajuane makubaliano yao walipokuwa himo ndani? Je kama huyo binti alimuibia pesa zake?
Huwa nawashangaa sana watu wanaoona 'any abusive habits' ni kawaida..!
Yaani umesema ni KAWAIDA how.??? kwamba kama kuna baadhi wanafanya ndiyo jambo hata kama ni ovu liwe kawaida..??

Naomba siku uone binti yako, ama mzazi wako wa kike afanyiwe hivyo kisha urudi hapa kusema ni kawaida na ni makubaliano yao..
Ahsante.
 
Hakuna suala la uzungu wala uafrika. Pdidy ni mnyama. Waafrika mnakosea mkitaka kupewa haki yenu mnataka jificha kichaka cha ubaguzi. Pdiddy alimla mpaka msanii wenu wa kiume mmoja wa hapa Tz. But wanaomfahamu pdidy watakuambia ni mnyama kinyama. Ni mafia. So si suala la wazungu wala waafrika.

Mkuu kwani ndugu yetu alibakwa? si walikubaliana wenyewe
 
Niko hapa nawasoma ambao mpo kwenye denial 😅

Diddy surely did everything. Kama hana cha kupoteza awalipue na hao wengine ili waende down wote, anaogopa nini? Anawaprotect wasiomprotect why? Ndio utaelewa kuwa anajiprotect mwenyewe kwa kuficha/kupoteza ushahidi. Its all about him.

He's powerful man, hataenda down kirahisi, ila lazima tujifunze kila jambo lina mwisho.

Bottom line, Mwanaume anayepiga wanawake 🚮🚮
 
Kawaida wangese huporomosha matusi ya nguoni. Hakuna jipya ulilofanya. Acha kutetea uovu kwa kujificha kwenye kichaka cha weusi na weupe. Wewe siku mumeo akikupiga hivyo utakaa kimya?
Mbona ww jana baada ya game nmekupiga hivyo na hukusema kitu? Au ukija humu kwa fake id unasahau kwamba umeolewa? Unajitoa ufaham kwamba ww ni mke wa mtu!
 
Yaliyojiri hatujui mpaka akampiga hivyo tusihukumu kama vile tulikuepo vyombo vitafanya kazi huko kwao sisi tujangaike na mabarabara yetu yaliyojaa mashimo kila sehemu nchi nzimaa
Hata sheria ya hiyo nchi yako ambayo mabarabara yake yamejaa mashimo hairuhusu kumpiga mwizi/kibaka ukimkamata anaiba. Hakuna justification yoyote kwenye hiyo video, Kwahiyo ondoa kichwani mwako hiyo "hatujui kilichojiri". Kilijiri/hakikujiri kitu, wrong is wrong.

Marekani si ukimani.
 
Tuombe uzima tuone hii ngoma itaishia wapi.

Hv ww ulishaona mtu anavamiwa kwake na FEDs na wanakosa kitu?

Na nahisi hata waloanzisha hili sekeseke la diddy wanajilaumu sababu ni timely bomb, ushahidi wa kumpeleka diddy jela maisha upo sana tu, ila unawahusisha wengine weeengi.

Tukirudi kwenye hii video, "There's no case kwa diddy" sabb hio kesi walishasettle mapema kabisa, files zake zimeshafungwa, unless waitumie kumotivate watu wengine alowafanyia assault wamfungulie class action. Na ni hilo pekee ndo wanalolitafuta sabab ushahidi mwingine unawahusisha hadi Wafanyabiashara, entertainers na Gurus wa Manhattan na viunga vyake huko wallstreet, etc...
we unang'ang'ania hiyo kesi walishai settle...wameimalizaje kwa rushwa au kisheria em tueleweshe kwanza
 
Tuombe uzima tuone hii ngoma itaishia wapi.

Hv ww ulishaona mtu anavamiwa kwake na FEDs na wanakosa kitu?

Na nahisi hata waloanzisha hili sekeseke la diddy wanajilaumu sababu ni timely bomb, ushahidi wa kumpeleka diddy jela maisha upo sana tu, ila unawahusisha wengine weeengi.

Tukirudi kwenye hii video, "There's no case kwa diddy" sabb hio kesi walishasettle mapema kabisa, files zake zimeshafungwa, unless waitumie kumotivate watu wengine alowafanyia assault wamfungulie class action. Na ni hilo pekee ndo wanalolitafuta sabab ushahidi mwingine unawahusisha hadi Wafanyabiashara, entertainers na Gurus wa Manhattan na viunga vyake huko wallstreet, etc...
Kesi ipo. Kilichofanyika hapo ni jinai na mtu yoyote anaweza kufungua kesi kumshitaki Diddy kwa kutumia hiyo video.

Kuna kesi ya dada alikuwa amepigwa na mwanaume wake hadi mguu umefungwa hogo, baadae kesi kufika mahakamani demu akawa anakataa kuwa jamaa hajamfanyia lile tukio so ushahidi ukawa hamna.

Ila story ilipata airtime kubwa sana mitandaoni sasa kuna mtu ana biashara yake ng'ambo au opposite ya eneo tukio lilipotokea na kamera ili nasa vizuri lile tukio,kuna ka NGO kana deal na maswala ya domestic abuse walienda kwa familia ya yule dada na kuwapa video kesi ikafunguliwa upya, demu anakataa sio yeye kwenye video ili kumprotect jamaa yake.

Ila mahakama kwa kutumia ushahidi wa video wakatupilia mbali maneno ya demu kuwa si yeye na kuendelea na kesi na kumkuta jamaa ana hatia na wakatumia ushahidi wa mashuhuda wa kwanza wa kesi jamaa akachezea kifungo vizuri tu.


Sasa hapo wewe ukitazama haumuoni Diddy hapo kwenye video na huyo si ni Case.

Hata kama walisettle issues zao ila ilikuwa ni kati yao ila huu ushahidi unatumika vizuri tu kufungua mashtaka mapya na mwamba atachezea kifungo bila ubishi.
 
Mimi namuombea Diddy ashinde tu. Ndio alikosea lakini sakata lote ni racial motivated. Mamchukia sana 50 cent yani kashadidia kweli. Inatakiwa am -support nigger mwenzake ama akae kimya.
Sasa atamsupport kwenye issue ya domestic violence wakati mwamba anazingua live hapo. We kumtia teke za kichwa mtoto wa watu unaona ni jambo zuri?

Diddy anazingua.
 
Acha kukaa vijiweni. Diddy alifanya ujinga na lazima sheria ichukue mkondo wake.

Diddy aliilipa hotel 50k USD video isitokee kumbe wajuba bado wanayo, diddy lazima awajibishwe kwa ujinga wake. Hakuna mtu alimtuma kuipiga hiyo pisi. Mchezo wa diddy umeisha.
Halafu nahisi alikuwa kashapuliza bangi na ngada hapa sio bure. We anampiga mtu namna hiyo as if anapiga jiwe.
 
Back
Top Bottom