Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi
Shuhudia sensa live kupitia TBC, nimeshuhudia live, citizen No. 1, Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan akihesabiwa toka katika makazi yake rasmi ya kiserikali Ikulu ya Chamwino Dodoma!.

Saa hizi ameisha maliza kuhesabiwa.

Wana JF, let's share different experiences za sensa na muendelezo wa zoezi la Kuhesabiwa toka maeneo tofauti tofauti. Mimi niko home kwangu hapa maeneo ya Tandale kwa Mtogolo ambapo nimepanga ubazi mzima, nawasubiria kwa hamu na shauku kubwa makarani wa sensa wananifikie, na kwavile tuna taarifa ya ugeni huu, kama jadi ya Uafrika, tumewaandalia chai ya rangi na vitafunwa vya huku kwetu Uswazi, chai na chapati, vitumbua na maandazi. Chai ya maziwa na Vitafunwa vya mitaa ya kishua ni keki, sambusa, mkate wa siagi na mayai ya kukaanga.

Bado nawasubiria makarani wa sensa, vipi wewe mwenzagu?. Tuhabarishane na kupashana kuhusu zoezi hili.

Paskali
 
Hivi nchi zilizoendelea wanahesabiwa hivi kama mifugo? Ukiwa na data za watu waliozaliwa, waliokufa, walioingia na kutoka nchini, siyo kwamba inabaki issue ya simple mathematics tu hapo?
 
Rais Samia baada ya kuhesabiwa, amezungumza, na Kamisaa wa Sensa, Spika Mstaafu Anne Makinda pia amezungumza, na kusema zoezi la sensa litadumu kwa siku 7, hivyo makarani wa sensa wasipopita kwako leo, watapita kesho au keshokutwa, acha majibu ya dodoso la sensa kisha endelea na shughuli zako.
P
 
zoezi la kuhesabiwa litadumu kwa siku 7 kuanzia leo, hivyo usipo hesabiwa leo huenda utahesabiwa kesho au keshokutwa.
jambo la msingi acha taarifa zako za msingi nyumbani.
kazi iendeleee hakuna kulala...
.
Hili halijaeleweka, sijui ni bahati mbaya au nimakusudi?

Macho namasikio Yako kwa siku yaleo TU.
 
Would be better if I had that job of counting people. But they refuse to give me that job while they know I'm jobless. therefore I came into the conclusion that they'll find me katika sehemu yangu ya kazi.
 
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜ƒ
Nimedhani live ukiwa chamwino kumbe kwenye tv!!!

Ila mkuu P, siasa nenda nazo polepole.
Hazitaki haraka. One day yes.
Kuna wazee wanapata fursa baada ya kustaafu (60+yrs) so, kikubwa uzima!
Muhimu, epuka kusifiasifia hata visivyofaa kusifiwa! Kuwa ndani ya CCM au kumkubali kiongozi fulani, haimaanishi kuunga mkono kila kitu!
 
Would be better if I had that job of counting people. But they refuse to give me that job while they know I'm jobless. therefore I came into the conclusion that they'll find me katika sehemu yangu ya kazi.
Unamkomesha S100, au?πŸ™‚
 
Pascal laiti kama usingekuwa mwenye njaa kali baas nazani ww ungekuwa mtu bora sana kwa nchi yetu..lakini njaa yako inakupotezea mengi sana. You have to stand on what you believe. Stop being dragged by dumbest politicians.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…