Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Rais Samia baada ya kuhesabiwa, amezungumza, na Kamisaa wa Sensa, Spika Mstaafu Anne Makinda pia amezungumza, na kusema zoezi la sensa litadumu kwa siku 7, hivyo makarani wa sensa wasipopita kwako leo, watapita kesho au keshokutwa, acha majibu ya dodoso la sensa kisha endelea na shughuli zako.
P
Unaachaje majibu ya dodoso wakati hunalo? Nafikiri dodoso lingekua oublic document. Likae hata kwenye websites za serikali ili tuandae majibu.
 
Ulikiacha jina langu, yote yaliobaki nitadanganya maana wakijua unavyvimiliki hawatakawia kukudandia kodi na tozo, tena mimi mlemavu wa macho
 
Hivi wale ndugu zetu wenye ulemavu wa akili wanahesabiwa?.
Wafungwa? wagonjwa mahospitalini?
 
Hebu tueleze ugeni huo kwa mama meza ya brekifasti ilitapakaa mapochopocho gani, mimi huku kwangu Vianzi nimewaandalia togwa ya Manelumango na magimbi.
Huku kwetu Kwa Mtogole, unadhani tuna meza za mapochopocho?. Huku ni mwendo wa birika la chai na kistuli cha kawa ukifunua ndio unakutana na Vitafunwa vya staftahi, chapati, vitumbua na andazi.
P.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hivi nchi zilizoendelea wanahesabiwa hivi kama mifugo? Ukiwa na data za watu waliozaliwa, waliokufa, walioingia na kutoka nchini, siyo kwamba inabaki issue ya simple mathematics tu hapo?
Marekani na utajiri wao wanafanya sensa kama sisi! Sensa si idadi ya watu pekee! Ni zaidi ya hapo! Taarifa nyingi zinahitajika
 
Wanabodi
Shuhudia sensa live kupitia TBC, nimeshuhudia live, citizen No. 1, Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan akihesabiwa toka katika makazi yake rasmi ya kiserikali Ikulu ya Chamwino Dodoma!.

Saa hizi ameisha maliza kuhesabiwa.

Wana JF, let's share different experiences za sensa na muendelezo wa zoezi la Kuhesabiwa toka maeneo tofauti tofauti. Mimi niko home kwangu hapa maeneo ya Tandale kwa Mtogolo ambapo nimepanga ubazi mzima, nawasubiria kwa hamu na shauku kubwa makarani wa sensa wananifikie, na kwavile tuna taarifa ya ugeni huu, kama jadi ya Uafrika, tumewaandalia chai ya rangi na vitafunwa vya huku kwetu Uswazi, chai na chapati, vitumbua na maandazi. Chai ya maziwa na Vitafunwa vya mitaa ya kishua ni keki, sambusa, mkate wa siagi na mayai ya kukaanga.

Bado nawasubiria makarani wa sensa, vipi wewe mwenzagu?. Tuhabarishane na kupashana kuhusu zoezi hili.

Paskali
Yeye ndio Mkuu wa Kaya??
 
Bado nawasubiria makarani wa sensa, vipi wewe mwenzagu?. Tuhabarishane na kupashana kuhusu zoezi hili
Nimewapa kifungua kinywa kwanza. Nimeweka hamira ya kutosha. Watashinda wameshiba, wanakunywa Maji tu
 
Attachments

  • IMG-20220823-WA0027.jpg
    IMG-20220823-WA0027.jpg
    84.8 KB · Views: 4
Huku kwetu Kwa Mtogole, unadhani tuna meza za mapochopocho?. Huku ni mwendo wa birika la chai na kistuli cha kawa ukifunua ndio unakutana na Vitafunwa vya staftahi, chapati, vitumbua na andazi.
P.
Mimi nilidhani uliona meza ya brekifasti kwa mama Dom, sisi huku Vianzi Vikindu huwa meza yetu ni mkeka japo umebaki kipande lakini unafaa sana na viti ni vipande vya minazi, ni vizuri sana kwa afya kwani vinajenga stamina.
 
Rais Samia baada ya kuhesabiwa, amezungumza, na Kamisaa wa Sensa, Spika Mstaafu Anne Makinda pia amezungumza, na kusema zoezi la sensa litadumu kwa siku 7, hivyo makarani wa sensa wasipopita kwako leo, watapita kesho au keshokutwa, acha majibu ya dodoso la sensa kisha endelea na shughuli zako.
P
Sasa hili la kuweka siku ya mapumziko ilimaanisha nini?
 
zoezi la kuhesabiwa litadumu kwa siku 7 kuanzia leo, hivyo usipo hesabiwa leo huenda utahesabiwa kesho au keshokutwa.
jambo la msingi acha taarifa zako za msingi nyumbani.
kazi iendeleee hakuna kulala...
.
Kwa haya maswali marefu kwenye dodoso la Sensa 2022, hawamalizi ndani ya siku 7. Labda 14 na ni wakifoji majibu!

Mi si mchumi lakini... tusubirie tozo ya simu, redio, laptops, taka, n.k miaka michache ijayo...
 
Wanabodi
Shuhudia sensa live kupitia TBC, nimeshuhudia live, citizen No. 1, Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan akihesabiwa toka katika makazi yake rasmi ya kiserikali Ikulu ya Chamwino Dodoma!.

Saa hizi ameisha maliza kuhesabiwa.

Wana JF, let's share different experiences za sensa na muendelezo wa zoezi la Kuhesabiwa toka maeneo tofauti tofauti. Mimi niko home kwangu hapa maeneo ya Tandale kwa Mtogolo ambapo nimepanga ubazi mzima, nawasubiria kwa hamu na shauku kubwa makarani wa sensa wananifikie, na kwavile tuna taarifa ya ugeni huu, kama jadi ya Uafrika, tumewaandalia chai ya rangi na vitafunwa vya huku kwetu Uswazi, chai na chapati, vitumbua na maandazi. Chai ya maziwa na Vitafunwa vya mitaa ya kishua ni keki, sambusa, mkate wa siagi na mayai ya kukaanga.

Bado nawasubiria makarani wa sensa, vipi wewe mwenzagu?. Tuhabarishane na kupashana kuhusu zoezi hili.

Paskali

Wewe Pascal umeshakua lipumbavu kabisa ! Yaani unaandika upuuzi ili iweje ? Lini uliishi kwa mtogole wewe ? Sema tu straight this sensor exercise has miserably failed ! Sema ukweli sio kuzunguka kipuuzi namna hiyo ! Bull sh..
 
Back
Top Bottom