Shule ambazo mtoto anashinda siku nzima shuleni kama watu wazima kazini ni hatari kwa future ya mtoto zama hizi

Shule ambazo mtoto anashinda siku nzima shuleni kama watu wazima kazini ni hatari kwa future ya mtoto zama hizi

kwa ambao wana wake wa nyumbani na ndugu waaminifu muda wote hawa ndio idadi kubwa ya watz ilipo.

Hivyo hao unaowasema wewe ni wachache sana hapa tanzania kwa msingi huo shule sio sehemu salama kwa asilimia kubwa ya watoto wa tanzania.
Fanya upya utafiti, labda kwa mikoani, ila mfano Dar, familia nyingi mama anauza vitumbua huko na mboga, baba yupo saidia ujenzi au kibarua kwa mhindi,

Kwa jinsi jamii yetu ilivyo ni mara mia watoto wakawa wanakaa shule hadi saa 12 kuliko kuwaacha mtaani,
Vitoto vyenyewe vina nyege balaa hususan sekondary hawa, ukiwaruhusu saa 8 hawa mimba za utotoni zitashoot hatutaamin,

Tupiganie watoto wawe wanapewa extra curricular activities huko huko shuleni, ila mtaa huu et mtoto wa Dar arudu home saa 8, kisa extra curricular activities, zipi hizo mtaani tunatoa ? Maisha mnayosemea ya watoto wa Mbezi ndio hao watafundishwa computer mara sijui vinanda etc, wew upo zako mpiji magohe wazazi tu kutumia Word hawajui ndo mtoto atafundishwa Computer sijui kinanda,

Kuhusu kilimo, kama wanataka waende SUA, wajifunze kilimo bora, watoto wengi hasa wa mijini familia zao hazilimi wala hazina garden,

Kuhusu kupika watoto watajifunza hata weekend aiseee,
Watoto wasome sana, niny wenyewe mnaona jinsi ufaulu unavyopanda kwa kasi, watoto wajue maisha ni kazi kazi sio kucheza tu
 
Yaani huwa kila siku nasema , ningekuwa na mtoto anasoma ningegombana sana na walimu kuhusu tuition za jioni na weekend za hapa DSM.

Haiwezekani mwanafunzi wa primary awe busy kuliko hata wanachuo
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Na bado anakaririshwa mambo ambayo hata kwenye maisha hayamsaidii kabisa.
 
Wanataka mtoto apate A kana kwamba A ndio utajiri was mapesa kumbe ni karatasi lisilo na maana kwa kijana was ki TZ!!

Mi nilishadharau Sana hii elimu japo Nina jiwe moja!!

Elimu ni mzigo mkubwa Kwa wazazi na watoto wetu!!
 
Fanya upya utafiti, labda kwa mikoani, ila mfano Dar, familia nyingi mama anauza vitumbua huko na mboga, baba yupo saidia ujenzi au kibarua kwa mhindi,

Kwa jinsi jamii yetu ilivyo ni mara mia watoto wakawa wanakaa shule hadi saa 12 kuliko kuwaacha mtaani,
Vitoto vyenyewe vina nyege balaa hususan sekondary hawa, ukiwaruhusu saa 8 hawa mimba za utotoni zitashoot hatutaamin,

Tupiganie watoto wawe wanapewa extra curricular activities huko huko shuleni, ila mtaa huu et mtoto wa Dar arudu home saa 8, kisa extra curricular activities, zipi hizo mtaani tunatoa ? Maisha mnayosemea ya watoto wa Mbezi ndio hao watafundishwa computer mara sijui vinanda etc, wew upo zako mpiji magohe wazazi tu kutumia Word hawajui ndo mtoto atafundishwa Computer sijui kinanda,

Kuhusu kilimo, kama wanataka waende SUA, wajifunze kilimo bora, watoto wengi hasa wa mijini familia zao hazilimi wala hazina garden,

Kuhusu kupika watoto watajifunza hata weekend aiseee,
Watoto wasome sana, niny wenyewe mnaona jinsi ufaulu unavyopanda kwa kasi, watoto wajue maisha ni kazi kazi sio kucheza tu
Unapotumia mfano wa dar kumbuka kwamba dar ni sehemu ndogo ya TANZANIA.

Dar sio tanzania nzima.

Mwenzetu unaona kama Dar ndio tz yooote hakuna watu sehemu zingine,fungua kidogo ufahamu mkuu

So hoja yangu bado iko pale pale niliposema kwamba 👇👇

Hivyo hao unaowasema wewe ni wachache sana hapa tanzania kwa msingi huo shule sio sehemu salama(kukaa masaa mengI)kwa asilimia kubwa ya watoto wa tanzania(SIO WATOTO WA DAR)
 
Mtoto anaamshwa saa 11 alfajiri kujiandaa kwenda shule. Kurudi saa 12:30 jioni n ujinga sana kwa wazazi.
Kuna baadhi ya shule mtoto jtatu hadi jmosi shule.
Sio hivyo Bali hata likizo hatakiw kwenda na unamkuta ana rundo la madaftar unaomzidi uzito, mateso sana kwakweli.
 
Feza, Agakhan, Braeburn,hopac,IST,ISM, hawana huo upuuzi.
Unajua ada zao lakini? Isije ikawa wao ndiyo wanaongoza kwa upuuzi huo sema indirectly! (Hii ni kwa hoja kwamba watoto wanakalishwa muda mrefu shuleni kama sehemu ya shule kujiongezea kipato!)
 
Hizi boarding schools zenyewe Vipi, wao wanarudi kwa muhula
 
Tena akibaki na Uncle kwenye gari ndio balaa kabisa
 
Nilipita Kondoa alfajiri ya saa kumi na moja aisee niliwakuta watoto wadogo wanasubiri bus la shule bara bara kuu ya Kondoa/Dodoma kwa mazingira yale wako peke yao usalama ni mdogo sana aisee bado waje wazunguke na bus mpaka kufika shule na kurudi daah hao mpaka wanamaliza shule washachoka saana..
 
Vitu vingine ni ulimbukeni tu.
Sema tu na mifumo wakati mwingine inachangia,ila uangalie: watu waliosoma zamani,mtoto alikuwa anaanza chekechea ana miaka 6, huko kazi inakua kucheza na kuimba. Anaingia la kwanza,ameshazoea watu,wanafunzi wenzie,haliilii.
Watu waliosoma mpaka chuo kikuu,wako vizuli sana. Hata kapa pesa ni kidogo,lakini kiakili wapo vizuri.
Sasa hivi, mtoto ana miaka 3, eti aende shule. Kitoto kidogo kinaamshwa saa kumi na moja.
Lakini,bahati mbaya,hata walimu wa siku hizi,walio wengi wanataka pesa tu,ushauli wa maana huwezi kupata kwao.
Mtoto miaka mi4, eti afundishwe lugha za kimataifa na makolokolo kibao. Mzazi fake nae anategemea eti mwanae atakuwa na akili. Ukweli usemwe,wanaochukia wachukie. Mtoto aliesoma kwa mtindo huo,atabebwa bebwa,wengine ndo hao wanaojitoa wapate magari na maisha mazuri,bila kupewa uwezo wa kufikiri hawana.
Mtoto anafika miaka 10, hata chupi yake hawezi kufua. Hata kujiogesha hawezi. Mi najiulizaga miaka kama 20 ijayo,nchi za kiAfrika tutakuwa wapi.
Huko walikoendelea, wana walimu wazoefu. Wanajua mtoto wamleeje,uwezo wake upo wapi. Hawana hizo biashara za vyombo na mifugo. Sasa kwetu huku unawaiga,kesho ukiyumba, mtoto haeleweki. Au akikosea hesabu za maisha,anaishia kujuta. Pia darasani,mtoto hajazwi ujinga. Leo hii,hawa wa kwetu anakalilishwa kwamba Hitler alifanya haya,Bonapalte Napoleon kafanya nini, unajiuliza haya yatamsaidia nini. Wenzetu kama ni kitengo furani,anadili na hicho hicho. Miaka 20, mtu kuna kitu anakiweza,na anakimudu vizuri. Kwetu,kahitimu chuo kikuu,hata barua ya maombi ya kazi,hawezi iandika.
Mifumo inaharibu watu aise. Sasa,unaongoza watu 10,000 waliosoma kwa mtindo huo, utaambulia nini!!!!
 
Nilipita Kondoa alfajiri ya saa kumi na moja aisee niliwakuta watoto wadogo wanasubiri bus la shule bara bara kuu ya Kondoa/Dodoma kwa mazingira yale wako peke yao usalama ni mdogo sana aisee bado waje wazunguke na bus mpaka kufika shule na kurudi daah hao mpaka wanamaliza shule washachoka saana..
Ndo maana siku hizi watoto hawapendi shule,wanalazimishwa tu
 
Fanya upya utafiti, labda kwa mikoani, ila mfano Dar, familia nyingi mama anauza vitumbua huko na mboga, baba yupo saidia ujenzi au kibarua kwa mhindi,

Kwa jinsi jamii yetu ilivyo ni mara mia watoto wakawa wanakaa shule hadi saa 12 kuliko kuwaacha mtaani,
Vitoto vyenyewe vina nyege balaa hususan sekondary hawa, ukiwaruhusu saa 8 hawa mimba za utotoni zitashoot hatutaamin,

Tupiganie watoto wawe wanapewa extra curricular activities huko huko shuleni, ila mtaa huu et mtoto wa Dar arudu home saa 8, kisa extra curricular activities, zipi hizo mtaani tunatoa ? Maisha mnayosemea ya watoto wa Mbezi ndio hao watafundishwa computer mara sijui vinanda etc, wew upo zako mpiji magohe wazazi tu kutumia Word hawajui ndo mtoto atafundishwa Computer sijui kinanda,

Kuhusu kilimo, kama wanataka waende SUA, wajifunze kilimo bora, watoto wengi hasa wa mijini familia zao hazilimi wala hazina garden,

Kuhusu kupika watoto watajifunza hata weekend aiseee,
Watoto wasome sana, niny wenyewe mnaona jinsi ufaulu unavyopanda kwa kasi, watoto wajue maisha ni kazi kazi sio kucheza tu
Kwa jinsi jamii yetu ilivyo ni mara mia watoto wakawa wanakaa shule hadi saa 12 kuliko kuwaacha mtaani,
Vitoto vyenyewe vina nyege balaa hususan sekondary hawa, ukiwaruhusu saa 8 hawa mimba za utotoni zitashoot hatutaamini

Kumbe hili na wewe unalijua? Kama kweli wewe ni mzazi, na ukawa na uchungu na wanao,mtoto anatoa wapi malezi kama hakai na wazazi!?
Hapo hapo,huyo mlezi akimgusa tu, mzazi anaibuka kwamba mwanae kaguswa. Unategemea utapata nini hapo?!
Hao wanaouza vitumbua na kusaidia kazi,hatukatai kwamba maisha ni magumu. Lakini ugumu tunasababisha wenyewe.
Kisa tu watu wa mjini wana V8, na wewe unauza kijijini,heka 10 unapewa milioni 3, unajiona tajiri unahamia Dar! Unafika huko unakutana na wahuni,hata ya kodi huna. Hapo hapo unazaa kila kuchako!
Wazawa sawa,japo wenye akili wakiona mji unawakimbia,wanahamia mikoani.
1. Jiulize,miji mikubwa,wazee humo wenye pesa,wanajenga vijijini,mijemgo yao wanaachia wapangaji. Unadhani hawana akili?

2. Tupia jicho kwenye mafuriko ya Dar. Mtu anapanga. Siyo kajenga; bondeni. Mvua zikinyesha,mwanaume anakuwa wa kwanza kupanda ngazi,anyeshewe juu ya bati. Mke na watoto,wanahangaika na mafuriko chini. Maji ya vyoo wanameza. Ndo uanaume huo? Ndo utafutaji huo? Utakuta miaka 20 iliyopita mtaa fulani ulikuwa umejengwa kwa mpangilio. Leo hii,ujenzi wa ovyo,ndo chanzo cha kuharibika na kulalamika,serikali inalaumiwa kutofanya lolote. Serikali ni nani? Haya yote,ndo yanatengeneza wahuni. Unajua nini! Miaka ya nyuma kipindi tuisheni hazipo,walimu,walikuwa wazuri mno. Wakitegemea mishahara. Leo hii, twisheni ndo inalipa vizuri. Shule hawafundishi wanategeshea jioni na weekend. Ndo maendeleo haya?

Walimu wazoefu,wana somo la Psychology (kama sikosei kuandika). Kila lika la umri,lina namna ya malezi na uelewa.

Hivi,uliwahi jiuliza kwa nini wenye uwezo mkubwa huwapeleka watoto wao kusomea nchi za nje? Wengine kwenye shule zenye mfumo wa nchi za nje?
Unadhani huko wanapokea tu!? Kwa nini wachuje!?
 
Back
Top Bottom