Fanya upya utafiti, labda kwa mikoani, ila mfano Dar, familia nyingi mama anauza vitumbua huko na mboga, baba yupo saidia ujenzi au kibarua kwa mhindi,
Kwa jinsi jamii yetu ilivyo ni mara mia watoto wakawa wanakaa shule hadi saa 12 kuliko kuwaacha mtaani,
Vitoto vyenyewe vina nyege balaa hususan sekondary hawa, ukiwaruhusu saa 8 hawa mimba za utotoni zitashoot hatutaamin,
Tupiganie watoto wawe wanapewa extra curricular activities huko huko shuleni, ila mtaa huu et mtoto wa Dar arudu home saa 8, kisa extra curricular activities, zipi hizo mtaani tunatoa ? Maisha mnayosemea ya watoto wa Mbezi ndio hao watafundishwa computer mara sijui vinanda etc, wew upo zako mpiji magohe wazazi tu kutumia Word hawajui ndo mtoto atafundishwa Computer sijui kinanda,
Kuhusu kilimo, kama wanataka waende SUA, wajifunze kilimo bora, watoto wengi hasa wa mijini familia zao hazilimi wala hazina garden,
Kuhusu kupika watoto watajifunza hata weekend aiseee,
Watoto wasome sana, niny wenyewe mnaona jinsi ufaulu unavyopanda kwa kasi, watoto wajue maisha ni kazi kazi sio kucheza tu
Kwa jinsi jamii yetu ilivyo ni mara mia watoto wakawa wanakaa shule hadi saa 12 kuliko kuwaacha mtaani,
Vitoto vyenyewe vina nyege balaa hususan sekondary hawa, ukiwaruhusu saa 8 hawa mimba za utotoni zitashoot hatutaamini
Kumbe hili na wewe unalijua? Kama kweli wewe ni mzazi, na ukawa na uchungu na wanao,mtoto anatoa wapi malezi kama hakai na wazazi!?
Hapo hapo,huyo mlezi akimgusa tu, mzazi anaibuka kwamba mwanae kaguswa. Unategemea utapata nini hapo?!
Hao wanaouza vitumbua na kusaidia kazi,hatukatai kwamba maisha ni magumu. Lakini ugumu tunasababisha wenyewe.
Kisa tu watu wa mjini wana V8, na wewe unauza kijijini,heka 10 unapewa milioni 3, unajiona tajiri unahamia Dar! Unafika huko unakutana na wahuni,hata ya kodi huna. Hapo hapo unazaa kila kuchako!
Wazawa sawa,japo wenye akili wakiona mji unawakimbia,wanahamia mikoani.
1. Jiulize,miji mikubwa,wazee humo wenye pesa,wanajenga vijijini,mijemgo yao wanaachia wapangaji. Unadhani hawana akili?
2. Tupia jicho kwenye mafuriko ya Dar. Mtu anapanga. Siyo kajenga; bondeni. Mvua zikinyesha,mwanaume anakuwa wa kwanza kupanda ngazi,anyeshewe juu ya bati. Mke na watoto,wanahangaika na mafuriko chini. Maji ya vyoo wanameza. Ndo uanaume huo? Ndo utafutaji huo? Utakuta miaka 20 iliyopita mtaa fulani ulikuwa umejengwa kwa mpangilio. Leo hii,ujenzi wa ovyo,ndo chanzo cha kuharibika na kulalamika,serikali inalaumiwa kutofanya lolote. Serikali ni nani? Haya yote,ndo yanatengeneza wahuni. Unajua nini! Miaka ya nyuma kipindi tuisheni hazipo,walimu,walikuwa wazuri mno. Wakitegemea mishahara. Leo hii, twisheni ndo inalipa vizuri. Shule hawafundishi wanategeshea jioni na weekend. Ndo maendeleo haya?
Walimu wazoefu,wana somo la
Psychology (kama sikosei kuandika). Kila lika la umri,lina namna ya malezi na uelewa.
Hivi,uliwahi jiuliza kwa nini wenye uwezo mkubwa huwapeleka watoto wao kusomea nchi za nje? Wengine kwenye shule zenye mfumo wa nchi za nje?
Unadhani huko wanapokea tu!? Kwa nini wachuje!?