Tetesi: Shule ya wasichana ya Huruma iliyopo Dodoma yazuia wanafunzi kurudi likizo

Mleta mada nakuona umetawaliwa na unafiki kwenye hili andiko lako.

Nasema ni unafiki kwasababu, umedai shule haina walimu mahiri wameondoka, hivyo itakuwa ngumu kwa wanafunzi kutaka kuhama shule kwasababu ya muda mfupi uliobaki, hii taarifa umeileta kama fact, sio tetesi.

Nakushangaa taarifa za usagaji ulizozileta kama tetesi ndio umezi bold, umefanya hivyo ili kuonesha kwamba lengo lako hasa kuleta huu uzi ni nini.

Sasa kama una kiherehere cha kuripoti taarifa za usagaji wa hiyo shule, kwanini usingefanya uhakika kwa vyanzo vyako ili utuletee taarifa iliyokamilika, badala ya kuzikuza hizi tetesi kwa bold ili zionekane kweli?
 
Yan shule ifungwe kisa kusagana? Kwan shule imewaruhusu au kuwashauri wasagane? Chuki zako ni bure
 
Miaka ya zaman kumuoa mwanafunzi wa HURUMA GIRLS ilikuwa jumapili tuu english service misa ya pili kanisa paulo wa msalaba. Those gals were smart jaman kuanzia sare waliovaa hadi usomaji wa somo kwa english.

Kunani tena jamani huruma yetu imekuwaje????
 
Mbona mleta mada una chuki binafsi? Hoja yako ni nini? Ukosefu wa walimu hapo Huruma Sec ama usagaji,?

Hivi hujui kuwa shule za kikatiloki ndiyo zinaongoza kwa maadili? Huo usagaji upo kila shule hivi Sasa lkn hutakaa usikie shule ikiwaambia wazazi juu ya uwepo wa tatizo hilo ili kuepusha lawama.


Watoto nchi nzima wameharibika. Mtoe mwanao Huruma sec mpeleke sehemu nyingine lkn atasagwa tu
 
Kama ni kweli mbivu na mbichi zitaonekana mara baada ya taarifa hii
 
Huyu ni mwl aliyefukuzwa pale, shule nyingi za kikatoliki zimekuwa na timuatimua nyingi ya wafanyakazi wake hasa wale wenye tabia mbaya, kwa hali yoyote ile wewe ni miongoni mwao. Swali ni je? Wanasagana kidato cha 4 tuu??? Kijana tafuta ajira kwingine, kanisa katoliki halina nafasi kwa tabia mbovu kama zako.
 
taarifa yako imekaa kimaslahi, shule zinaendeshwa kwa utaratibu sio kirahisi kama unavodai,
umekadhia sana , walimu mahir : walimu katika shule binafsi huhama na pia watu wengine mahiri huja pia, hiyo ni taasisi haiendeshwi na mtu bali na mfumo

acha kuchafua shule za watu kijana haitakusaidia
 
Elimu ya Tanzania Haina msimamizi Kila mtu ni msimamizi !!! Hufanya anachojisikia .
Mfano utaratibu unasema shule zifungwe mwanafunzi apunzike,anaibuka mtu anasema shule haitafungwa na mamlaka zinafumbia macho
 
Kisa tu umetimuliwa kazi, ukaamua kuwasagia kunguni. Hiyo shule ni moja ya shule bora kabisa Jijini Dodoma. Hata hivyo vyombo vya dola vyenyewe vitakuwa vinakushangaa kupitia huu uzushi wako.
 
Mbona kubaki shule ni jambo la kawaida kwa madarasa ya mitihani ya kitaifa. Acha unafiki wewe
Huyu mtoa mada ana mambo ya kipumbavu sana. Hata shule za Kata zenyewe tu nyingi zimeshaitisha vikao na wazazi kwa ajili ya kuwachangisha michango ili wanafunzi wafundishwe wakati wa likizo!

Shule nyingi za ptivate nao zina utaratibu wa aina hii hii wa kuyabakisha madarasa ya mitihani wakati wa likizo kwa makubaliano na wazazi kuchangia gharama kidogo. Sasa huyu jamaa baada ya kufukuzwa kazi, hasira zake zote ameona azielekeze kwenye kuichafua shule.
 
Uko sahihi kabisa. Huyu mtoa mada anaonekana wazi alikuwa ni mwalimu anayejiona ni mahiri katika kufundisha, pamoja na wenzake wachache!
Kutokana na ujuaji wao uliopitiliza, shule iliamua kuwatimua. Na hapa ndipo tatizo lilipoanzia. Ukisoma maelezo yake, hata huwezi kuelewa kiini cha malalamiko yake.

Maana alitakiwa aje na shida moja tu kuu ya hiyo shule ili aeleweke! Kama ni usagaji (amekiri mwenyewe ni tetesi), kufukuzwa kwa yeye na wenzake (walimu mahiri), au kuwazuia watoto kurudi likizo (shule hufanya hivi kwa makubaliano na wazazi).
 
Muda unabadilisha MAMBO MENGI SANA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…