Tanzania Haina usawa,Kuna gepu kubwa sana Kati ya walionacho na wasionacho.
Ninaamini Kuna jambo linapikwa kupitia udini,na muungano.
Haya mawingu ni mosh utakao chini.
Acha uwake tu.
Ni kweli .
Kuna pesa nyingi sana zinaletwa na matajiri wa Kizungu na Waarabu .
Wazungu wanapitia misaada Kwa lengo kupata fursa za kuwashawishi watawala wagawe rasilimali za nchi Kwa mabeberu na masuala mazima ya Ushoga na usagaji. Zamani walianza kupitia kwenye dini ya kikristo Sasa Wazungu wanapitia kwa watawala na ma NGOs na Demokrasia.
Lakini Pia Kuna mapesa mengi sana yanayotoka Kwa waarabu kupitia dini ,ugaidi na madawa ya kulevya . Haya mapesa yanapitia Kwa wafanya Biashara wenye asili ya Asia kushirikiana pia na watawala yanaingizwa ambao wanageuka kuwa washishirika wao . Hapa pia dini ni kigezo.
Uchochoro unanza taratibu mwishowe unakua njia.
Pesa haijawahi kuiacha afrika na Dunia salama.
Lengo la matajiri wa kiarabu ni kushika uchumi wa Dunia kupitia rasilimali za Afrika kama walivyo wazungu.
Lakini Lengo la watawala wa Afrika ni kukaa mdarakani Kwa namna yoyote na kujilimbikizua Mali na familia zao. Uatasikia mitano Tena. Yaani Afrika mtu akawa makama wa Rais miaka sita na Rais miaka minne Jumla kumi lakini bado hatosheki anatafuta Kila mbinu na kuuza rasilimali zote za nchi ili tu apate pesa za kampeni na kushinda uchaguzi tuu.
Lakini Pia kulingana na umaskini wa Waafrika wengi na kutotambua kuwa Kila jamii duniani imewekwa sehemu yake na Mwenyezi Mungu Kwa lengo maalumu Waafrika wameaminishwa kuwa Dini za wazungu na Waarabu ni suluhisho la matatizo Yao huku wakiwa wanafarakana na kubaguana na kuchukiana na hata kuuana Kwa kugombania nafasi za Ahadi ya Kwenda mbinguni .
Mbaya zaidi matajiri na watawala wakishapata pesa za kutosha wanaamini kuwa wataenda pepoponi Kwa kufadhili harakati za kidini ziwe mbaya au nzuri.
Tusipokuwa na Katiba Bora inayowapa wananchi fursa ya kuchagua viongozi Bora Kwa manufaa ya Nchi yetu na Watu wetu hakika ipo siku tutachaguana Kwa misingi ya dini na makabila Kwa sababu watawala kupitia CCM wanachoangalia ni kutawala tu . Akiwa Rais Mkristo wanajifanya wapo bega Kwa bega na Wakristo na kuwafarakanisha kupitia Ukatoliki na ulokole.
Akiwa muislam CCM itatoa mpaka Ahadi ya Mahakama ya kadhi na Sasa wanawaahidi kuwa waarabu wakijaa hapa Tanganyika basi watu watapata vibarua au Kazi za kitumwa. Kutokana na umaskini watu wanawapa kura na wao wanafadhiliwa Kwa khanga na tishrt za chagua CCM Kazi iendelee.