Na mimi nimepata hisia kama hii, kwamba ni vigumu Makonda kuanza kusema maneno haya bila kupata ruhusa ya aliyemteua.
Kitaratibu, Samia alitakiwa kuunda upya baraza la mawaziri alipokuwa rais, na ama kumteua upya Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, ama kumuondoa na kumuweka mtu mwingine. Samia hakufanya hivyo.
Mpaka leo Samia amekuwa na Waziri Mkuu wa urithi ambaye kwa upande mmoja hajamuondoa kwenye hiyo nafasi, na kwa upande mwingine anaonesha kwamba "huyu si Waziri Mkuu niliyemteua mimi, nimeachiwa tu na Magufuli".
Anamfanyia mpaka hila za kumteulia Makamu Waziri Mkuu akionesha kwamba Majaliwa amepwaya.
Hamkupata message pale?
Waziri Mkuu alishahujumiwa hata kabla ya uteuzi wa Makonda.
Makonda amewekwa kimkakati kumuumbua zaidi tu.
Makonda kasema si yeye anayesema hayo, ni chama. Sasa unafikiri Makonda anaweza kuwa na ujasiri wa kusema haya ni maneno ya chama bila kupata ruhusa ya Samia? Kwa Waziri Mkuu?
CCM wanajivua nguo hadharani. Viongozi hawasikilizani. Maneno ambayo yalitakiwa kutolewa kwenye vikao vya ndani yanaanikwa wazi. Watu (CCM) wamestukia uchaguzi unakuja, wanatafuta mbuzi wa bangusilo kumtoa kafara tayari.