Si sahihi kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani, si kila kiongozi anaweza kupewa maagizo hadharani

Si sahihi kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani, si kila kiongozi anaweza kupewa maagizo hadharani

Anachokifanya Makonda ndicho haswa alichoteuliwa kukifanya.

Makonda ni mithili ya udongo, unamfinyanga vile unataka awe.

Makonda ni mouthpiece ya waliomteua ili aongee yale wasioweza kuyaongea kwa wanaotakiwa kufikishiwa ujumbe.
Umeongea point sana watu hawajui kazi ya makonda yupo kwa ajili ya kuludisha chama matumaini kwa wananchi watu mnamuona kama vile anamsema waziri mkuu ila nikama maigizo hayo wanafanya wana ccm ili muone kama chama hakiwaogopi viongozi ili wananchi muludishe Imani kwa chama
 
Waziri Mkuu ana majukumu makubwa na mengi. Anafanya kazi kubwa na nyingi. Anafanya kazi za chama chake-CCM na Serikali yetu. Tumheshimu Waziri Mkuu wetu....asitwezwe kwa mgongo wa chama na maagizo ya chama.
Sasa wewe mtu km ana uwezo wa kuwakata makofi mawiziri wakuu wastaafu (Mheshimiwa sana Jaji Joseph Sinde Warioba) bila uoga atashindwa nini kuwakata makofi mawiziri wakuu waliopo madarakani (Mheshimiwa Majaliwa Kasim Majaliwa)?
 
Tuende mbele na kurudi nyuma: Baada ya JPM watendaji serikalini wamejisahau sana!! Mama hawamheshimu, uuonevu makazini umerudi tena kwa kasi, ubadhirifu umerudi kwa kasi! Mabosi kuweka kikao ofisini na kula sitting allowance kumerudi kwa kasi!! Semina, warsha na makongamano yasiyokuwa na kichwa wala miguu yamerudi kwa kasi!! Uonevu kwa wananchi umerudi kwa kasi. Na vyote hivi vimeendelea bila mkemeaji!! Matatizo huko Ardhi hasa baada ya kuondoka huko yule waziri nguli, yamerudi upya!! Yote haya yanataka mtu jasiri, anayeweza kukemea na kuwajibisha kwa ujasiri na kufuatilia mguu kwa mguu kama Makonda!! Uwepo wa Makonda ni kete nzuri sana kwa CCM na kwa mama katika kurejesha tena imani ya wananchi kwa serikali yao, hasa tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025. Kwa dati kabisa ninapongeza sana uteuzi wa Makonda!!
NIPENDEKEZE: Makonda awe mgombea mwenza wa Samia kwenye uchaguzi mkuu!! Watanzania tutashuhudia namna makamu wa Rais anavyoweza kupiga kazi!!​
Watanzania wanapenda kuona watumishi wanateseka sijui hii wivu imetoka wapi .wakisikia hawaongezi mishahara wanashangilia kabisa .watumishi wanahaki ya kufanya kazi wakiwa wanaenjoy kuwa serikalini .nenda dunia nzima uone watumishi mpaka hapo kenya wanawekewa party kila mwezi wakifikia malengo.ndo maana vijana wenye akili mingi wanaingia serikalini miaka 5 wanatoka wanaanzisha kampuni za sheria serikali inashindwa kesi inapoteza mabilion .mkono advocate anaajiri best students wa sheria anawalipa mil 5 kwa mwezi na gari na kuwapangia mikochen kila 2 yrs wanaenda Soma nje wanarudi .siku bakhresa anabishana na tra anaajir mkono advocate wanaenda kukutana na maofisa tra wanaolipwa 1.3mil .ambao et hata wakipwa sitting allowance wanaonewa wivu na wananchi.bakhresa anashinda anaitia serikali hasara ya bil 30 ambazo zingetosha kujenga hospital za kisasa 6
 
"mtoto pendwa" wa SHUJAA karudishwa kundini baada ya kutengwa na kondoo zingine, sasa kapanda juu ya meza na kujamba mbele ya wageni!
😆😆😆 Kajamba mbele ya wageni Jr au sio?
Screenshot_20230816-151755.png
 
Nampenda sana Makonda kwa ule uthubutu wake, ila ni lazima ajali anayoyaongea anaposhika mic. Wakubwa wake wamueleze wazi ni mambo gani aongee na yapi aachie vikao vya chama. Ni lazema apewe ABCs, asiachwe hivi hivi. Mambo mengine yanaongeleka kwenye vikao vya chama.
 
Kuna namna Waziri Mkuu anapaswa kusoma alama za nyakati na kuamua namna nyingine. Kwanza ameletewa naibu hii nikusema kwamba hatoshi lakini pia hizi amri za Makonda zina baraka za aliyemteua. Ni fedheha mtu kama Majaliwa kupewa amri hadharani na Makonda jinsi ya kutekeleza majukumu yake.

Na akisema aondoke pia itakuwa nongwa, ataonekana amesusa, ametangaza vita na hao wanaomuandama. Busara ni kusubiria muda wake ufike (awamu iishe), basi astaafu.
 
Mama Samiah naye mnafiki, alisahuriwa na TLS ateue Waziri Mkuu Mpya Kama ni awamu mpya akakataa, Sasa hivi anatumia njia ndefu kumtoa, mara huku dotto kule Makonda, kesho sijui atakuja na Nini.
Na waziri mkuu nae kin'gan'gizi balaa kama kupe!![emoji2]
 
Mi naona kama utovu wa nidhamu. Waziri mkuu ni kiongozi mkubwa hapaswi kuagizwa kufanya jambo fulani na katibu muenezi wa chama. Serikali ni kubwa kuliko chama. Kuna nchi rais wake anaweza kuachana na chama chake kilichomuingiza ikulu na akaanzisha chama kingine huku akiendelea na urais wake
Hata hapo Malawi ilifanyika hivyo !
Rais alianzisha Chama chake akiwa Ikulu !
 
Na mimi nimepata hisia kama hii, kwamba ni vigumu Makonda kuanza kusema maneno haya bila kupata ruhusa ya aliyemteua.

Kitaratibu, Samia alitakiwa kuunda upya baraza la mawaziri alipokuwa rais, na ama kumteua upya Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, ama kumuondoa na kumuweka mtu mwingine. Samia hakufanya hivyo.

Mpaka leo Samia amekuwa na Waziri Mkuu wa urithi ambaye kwa upande mmoja hajamuondoa kwenye hiyo nafasi, na kwa upande mwingine anaonesha kwamba "huyu si Waziri Mkuu niliyemteua mimi, nimeachiwa tu na Magufuli".

Anamfanyia mpaka hila za kumteulia Makamu Waziri Mkuu akionesha kwamba Majaliwa amepwaya.

Hamkupata message pale?

Waziri Mkuu alishahujumiwa hata kabla ya uteuzi wa Makonda.

Makonda amewekwa kimkakati kumuumbua zaidi tu.

Makonda kasema si yeye anayesema hayo, ni chama. Sasa unafikiri Makonda anaweza kuwa na ujasiri wa kusema haya ni maneno ya chama bila kupata ruhusa ya Samia? Kwa Waziri Mkuu?

CCM wanajivua nguo hadharani. Viongozi hawasikilizani. Maneno ambayo yalitakiwa kutolewa kwenye vikao vya ndani yanaanikwa wazi. Watu (CCM) wamestukia uchaguzi unakuja, wanatafuta mbuzi wa bangusilo kumtoa kafara tayari.
Mtafaruku Chamani !! 2025 inaleta mazonge 😅😅🙏🙏
Ngoja Tusubiri tuone “Karma” !
 
Back
Top Bottom