Huwezi kuacha kuji
Hushiaha
Siasa ni Pana sana,ni zaidi ya uchaguzi,vyama vya Siasa,ubunge,nk,Siasa za nchi ndio zinashawishi taasisi gani za kiuchumi zianzishwe,na zitende vipi,,Siasa ndio zinaamua nani awe na nguvu ya kiuchumi,na kwa eneo lipi,Siasa ndio Zina control njia za uchumi,na kuamua wananchi wawe maskini au matajiri,usifikili Samsung na hyundai kutokea Korea ya kusini badala ya kaskazini ni jambo la bahati tu,mazingira ya kisiasa yaliyopo kusini ni wezeshi kwa ujasiliamali kuliko Yale ya kaskazini kwenye ujamaa wa kidikiteta usiotaka private ownership wa njia za kiuchumi.
Kenya kuwa na uchumi mkubwa na makampuni mengi kuliko sisi,sio bahati,Siasa zilifanya hivyo,ujamaa wetu haukutaka ubunifu binafsi,na mtu mmoja mmoja kumiliki njia za uchumi,Kenya ubepari ulipewa nafasi,watu waliruhusiwa kushika njia za kiuchumi na kukusanya ukwasi kadri wawezavyo.
Kwahiyo ukiacha kujihusisha na Siasa,unakuwa unataka kufa na kuzikwa,Siasa sio ccm na Chadema,nccr na Samia,na ubunge,ni zaidi,ni maisha ya kila siku.