Hero,
Mkuu
Naelewa unachosema
Grading katika vyuo vyetu ni tatizo,hilo tunalijua!
Sasa tuende wapi?Tupimeje sasa?Mbadala hatuna
Ni lazima tutumie GPA!
Cha msingi labda tudhibiti upimaji wa GPA zetu uwe bora,hilo ndilo suluhisho!
Na kuhusu kua eti mtu hana GPA nzuri ila anajua sana udaktari ni kweli ni kama fundi wa umeme wa mtaani au gereji anajua kujenga magari zaidi ya engineer wa Motor Vehicle Engineering ila kwanini tunamchukua engineer huyo kufundisha kuliko huyo fundi mtaani?
Ni kwa sababu ana ubongo wa kufanya analytical skills na kuchakata information zaidi ukimpa kitabu ana uwezo wa kusoma na kuelewa na kufundisha watoto
Ila fundi ukimtoa kwenye topic yake kidogo unampoteza!
Pia mwenye GPA kubwa anauwezo wa ku-link concepts za udaktari na other disciplines ina broader view maana anaweza elewa information nyingi na kuzifanyia analysis
Unajua hawa madaktari-uzoefu na mafundi-uzoefu mpo overrated sana...Na kuna mahali mnachanganya mambo kabisa...Mnadhani uzoefu wako wa wodini ndio ultimate ,kumbe mnashindwa kuelewa kabisa kwamba knowledge ya wodini jumlisha na other societal concepts na mambo mengine kibao ndio wanafundishwa watoto
Pamoja na hayo,daktari-uzoefu yupo limited na practicals zake tu huko wodini wakati kumbe udaktari ni mlolongo wa kibao ya ndani ya wodi na nje ya wodi
Wanaoweza ku-handle ndani ya wodi na nje ya wodi ni waliopata GPA kubwa tu..ndio maana mawaziri wa afya au wakuu wa mahospitali ni watu wenye GPA kubwa au wakufunzi wa vyuo vya utabibu ni watu wenye GPA kubwa tu,huwezi kuweka chini ya hapo mkuu