Siasa za kindugu, umwagaji damu na Ukatoliki nchini Ufilipino

Mi nasaidia kujibu moja kwa sasa,

Walivyoshtakiwa kwa papa, badala ya kujibu kistaarabu wao wakawatukana wenzao
Huu ulikuwa ni udhaifu

TEC wanatetea haki yako, maisha, uhai wako, uhuru wako wa kujieleza na uhuru wa hao vijana kujieleza. Fr Kitima hajasema kitu chochote kibaya hajamtukana Samia au mtu yoyote.

Nyuma Kidogo walimpiga na Nyundo wakitaka kumuua.

Hoja ya wale vijana unaweza kuiitaje? Na hao vijana utawapa jina gani?
 
TEC imefanya makosa mengi sana tangu kuanzishwa kwake. ​
Taasisi yoyoymte ya umma inayoendeshwa na binadamu kufanya makosa ni kawaida.

Hata wakati Mwinyi anakuwa Raisi kuna baadhi ya viongozi walimfuata Nyerere kusema kwamba huyu mbona ni Muislamu.​
Hao baadhi ya viongozi ni kina nani?
Viongozi wa kisiasa au Kikatoliki?
Ushahidi uko wapi?

Nyerere alifanya nchi hii SECULAR.

Hivi kungekuwa na nia mbaya, angeifanya nchi ya kikatoliki na ingekuwa hivyo mpaka leo. Wakati wa Mwinyi alikuwepo, liliwezaje kutokea?
Nyerere akasema mimi mbona Mkristo nimetawala miaka zaidi ya 20 hamkuniuliza ??? ​
Ushahidi wa hili uko wapi?

Ushawahi kutokea mvutano mkali TEC na MUSLIMS hapa Tanzania kuhusu , Mzee Nyerere akasema hawezi kuwaonea haya Wakristo kwenye baadhi ya mambo na kuwakemea vilivyo. Mbona haya hamtaki kuyasema, au ndiyo SELECTIVE OUTRAGE ???​
Mvutano kuhsu nini?

OIC na Kadh courts?

au kuhusu nini?

Na tangu lini TEC wamewahi kujibizana na MUSLIMS?


Kwahiyo mapambano ya Magufuli yalikuwa dhidi ya ACACIA na siyo MIKATABA ya MADINI???
 
Huyu KIBUYU hana MAJIBU.
 
HAPANA kuhusu MIGA lilikuwa ni suala la Acacia siyo Winshare.

Magufuli alifuata utaratibu wote wa kisheria ambao umewekwa.

Kuhusu kuwa bayana mbona mazungumzo ya Lissu na Nyanda kwamba JPM kashinda kwenye hili huyasemi. Alitumiwa ujumbe kwenye WhatsApp Group kuhusu matokeo yote ya hili na jumbe zake zikawekwa Online na wote tukaziona. Lissu mwenyewe akasema hivi "Okay Brother you win", mbona unataka kukanusha ambacho Lissu mwenyewe alikiri ???

Mtafute Nyanda atakupa zile SMS za Lissu kukiri.
=====================================================================
Kuhusu TEC sasa: Ni lazima niwalete Mkapa, Mwinyi na Nyerere kwasababu ili kupima uhalali wa madai ya Samia anaposema kwamba anakosolewa kwasababu ni Muislamu. Nikauliza kwani TEC hawakuwahi kuwakosoa watawala wa Kikristo na wengine na waislamu huko nyuma ????

Nikaenda mbali na kuzungumzia dhana nzima inayozunguka na kusema Mzee Nyerere hakuwahi kukosolewa na TEC. Nikasema wazi kwamba alishawahi kuvutana nao, ilhali yeye ni Mkatoliki kindakindaki. Nikataja na Mzee Mkapa ambaye naye ni Mkatoliki kindakindaki. Nikataja Mwinyi na Jakaya ambao nao pia waliokosolewa lakini hawakuwahi kutumia karata ya udini kama Samia. Nashukuru umemzungumzia JPM na TEC.

Sasa hoja zangu za msingi ni hizi:

Mosi: Je, TEC wanamping Samia kwasababu ya Uislamu wake ???

Pili: Je, TEC hawakuwahi kuwapinga maraisi wakristo ???

Tatu; Je, ni sawa kutumia makosa ya zamani ya kanisa kupinga Samia kukosolewa ???

==================================================================
HALAFU NAMALIZA: A Bigger Picture, hivi unadhani hata kama Samia akiondoka madarakani huu mvutano utaisha. Unaamini kabisa kwamba unaweza kucheza na dini halafu yasiyokee madhara ???

Huu mvutano wa TEC vs BAKWATA vs CCM unadhani una afya kwa usalama wa taifa na kanda yetu hii nzima ???

SWALI CHOKONOZI: Hivi mbali na haya mauaji ya kikatili yaliyofanywa na Samia, unadhani madai ya waislamu ya muda mrefu dhidi ya Kanisa Katoliki yanaweza kuwa na uhalali wowote ule ??? Kwamba Waislamu hawajawahi kukosewa ??? AU kila kitu wenzetu huwa wanatunga na kulalamika tu ???


​
 
Kuna kakikundi (proven CCM Mtandao) cha Kikwete na Rostam Aziz kimeshanunua kila taasisi ya umma na media na JESHI.

Wameshapanga safu yote ya BUNGE, na MADIWANI.

Taasisi pekee iliyobaki kwasasa ni TEC, kwasababu haina NJAA ya PESA na MADARAKA.


Ndio maana unaona MASHAMBULIZI UCHWARA yanaelekezwa kwao kwasasa.

Na bahata mbaya hivi vikundi vinavyoweka wanasiasa madarakani, huwa vinatafuta "THE MORE DUMBEST POLITICIANS" ndio vinawapa madaraka ili vipige vizuri.
 
Twende taratibu na ushahidi.

MOSI: Tunaanza kabisa na MCHAKATO WA KATIBA. Nani alikuwa mtu wa mwisho kuuvuruga kwa kutumia nafasi yake ya UASKOFU ??? Ni Mzee wetu Askofu Kadinali Pengo, ambaye hata baada ya wenzake kusema wanaunga mkono serikali tatu, yeye aliitisha waandishi wa habari na kusema anatoa maoni yake binafsi.

Kadinali Pengo alisema kwamba anaunga mkono Serikali Mbili na huo ndiyo ukawa mwisho wa mjadala. TEC walikuwa na msimamo wao na kanisa linaongozwa na TEC siyo Kadinali, lakini hawakudiriki kupingana naye. Je, yale maoni ya Kadinali pengo yalikuwa ni ya mtu binafsi au madaraka yake yalitumika vibaya ??? Je, alikuwa sahihi kufanya vile ??? Alifanya vile kama nani na kwa malengo yapi ???

Historia ya nchi itabaki kukumbuka kwamba Kadinali Pengo alitumia nafasi yake kuhujumu mchakato wa KATIBA. TEC walitoa msimamo wao, baadaye Pengo akatoa msimamo wake. Msimamo wa Kadinali siyo tu ulivuruga Mchakato wa katiba, bali pia ushawishi wa Mzee Pengo na Mkapa ndiyo ulisaidia CCM kubaki madarakani mwaka 2015 kwa kumuweka kijana wao wa Seminari JPM.

NDIYO, hili hatuwezi kulisema lina ukakasi sana
==================================================================

PILI: Mwaka 2014 nchi inahujumiwa kwa ufisadi wa kutisha ulioshusha thamani ya sarafu yetu, taasisi za Kanisa na Maaskofu walihusika. MKOMBOZI BANK chini ya MAMA LUPEMBE a.k.a Mrs Alan Mbunda walitakatisha (Launder) MABILIONI ya fedha za TEGETA ESCROW bila kufuata sheria za kibenki. Maaskofu walipewa mgao huo, mfano Father Kilaini alipewa zaidi ya Milioni 400 na Rugemalira.

Dr Wilbroad Slaa alienda wazi-wazi kukosoa kanisa kwa kusema "Inasikitisha kuona watumishi wa Mungu wanafanya ufisadi". Hili halikuzungumzwa sana wala hakuna waraka wowote wa TEC ulitolewa na hakuna Askofu aliyewajibishwa. Father Kilaini alipohijiwa alisema "Mbona hizo ni fedha ndogo, Rugemalira huwa anatoa sadaka kubwa zaidi ya hiyo". Wote tunafahamu kwanini hili halikuzungumzwa sanaa.
====================================================================

WALOKOLE waliwahi kuleta UTAPELI WA DESI ikala kwao na walikamatwa. Kwanini MKOMBOZI BANK, ambayo ni taasisi ya kanisa haijawajibishwa mpaka leo hii kwa ufisadi mkubwa kiasi kile ??? Kwanini Maaskofu waliokula pesa za wizi hawakuwajibishwa ??? Hivi angefanya Sheikh Zuberi yale ya Mkombozi kipindi cha utawala wa JPM angepona kweli ???

========================================================
TUJADILI TARATIBU...




​
 
Ni hivi, kwanza nchi nyingi ulizozingumzia zinatutugemea kwa usalama karibia zote tayari zimepitia au bado zinaendelea kupitia machafuko ya kisiasa, ugaidi na hata vita vye wenyewe kwa wenyewe kwa hiyo sisi hatujawa na msaada wowote mkubwa wa maana kwa usalama wao, labda kuhifadhi tu wakimbizi wao kwa muda, hivyo hoja yako kuu ya kwamba sisi ndio tegemezi kwa usalama ukanda huu inakosa mashiko na inakafua kifo cha mende.

Pili, kama Waislamu wa Tanganyika wamesoma na kupelekea kuwa wauangwana tofauti na wa sehemu nyingine za Africa basi ni kwa sababu ya juhudi za Nyerere kuhakikisha raia wote wa nchi hii wanaelimika kwa usawa bila ubaguzi au ukanda na akaonyesha mfano kwa kuchukua shule karibia zote za makanisa na kuzifanya za umma.
Hata hivyo uungwana wa Waislamu kutokana na kuelimika inaweza kuwa ni sababu mojawapo katika sababu nyingi zilizoondoa hamasa ya ugaidi Tanzania kwani sababu za Ugaidi ni complex sana, nyingi na zenye mchanganyiko wa mambo mengi, mfano Ugaidi wa Somalia ulianzia na utawala mbovu wa mabavu na ubaguzi wa kikoo na kikanda wa Mohamed Siad Bare pamoja na mauaji ya kimbari ya Isaaq( Isaaq Genocide)

Ugaidi wa Nigeria chanzo ni siasa za ubaguzi wa kikanda, siasa mbovu kiujumla zisizo na utulivu, ufisadi uliokithiri unaowanaufaisha wachache huku mamilioni wakiachwa katika hali duni sana za maisha na hao ndio wanakuwa kivutio cha magaidi. Ninaweza kuendelea kila nchi na sababu zake mahususi za ugaidi na jinsi gani mazingira hayafanani kabisa na Tanzania.

Mengine kuhusu CIA kupewa au kunyimwa taarifa na TISS ni conspiracies tu au story zisizo na mashiko. CIA wakizitaka taarifa za ugaidi kwa yeyote na sehemu yoyote watazipata tu kwa njia rahisi au ngumu, kwa ushirikiano rasmi au hata kwa vipenyo wao ambao hata ni TISS na ni sehemu ya jamii kabisa.
 
Kuna kitu kinapikwa,

Padre Kitima aongezewe ulinzi na waombaji tuongeze bidii kuomba.
Nikupashe na kukumbusha kingine.

Vita dhidi ya WAKATOLIKI imeanza rasmi kipindi cha JPM.

Father Ngalalekumutwa alikimbiza mapadri wengi nchini kwenda kusoma nje kwasababu walikuwa wanawindwa na JPM. Akiwa Iringa anafanya mazungumzo na baadhi ya makada wa CHADEMA alisema bayana kabisa, kwamba "Huyu kijana siyo yule ambaye tulikuwa tunamfahamu seminari"

Kuna mambo yalikuwa yanafanyika hatuwezi kuyasema hadharani. Ila wengi tulimkosoa sana JPM na watu kama ninyi mliturushia kejeli na kashfa. Ila hata Samia akiondoka haya mambo hayawezi kuisha.

==================================================================
​
 

Wamejipanga vizuri, wanataka kumaliza kazi kwa namna yoyote ile kuzinunua,kuzitisha, kuzinyamazisha su kuzifungia taasisi huru chache zilizobaki kama TEC, mitandao.

Kama ume- notice hapa JF wamemwagwa, na kununua chawa wengi sana kuanzia kama miezi sita iliyopita. Wengi wamebadilika ghafla badala ya maoni ya kujenga sasa hivi wanajaza vitisho, matusi, kejeri, kebehi, dhihaka, kudanganya, kupindisha ukweli, kubadili ukweli, kuharibu mada na propaganda zingine nyingi tu.
 
Sasa mtu kaua, umekubali kaua, Wakatoliki wamemsema kaua, halafu unawalaumu Wakatoliki wadini?

Mimi ni atheist siamini katika kuwepo Mungu, lakini kama udini ni kuwasema wauaji, udini huu nauunga mkono.
 
Jikite kuthibisha shutuma zako dhidi ya chombo rasmi, taasisi inayowakilisha wakatoliki Tanzania. Hao ndio uliowashambulia.
 
Elimu ni REASONING na kile unachofanya.

Siyo makaratasi ya vyuoni, ambayo sikunhizi yanauzwa.

Waislam wana uvumilivu wa juu kwenye nini?

Tunapenda kuwabagaza sana Waislamu wa Tanganyika ila ukweli ni kwamba ndugu zetu wana kiwango kikubwa cha Tolerance kuliko hata Zanzibar. ​
Nani anawabagaza?
Kuhusu nini?

Wakristo waliruhusu Waislam.kuchinja ili watu wote wale?

Au unafikiri Wakristo hawawezi kuchinja?

Katika hili, huyo Mkristo na Muislam ni nani ana uvumilivu wa hali ya juu?

Zanzibar hakuna uvumilivu wa kidini.

Kuna DAMU ZA KIARABU (CUF), na ASP (CCM) na kwasababu watu ni wachache wamepigwa sana na kutengwa na hivyo kulazimika kutii.
Ukienda hata Nigeria huwezi kukuta ushirikiano mkubwa baina ya Wakristo na Waislamu kama ilivyo hapa nchini Tanganyika. Kule Zanzibar Wakristo wanabaguliwa mno na waislamu.​
TZ ina misingi yake, ambayo ndio matokeo ya amani iliyopo.

Misingi hiyo Nigeria haipo.

Hiyo misingi TZ , imetikishwa ndio maana tumefikia stage JWTZ limegeuka kuua wananchi wake wenyewe.

  • TZ haina vikundi vya waasi kwasababu sote tulikuwa tunajua madaraka yanapatikana kwa njia ya kura
  • TZ ilikuwa na amani kwasababu sote tunanua, mtu akiwa na kosa anakamatwa na polisi na anapelekwa mahakamani.
  • TZ tulikuwa na amani kwasababu sote tunajua mali ya umma ni kwaajili ya umma.

Yote haya kwasasa yamekufa.

Mwisho wa siku tutakuwa kama DRC, watu wataanza kuamini madaraka yanapatikana MSITUNI.

Huu ni UPUMBAVU.

Mitandao ya kigaidi haikufanikiwa TZ, kwasababu watu walilipenda taifa lao na walilinda. Ili mtandao wa kigaidi ufanye kazi, ni lazima wananchi wako wahusike.

Leo umegeuzia bunduki wananchi wako?

Wasipokupa taarifa, utapambana vipi na huo ugaidi?

Miaka ya 2000's wakati ugaidi umeshamiri kwenye ukanda wetu TISS ilisaidia mno kuimarisha usalama kwasababu ilikuwa na taarifa nyeti kuhusu mitandao ya waislamu wenye msimamo mkali kwenye ukanda huu. ​

Hakuna TAASISI TAKATAKA nchi hii kama TISS.

Hakuna wanachojua.

Tunafanya nao kazi kwenye ofisi za DCs, RCs na wengine ndugu zetu tunawajua.

Wana taarifa nyeti????
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

TISS???

πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…


Lala tena uendelee kuota.
Watu kama Balozi Adadi Rajabu ambaye ni Muislamu kindakindani ndiyo walikuwa vinara wa kupambana na magaidi. CIA na MI6 mpaka leo hii wanategemea taarifa kutoka TISS kuhusu mitandao ya kigaidi.​
Huu upumbavu kasimulie wajukuu zako.

Marekani walipoanza kuvutana na Magufuli, aliwaambia TISS waache kuwapa CIA taarifa za kiintelijensia kuhusu makundi ya kigaidi ukanda huu. Huu ni ukweli ambao wengi hamuujui. ​
Kasimulie wajukuu zako huu upumbavu.

Illusions.
CCM kwanza ilishakufa.

Kuna Dola.

Ndio maana mitaani huoni CCM ikifanya siasa.

Unaona JWTZ, TISS, UHAMIAJI, POLISI, TCRA, TRA, etc
Hizi ni AKILI ZA KIZEZETA.
ZEZETA
 
Mkuu Malcom, hii mada yako ngumu kidogo na ni mkuu Lord Denning ndie amekupata uzuri mtatuelimisha uzuri.

Na hilo la mgosi Adadi Rajabu lifanyie utafiti kidogo maana huwa anasali pale St Albans Anglikana na mie huwa nasali pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…