Kwa mtazamo wangu naona, kila kitu kinaanzia kwa mwanaume, au kama ni mwanamke ndio anatafuta wa kuolewa nae basi, itaanzia kwake,
1. Tuanze swala la bikra, Naamini mwanamke kutokuwa na bikra sio sababu ya msingi mkashindwa kuishi maish ya amani, maana maisha ya amani katika ndoa hayaletwi na ngono pekee yake, kuna tabia ya mtu, dini, malezi, tv anazoangalia, na mambo mengi tuu, pia hapo ikumbukwe bikra hutoka kwa njia tofauti tofaut sio ngono pekee yake, na mtu kuwa bikra haimaanishi hajawai kuwa kwenye mahusiano na wanaume pia
Basi tuje kwenye swala la msingi kuhusu bikra, kwanin nasema inaanzia kwako wewe mwanaume, ni kuwa wakati wewe unataka mwanamke mwenye bikra wewe unayo hiyo bikra? kwanin nasema hivyo, wakati wewe ukioa bikra na wewe sio bikra, pia itakua ni matatizo vile vile ndani ya nyumba, kwani tunajua mwanamke bikra hajazoea kufanya ngono muda mrefu na mara kwa mara, vipi wewe sasa na experience yako ya miaka 10 ya kufanya ngono Gia ishatumika mpaka inahitaji busta kuzunguka, ukiwa unahitaji mara kwa mara na akasema akasema hajazoea, utaenda nje ya ndoa kutafuta bikra mwingine ama utarudi kwa hao mnaowaita malaya, (kwanini usioe haohao mnaotoshelezana sasa ili upewe unavotaka) na ukitoka nje ya ndoa hujatatua tatizo pia kumbuka.
2. Tukija kwa upande wa umasikini ni vile vile wakati unataka kuoa kwenye familia za kitajiri au mwanamke tajiri, unasemaje wew kwa upande wako, ni tajiri? familia yako ni ya kitajiri (hawakumbatii umasikini?) mimi na nyinyi wote tumeshashuhudia mwanaume akiteswa na kunyanyaswa kisa mwanamke ana kipato kuzidi huyo mwanaume, humajawai kusikia msemo unaosema mwanaume anaweza kuishi na mwanamke asie na kazi kwa miaka 5 ila mwanamke awezi kuishi na mwanaume asie na kazi kwa siku 5? kama unatak kuishi na familia ya kitajiri basi hakikisha na wew ni tajiri wa kuzidi, na ukiwazidi tunarudi pale pale, kuwa lazima majukumu yatakuepo kwa upande wa wakwe, sasa usitake nikuelezee majukumu yana ghalama kiasi gani kwa hao matajiri, pia nakubaliana na kuoa familia za kimasikini unaweza ukaonekana kama ndio mkombozi wao wa kuwatoa kwenye janga lao la umasikini, lakini sio wote, sio familia zote zipo hivyo, na hata kama kuna hela unatakiwa kuwapa hiyo familia usichukulie kama wanakumola ila chukulia kama ni moja ya familia na unawasaidia kama mmoja wa wana familia, em jichukulie wew ndio mkwe sasa na binti yako kaolewa usingependa usaidiwe kwa namna moja au nyingine? kwani wew pamoja na hela zako zilizo wazidi unahisi hamna siku utataka msaada kutoka kwao? maisha ni kusaidiana jamani, pia wanaume msichulie kila siku kuwa mnatumika kwenye hela zenu, maisha ya sasa yamebadilika, mahitaji ni mengi sana, kwa kila mtu, hivyo ni vyema kusaidiana kwa hapa na pale inapobidi, ila msaada usizidi uwezo wako, hivyo basi weka bayana kwa mwenza wako kiasi unachopata ili kusiwe na chuki pale unashindwa kumpa mtu hela
MWISHO.
Ndoa bora na imara huja kwa kupitia wanandoa wanaohusika na sio Baba mkwe, mama mkwe, shemeji wala wifi, Biblia inasema atatoka mtu mmoja kwenda kuungana na mwenzake nao watakua mwili mmoja, aisemi atatoka na shemeji wala wifi wala mkwe, na ndoa hudumishwa Upendo, uvumilivu, kutokua na husuda, pasipo masengenyo, furaha ya wawili. Ndoa haidumishwi na Mali (mnahitaji Mali ila sio mali pekee itafanya mdumu), uchoyo haufai katika ndoa, Ndoa haidumishwi na bikra, kama mkeo ni malaya ni malaya tuu haijarishi ulimvunja bikra ama la. (maana hata malaya alizaliwa na bikra), kama mkeo ni malaya hata ukimvunja hiyo bikra ataendelea kuwa malaya, kwani nyinyi hamjasikia malaya wenye bikra?
Hapa muhimu Tunatakiwa tumuombe sana Mungu ili tunapochagua mwenza wetu awe ni yule ambae tumepewa na Bwana na sio hawa tunawaangalia kwa macho tuu na kuwatani kwa shepu walizonazo, sura au wanavojipamba, vifua, pesa, magari na mengine mengi.
Bikra au pesa havitakupa ndoa bora, bali inaanzia kwako kama utaendana na hiyo bikra au huo utajiri