Uchaguzi 2020 Sijauona ‘u-kibaraka’ wala ‘ubeberu’ kwa Lissu mpaka sasa

Uchaguzi 2020 Sijauona ‘u-kibaraka’ wala ‘ubeberu’ kwa Lissu mpaka sasa

Najaribu kuutafuta Ukibaraka wa Lissu siuoni.

Nautafuta Ubeberu wake siuoni.

Nampekua na namchimba zaidi ninachokiona ni kua Tundu Lissu ni Mzalendo wa Kweli na wa kuigwa.

Eti oooh, anatumika na Wabeligiji, swali la kujiuliza hapa Je, Lissu alifikajefikaje huko Ubeligiji (Jibu Risasi zenu ndio hatimaye zilimfikisha huko)

Eti oooh, anataka Migodi yetu na Madini yetu yachukuliwe na Mabeberu (Hivi Mnajua halakati za Lissu katika kupambania Madini yetu na Migodi yetu?)

Nasema tena Lissu ndio Mzalendo wa kweli namba moja Tanzania hii, sisi wengine ni Wanafiki tu tena Wanafiki Uchwara.

Tusikalilishwe kila kitu. Mengine Tuhoji.
Nyongeza ya wanaodai anataka wauze madini yao kwa wanaowaita mabeberu hebu waulize, kwani sasa hivi hiyo migodi inamilikiwa na nani?

Na je hayo madini wakiyachimba wanayauza wapi?

Tukianza na Barrick, Geita gol mine, nk. Je wakichimba hayo madini wanaizuia serikali ya Tanzania?

Wanaochimba ni Mababeru na wakiyapata wanayapeleka kwa Mabeberu wenzao. Hivyo kelele zao juu ya Lissu hazina maana hata kidogo.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
 
Wamkopeka ,

..kuongeza kwenye maswali yako.

..Walitunga na kupitisha sheria za madini zinazotunyonya ni wana-CCM.

..Waliosaini mikataba mibovu ya kisaliti ni watendaji wa CCM.

..Watanzania waliotumikia ktk nafasi za juu ktk makampuni ya madini baadhi yao ni viongozi na wagombea wa CCM.

..Dr.Kalemani aliwahi kuajiriwa na moja ya makampuni ya madini.

..Deo Mwanyika, mgombea wa CCM Njombe, alikuwa CEO wa Accacia hapa Tanzania, VP wa Africa wa Barrick.
 
Wote hawa ni wanyonyaji
 
Utauoje na wewe unatamani kuwa kibaraka wa mabeberu
Najaribu kuutafuta Ukibaraka wa Lissu siuoni.

Nautafuta Ubeberu wake siuoni.

Nampekua na namchimba zaidi ninachokiona ni kua Tundu Lissu ni Mzalendo wa Kweli na wa kuigwa.

Eti oooh, anatumika na Wabeligiji, swali la kujiuliza hapa Je, Lissu alifikajefikaje huko Ubeligiji (Jibu Risasi zenu ndio hatimaye zilimfikisha huko)

Eti oooh, anataka Migodi yetu na Madini yetu yachukuliwe na Mabeberu (Hivi Mnajua halakati za Lissu katika kupambania Madini yetu na Migodi yetu?)

Nasema tena Lissu ndio Mzalendo wa kweli namba moja Tanzania hii, sisi wengine ni Wanafiki tu tena Wanafiki Uchwara.

Tusikalilishwe kila kitu. Mengine Tuhoji.
 
Aisee mimi pia nimetumia hadi miwani lakini hiyo mambo sijaiona! So nimepotezea maana nimegundua kuna watu wamefilisika hoja sasa wanadaka na kudandia chochote ilimradi kiwasaidie kuongeza maneno ya kuongea!
 
Wakati mwingine ni vizuri kujua nafasi yako, Yuko wapi Kashogi? Vipi kuhusu Julian Assenga wa WeakLeaks? Wewe unapiga kelele na hakuna unachofaidika nacho zaidi ya kutafuta umaarufu wa kijinga.

Haya Tujikumbushe Snowden licha ya alichokipata baada ya kuituhumu serikali inachunguza mawasiliano ya wananchi, sasa anaishi maisha ya hofu na bado hamna uhakika kama aliyoyapinga kama hayatendeki. Kwa hiyo wakati mwingine ni vizuri kujua nafasi yako na usipende kushindana na mamlaka.
We ndio mjinga, sasa mamlaka zikiua na kutesa wakosoaji ziachwe tu, kwasababu Snowden anaishi uamishoni?!

Mbona ulimsahau Nelson Mandela kwenye idadi za wakosoaji wako?!
 
Baada ya Nyerere mzalendo wa pili ni Lissu,nasema kutoka moyoni sina maslahi yoyote na chama chochote cha siasa au mwanasiasa yeyote ndio maana nasimama katika ukweli.
Acha ujinga wewe, huyo Lissu unayesema ni mzalendo namba mbili na Nyerere mzalendo namba moja iweje Lissu amtukane Nyerere? Au hujui Hilo? Huyu Lissu Ana laana mbaya Sana toka kwa mzalendo namba moja Nyerere.
 
Ilianzishwa operation ya ukaguzi wa siraha zinazomilikiwa na raia,hivi kwa fukunyuku la mwenye akili achana na siasa uchwara lengo lake kuu ilikuwa nini hasa.

Na baada ya hapo kama mnakumbukumbu nini kilianza kufanyika .Na nina imani udhalimu ndo ulipamba moto ka sikosei.ila uzuri watz huwa tunasahau mapema.

Hata swala la TL asingejisimamia yeye kama yeye angesahaurika.hii TZ bhana.

Kwa hiyo mwacheni anaowaeleza wanamwelewa,sio kwba anakueleza wewe ili umsaidie Bali yawezekana anakueleza ili uone aibu kwa nia ovu uliyonayo juu yake.Wenye nia njema kwake wanamwelewa.

Kwa taarifa yenu sasa,kwa mda huu hata Rais hana chakumfanya.viva TUME viva WATEULE.Wanasafari ndefu kwenye kampeni.

Sidhan kama kuna MTU anaeipenda nchi hii kama TL.

Eti beberu,unapost,unamwona,unatukana,unakebehi kwa kutumia vitu vya mabeberu.
Ifikie hatua tuone aibu jamani.
Umeajiriwa haijarishi,unaishi kwenu haijarishi.
Tunahitaji maendeleo ya wote na si ya wachache.
MPE haki yake mnyonge kabla hujanyonga,ili akuulize kwa nn unataka kumnyonga.

Wengi tu MAJUHA,ila hatujielewi.
Nchi niya wote,

Siasa haifi,ila mwanasiasa anakufa.

Ngoja nikanywe zangu mbege kwa mama D.loading
 
Baada ya Nyerere mzalendo wa pili ni Lissu,nasema kutoka moyoni sina maslahi yoyote na chama chochote cha siasa au mwanasiasa yeyote ndio maana nasimama katika ukweli.

meanwhile lissu alitoka kumtukana nyerere
 
Mzee labda unamzungumzia Lissu wa enzi ya Dr Slaa huyu Lissu wa sasa mzee wa Miga ni tofauti sana na Lissu wa Slaa leo ukizungumzia mzalendo wa Nchii hii kati ya Lissu na JPM hata mtoto mdogo anajua nani ni mzalendo mzalendo si maneno ni pamoja na vitendo leo Mwenye nyumba wako aje kutembea na mkeo na kuchukua chakula cha watoto wako ukaogopa kusema kisa utapewa notice huyo ndo Lissu aliyesema tutapelekwa mahakamani kwa kuwakataza wazungu wasiibe na kuchukua madini yetu but JPM alisimama kidete na kutetea hakujali kama kuna Drone zinaweza kutumwa au kupelekwa mahakamani leo hii tuna kampuni ya Twiga

Leo unafurahia Uhuru wako wa kutembea na unajitafutia mkate wa kila siku lakini chama chako kilisema tuwekwe ndani mpk wakatoka Bungeni , mwenyekiti wenu anahutubia nyumbani kwake peke yake lakini kavaa groves utadhani Michael Jackson. Leo hii mnasimama majukwaani na kutukana matusi (Kwa maana hamna sera yeyote ya kuwambia watanzania )je tungewekwa ndani leo mngesimama jukwaaa gani wkt tupo ndani??
Punguza uongo na uzushi
 
Wamkopeka ,

..kuongeza kwenye maswali yako.

..Walitunga na kupitisha sheria za madini zinazotunyonya ni wana-CCM.

..Waliosaini mikataba mibovu ya kisaliti ni watendaji wa CCM.

..Watanzania waliotumikia ktk nafasi za juu ktk makampuni ya madini baadhi yao ni viongozi na wagombea wa CCM.

..Dr.Kalemani aliwahi kuajiriwa na moja ya makampuni ya madini.

..Deo Mwanyika, mgombea wa CCM Njombe, alikuwa CEO wa Accacia hapa Tanzania, VP wa Africa wa Barrick.
Umenena vyema, ni CCM na sio Magufuli, Na kama umeona hatua alizochukua Magufuli baada tu ya kuingia madarakani utakubali kuwa kuna CCM na wanaCCM. Baba ukiwa mwizi ni rahisi sana watoto kuiba pia na hutakuwa na nguvu ya kuwakemea. Sasa Tundu issu angekoma na CCM akaachana na Magufuli, najua hawezi kumuacha magufuli na kudeal na CCM kwani anajua watanzania tumeona CCM ya MAGU haipo sawa na zilizopita.
 
We ndio mjinga, sasa mamlaka zikiua na kutesa wakosoaji ziachwe tu, kwasababu Snowden anaishi uamishoni?!

Mbona ulimsahau Nelson Mandela kwenye idadi za wakosoaji wako?!
Snowden kuishi uhamishoni imesaidia nini kuzuia kufuatiliwa kwa mawasiliano ya watu? Ametengwa na familia anaishi kwa hofu bila uhuru maana anajua mda wowote CIA wanamfuta kama kashogi. Sijasoma History lakini najua Nelson Mandela hakuwa mkosoaji bali alikuwa mtumwa ndio maana akafungwa jela kibabe. Tafakari ujinga wako kabla hujautangaza usije ukasema Nyerere alikuwa anakosoa utawala wa Mwingereza.
 
Mandela alikuwa mpigania haki kama Lissu, hakuwa mtumwa.

Hahaha mimi nikiwa mjinga wewe akili utazitoa wapi?! Mimi babu yako nilimtongoza bibi yako tukamzaa baba yako, nikachepuka upande wa pili nikamzaa mama yako, kama una vijiakili hata kidogo jua umerithi toka kwangu.
 
Kwa ujumla Lisu hajawahi kuwa na wala sitarajii kama atakuja kuwa kibaraka wa mtu yeyote.

Tundu Lisu, kwa asili yake ni mkweli katika nafsi yake. Tundu Lisu ni mtimwa na kibaraka wa ukweli.

Uzalendo wa Tundu Lisu siyo wa kuhojiwa wala kutiliwa mashaka.

Wanaosema Tundu Lisu ni kibaraka au ndio wale waliotaka kumwua au wale vibaraka wa waliotaka kumwua Tindu Lisu kitokana na kuwa mkweli na mtii wa nafsi yake, nafsi ambayo daima humtaka aseme ukweli na siyo hizi siasa za hadaa za CCM na viongpzi wake.

Maombi yangu daima, "Mungu qetu muweza wa yote, wewe huoanga kila jambo kwa wakati na kwa makusudi yako. Umeruhusu uovu wa watawala utamalaki dhidi ya watu wako, hata watu wako wakaishi kama mateka. Lakini kwa wakati sahihi utawafurumsha watawala waovu, wanafiki, wauaji, watekaji, wateseji na watawalao kwa hila na uwongo. Sasa tunakuomba usimike utawala wako, utawala utakaowaongoza watu kwa haki, utawala utakaowaletea watu wako umoja, utawala utakaoondoa uonevu, utawala utakaoondoa dhuluma, upendeleo na ubaguzi.

Daima Mungu wetu ukamlinde mtumishi wako Lisu ambaye umemjalia kinywa cha ukweli, moyo wa ujasiri, na akili yenye tafakuri. Tunakuomba wale wenye dhamira mbaya dhidi yake ukawaadhibu kwa mapigo ya kusimuliwa vizazi vingi vijavyo. Tumeuona mkono wako wenye nguvu ulivyowatenda kwa wal waliotaka kumwua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee labda unamzungumzia Lissu wa enzi ya Dr Slaa huyu Lissu wa sasa mzee wa Miga ni tofauti sana na Lissu wa Slaa leo ukizungumzia mzalendo wa Nchii hii kati ya Lissu na JPM hata mtoto mdogo anajua nani ni mzalendo mzalendo si maneno ni pamoja na vitendo leo Mwenye nyumba wako aje kutembea na mkeo na kuchukua chakula cha watoto wako ukaogopa kusema kisa utapewa notice huyo ndo Lissu aliyesema tutapelekwa mahakamani kwa kuwakataza wazungu wasiibe na kuchukua madini yetu but JPM alisimama kidete na kutetea hakujali kama kuna Drone zinaweza kutumwa au kupelekwa mahakamani leo hii tuna kampuni ya Twiga

Leo unafurahia Uhuru wako wa kutembea na unajitafutia mkate wa kila siku lakini chama chako kilisema tuwekwe ndani mpk wakatoka Bungeni , mwenyekiti wenu anahutubia nyumbani kwake peke yake lakini kavaa groves utadhani Michael Jackson. Leo hii mnasimama majukwaani na kutukana matusi (Kwa maana hamna sera yeyote ya kuwambia watanzania )je tungewekwa ndani leo mngesimama jukwaaa gani wkt tupo ndani??
Tukumbushane wabunge waliokufa kwa hili janga .... naona umesahau mkuu
 
Tangu hoja za kumuita Lisu Mr Robert nilikuwa naona hazina mashiko hata kidogo walopokaji ukiwauliza ubeberu wa lisuu uko wap hawana majibu wanaishia kutukana tuu
 
Back
Top Bottom