Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Ku change hela kwa mkononi huko risky wabongo hawafai,wachache sana waaminifu
Ila kwenye hotel hapo ya Silverstone kna mbongo mmja huwa anabadili hela na yuko smart sana

Ova

Waliobaki wote wahuni, nilizoeana na jamaa anaitwa paulo, siku nimetoka zangu Angola, nimechoka nikaenda kulala lodge nikaona ngoja nimpigie paulo aje nichukue pesa kidogo shilingi, haaa dola 250 kapotea nayo hadi leo sijawahi kumuona nikajiuliza huyu dogo kapotea na hizi pesa kidogo atafanyia nini? Wakati tip tu nilikua naweza kumpa hata jiwe na nusu nikaona bwege kumbe alikua ananilia timing, nikahamishia mambo yangu yote kwa yule mpemba sijui msomali alikua na burea pale opposite na taqwa, nikazoea nikitaka kusafiri pana chimbo kariakoo nilikua nafuata, kuanzia dola hadi rand naruka nikiwa kamili kabisa, lakini kuchenji kama umeshindwa bora uende benki kuliko kwa wale mawinga washapotea na mitaji ya watu, sehemu ambayo kwenye chenji mawinga sio wababaishaji ni Rwanda lakini upande wetu pale rusumo ni weziwezi hatari, Uaminifu utaukuta asilimia kubwa kwa mkinga kwa bongo lakini jamii nyingine ni tia maji tia maji hakuna unafuu
 
Kwa wapambanaji kuna somo limeibuka kwenye thread hii la uaminifu, niwasihi kwenye biashara na kokote unakopambana uaminifu iwe nguzo yako kubwa kuna siku itakulipa ukiacha amani ambayo utaweza kwenda popote bila kujiuliza maswali, kudhulumu cha mtu mara nyingi itakurudia tu, ni vizuri kupambana kwa bidii sana lakini ujanja ujanja hautakiwi kwani kupotea kwenye ramani ni dakika chache sana.
 
Jamani jamani Wazambia wanao chenchi Hela boda ya Tunduma ni wapigaji Balaa usiyakanyage Mimi ni msafiri wa kila siku msijifariji Wapigaji wapo watu wanaibiwa kila siku mabegi na mizigo yao pale stend ya Lusaka inter city endeleen kujifariji tu
 
Ushamba mzigo kufika hapo Nakonde (border town) unaona umeyapatia!
Binadamu tunatofautiana, wewe kwako unaweza ona kufika nakonde sio kitu ila kuna sisi tunaona ni mafanikio maana hatujawahi fika na yeye kwake ni kitu kikubwa sana, nisamehe lakini umekaa na akili za kimasikini masikini sana mkuu
 
Uaminifu ni changamoto tena kuanzia juu, angalia report za CAG inasikitisha sana yaani watu wanawaza upigaji na huku street raia wanawaza kutapeli na kupiga tuu hakuna EMPATHY.
 
Huijui vizuri Zambia wewe kule uhalifu ni sawa na South Africa
 
Uaminifu ni changamoto tena kuanzia juu, angalia report za CAG inasikitisha sana yaani watu wanawaza upigaji na huku street raia wanawaza kutapeli na kupiga tuu hakuna EMPATHY.
Nchi yote hii kiongozi ambae hakupiga au asie na Mali hata 1 ya kisingiziwa Ni Nyerere tu, wengine wote waliofuata wali-set precedence ya upigaji nasi tunaifuata kiroho Safi.
 
Nadhani hata Uganda wizi wa kijinga hamna, askari wametapakaa sehem nyingi, kuna kijana alijaribu kuiba side mirror ya gari, alitandikwa shaba hapo hapo... Mwizi ni kutandikwa shaba tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…