Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Huijui vizuri Zambia wewe kule uhalifu ni sawa na South Africa
Umetumia kigezo gani mkuu hadi kuifananisha Zambia na Kaburu? Mimi naishi Kaburu zaidi ya miaka 17 sasa, lkn pia Zambia naifahamu maana nimekuwa nikipita pale mara kwa mara na biashar zangu kuja bongo, tena sometimes nakaa hata wiki 2 au 3 pale Zambia, so kwahiyo najua ninachokiandika.
 
Binadamu tunatofautiana, wewe kwako unaweza ona kufika nakonde sio kitu ila kuna sisi tunaona ni mafanikio maana hatujawahi fika na yeye kwake ni kitu kikubwa sana, nisamehe lakini umekaa na akili za kimasikini masikini sana mkuu
Mkuu asante sana kwa kumpa makavu live. Huyu jamaa anaonekana amekata tamaa ya maisha, ndo maana kwake yeye kila mtu ni adui. I mean tayar ameshachoka akili na mwili.
 
Jamani jamani Wazambia wanao chenchi Hela boda ya Tunduma ni wapigaji Balaa usiyakanyage Mimi ni msafiri wa kila siku msijifariji Wapigaji wapo watu wanaibiwa kila siku mabegi na mizigo yao pale stend ya Lusaka inter city endeleen kujifariji tu
Mkuu, Tunduma kuna mchanganyiko wa wazambia na wabongo. Kwahiyo unaweza kupigwa na mbongo afu ukaambiwa kuwa jamaa aliekupiga ni mzambia ili usipate nguvu ya kumfatilia umkamate. Kumbuka sheria za kimataifa zinamkataza askari wetu kuvuka boda kwenda kumkamata mtu upande wa pili, so ili kukuvunja nguvu ww ni lazima ionekane kuwa umetapeliwa na mzambia ili usiwe na nguvu ya kumfatilia tapeli wako ili akamatwe. Kuhusu watu kuibiwa mabegi pale lusaka, sina uhakika nalo maana mwenyew nimeshawahi kulala pale zaidi ya mara 1 na mizigo ya maana ila sijawahi ibiwa chochote. Sana sana kuna wale wazee wa manispaa ambao hupita usiku kuwalipisha watu wote wanaolala pale stand ya mabasi.
 
Pale pale kaunda terminal but Bei za vyumba ni ghali ....Kuna vyumba kwacha 200000 hadi 300000 ambazo ni TSH 40 to 50 thousand, na hapo ni chumba kibaya sana....bongo chumba 30000 elfu unapagawa
Chumba cha kulala wageni kwacha 200000? You can't be serious mkuu. Unajua kw 200000 ni usd ngapi au shingapi ya Tz?
 
Habari zenu wana JF wenzangu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Katika zunguka zunguka yangu yote katika nchi mbali mbali nikianza na nyumbani Tanzania, kwa kweli sijawahi kuona nchi yenye amani na usalama wa hali ya juu kama Zambia.

Kwa wale wenzangu waliowahi kuikanyaga nchi hii bila shaka wataleta ushuhuda wa hiki ninachoongea. Zambia ndio nchi ambayo unaweza kununua kitu njiani huku basi linakwenda, cha ajabu kama ulitangulia kumpa muuzaji hela kubwa, basi muuzaj atalikimbilia hilo basi hadi ahakikishe amekurudishia chenji yako, kitu ambacho kwa nchi nyingi including Tanzania hakipo. Yani ukinunua kitu ukatangulia kutoa hela na basi likaanza kwenda, basi uhesabu ushapigwa, maana muuzaji hatokupa chenji yako, badala yake atakimbia zake akijua hauna uwezo wa kutoka ndani ya basi linalotembea ili umkimbize yeye.

Hiyo tisa, kumi ni pale unapofika Lusaka katika ile stand yao kuu inayoitwa Kaunda bus terminal. Aisee pale utakuta wale jamaa wanaochenji hela wakiwa na maburungutu ya dola za mia mia, hamsini hamsini nk wameziweka mezani kwa ajili ya kuwachenjia wasafiri mbali mbali wanaoshukia pale kutoka nchi mbali mbali. Lile soko liko wazi masaa 24, na hakuna anaeingia kuwasumbua au kuwaibia wale wanao anika madola yao hadharani kwa ajili ya chenji. Kwa Tanzania ukiwa na sh laki 1 ukienda kariakoo kununua kitu, basi muda wa kulipa inabidi usogee kona kidogo ndo uchomoe hela, tena kimagutu magutu unaangalia huku na kule ili usije fatwa na vibaka. Kwa Zambia hiyo haipo.

Kuna siku nilishuka pale na mzigo wa maana, kwa vile nina mjomba wangu anaishi pale ikabidi na mimi nichukue hata wiki moja ili niuze mzigo wangu mdogo mdogo. Aisee nilishangaa kuona jamaa amekuja na zaidi ya dola 2500 tena kaziweka mfukoni tu, hana wasi wasi wowote mpaka pale town lilipo duka la mjomba wangu, akanipa changu na mimi nikamkabidhi mizigo yake akaita gari akapakia akaondoka.

Mimi mcheche ukanishika nikifikiri labda kuna watu wametuona kwahiyo wanaweza kuja kutupora yale madola aliyoniachia jamaa, mjomba wangu akacheka na kuniambia kuwa hapa watu huwa wanatembea mpaka na dola elf 7 town, itakuwa mimi wa dola elf 2 bwana.

Ki ukweli style ya maisha ya pale niliipenda sana haswa kwa upande wa usalama, sema ndo hivyo sehemu ambayo haukuanzia maisha ukisema uende kuanza tena itachukua muda kutoka.

Hizi nchi zetu zingine usalama ni zero, mpaka inafika kipindi wengi wetu tunakuwa tunatembea na kadi za bank tu mifukoni, ili kuepusha wizi wa fedha unaoweza kutokea wakati wowote. Mpaka sasa sijajua ni mbinu gani wanayotumia hawa jamaa kudhibiti wizi na ujambazi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Lusaka na Zambia yote kwa ujumla.
Hata Malawi napo si haba.
 
Unafikiri bongo shaba zingekuwepo hadharani ustaarabu usingekuwepo? Huu upuuzi si sababu mtu anajua anaweza akafanya uhalifu na akatoka salama kwa hongo mahakamani tu.
Labda kwa sababu wale wazee wa zamani waliokuwa wanatumiwa kuwatoa wezi vibusha wameshakufa.
 
Uaminifu ni changamoto tena kuanzia juu, angalia report za CAG inasikitisha sana yaani watu wanawaza upigaji na huku street raia wanawaza kutapeli na kupiga tuu hakuna EMPATHY.
Yani ni majanga kuanzia serikalini hadi mtaani.
 
Nadhani hata Uganda wizi wa kijinga hamna, askari wametapakaa sehem nyingi, kuna kijana alijaribu kuiba side mirror ya gari, alitandikwa shaba hapo hapo... Mwizi ni kutandikwa shaba tu
😀😀😀 huku polisi wetu akimtandika shaba mwizi wa set mirror, lazima wanasiasa wetu waanze kumlaumu polisi kwa mauaji hayo, na akikaa vibaya anaweza akashtakiwa na kufungwa kwa kesi ya mauaji.
 
😀😀😀 huku polisi wetu akimtandika shaba mwizi wa set mirror, lazima wanasiasa wetu waanze kumlaumu polisi kwa mauaji hayo, na akikaa vibaya anaweza akashtakiwa na kufungwa kwa kesi ya mauaji.
Huku utaskia mambo ya haki za binadamu ila kimsingi mwizi ni mshenzi sio binadamu maana angekuwa na ubinadamu asingeiba.
 
Huku utaskia mambo ya haki za binadamu ila kimsingi mwizi ni mshenzi sio binadamu maana angekuwa na ubinadamu asingeiba.
Kweli kabisa, mwizi ni mshenzi sana. Hatakiwi kulindwa na hizi sheria uchwara za haki za binadamu, maana hata yeye wakati wa kufanya wizi wake tayari anakuwa ashavunja sheria zenyew za haki za binadam.
 
Ustaarabu na uaminifu ktk biashara au kitu chochote kinachohusiana na majority ni nature ya mtu/watu haihusiani na hizo dini zenu,wapo wasioamini dini waaminifu wapo wanaoamini dini bila kujali dini gani waaminifu au siyo waaminifu.

Mimi ni mfanyabiashara kuna siku nilijichanganya kwa Mchina nikamzidishia 500,000/= cash Tsh nimekaa sina habari siku nikaagiza mzigo mwengine kunitumia bill yangu naona haiko sawa malipo yanaonyesha madogo nikamuelewesha thamani ya mzigo niliochukua akanitumia screenshot kuonyesha malipo niliyofanya mara ya mwisho nilimzidishia hela but wapo watu wa hizi dini nawakopesha sana vitu hata havizidi 120K Ila wanakimbia maisha siwaoni nikiwaona maneno meengi.
Kweli mi kuna jamaa anajifanya swala tano alinitapeli 80000
 
Kitu cha kwanza ninacho wasifu Wazambia ni binadamu wanaojaliana sana na kuheshimiana uwezi kukuta Mzambia anatukanana ovyo na mwenzie adharani, binafsi nafikiri na malezi yanachangia sana katika hili.
Si unaona chama na bwalya walivyo na heshima huwezi kuta ata mtu wa yanga anawasema vibaya kwa sababu wanajiheshimu na nidhamu
 
Uko sahihi Somalia ndio kiboko

Mtu anaenda msikitini kaacha maburungutu ya hela wazi njiani anapobadilishia na haibi mtu

Nchi Haina amani vurugu tupu lakini uaminifu wa pesa uko juu mno kuliko Sisi watanzania tuliojaa amani
Wasomali wanaiogopa sana dhambi ya dhuruma wao bora waue kuliko dhuruma yupo msomali mmoja Namanga akizidishiwa pesa atamtafuta mpaka mwenyewe ampate hata avuke awe Nairobi ukirudi utakutana na hela yako na hata ajali iwe kiasi chochote..
 
Back
Top Bottom