Mkuu, Tunduma kuna mchanganyiko wa wazambia na wabongo. Kwahiyo unaweza kupigwa na mbongo afu ukaambiwa kuwa jamaa aliekupiga ni mzambia ili usipate nguvu ya kumfatilia umkamate. Kumbuka sheria za kimataifa zinamkataza askari wetu kuvuka boda kwenda kumkamata mtu upande wa pili, so ili kukuvunja nguvu ww ni lazima ionekane kuwa umetapeliwa na mzambia ili usiwe na nguvu ya kumfatilia tapeli wako ili akamatwe. Kuhusu watu kuibiwa mabegi pale lusaka, sina uhakika nalo maana mwenyew nimeshawahi kulala pale zaidi ya mara 1 na mizigo ya maana ila sijawahi ibiwa chochote. Sana sana kuna wale wazee wa manispaa ambao hupita usiku kuwalipisha watu wote wanaolala pale stand ya mabasi.