Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Huijui vizuri Zambia wewe kule uhalifu ni sawa na South Africa
Umetumia kigezo gani mkuu hadi kuifananisha Zambia na Kaburu? Mimi naishi Kaburu zaidi ya miaka 17 sasa, lkn pia Zambia naifahamu maana nimekuwa nikipita pale mara kwa mara na biashar zangu kuja bongo, tena sometimes nakaa hata wiki 2 au 3 pale Zambia, so kwahiyo najua ninachokiandika.
 
Binadamu tunatofautiana, wewe kwako unaweza ona kufika nakonde sio kitu ila kuna sisi tunaona ni mafanikio maana hatujawahi fika na yeye kwake ni kitu kikubwa sana, nisamehe lakini umekaa na akili za kimasikini masikini sana mkuu
Mkuu asante sana kwa kumpa makavu live. Huyu jamaa anaonekana amekata tamaa ya maisha, ndo maana kwake yeye kila mtu ni adui. I mean tayar ameshachoka akili na mwili.
 
Jamani jamani Wazambia wanao chenchi Hela boda ya Tunduma ni wapigaji Balaa usiyakanyage Mimi ni msafiri wa kila siku msijifariji Wapigaji wapo watu wanaibiwa kila siku mabegi na mizigo yao pale stend ya Lusaka inter city endeleen kujifariji tu
Mkuu, Tunduma kuna mchanganyiko wa wazambia na wabongo. Kwahiyo unaweza kupigwa na mbongo afu ukaambiwa kuwa jamaa aliekupiga ni mzambia ili usipate nguvu ya kumfatilia umkamate. Kumbuka sheria za kimataifa zinamkataza askari wetu kuvuka boda kwenda kumkamata mtu upande wa pili, so ili kukuvunja nguvu ww ni lazima ionekane kuwa umetapeliwa na mzambia ili usiwe na nguvu ya kumfatilia tapeli wako ili akamatwe. Kuhusu watu kuibiwa mabegi pale lusaka, sina uhakika nalo maana mwenyew nimeshawahi kulala pale zaidi ya mara 1 na mizigo ya maana ila sijawahi ibiwa chochote. Sana sana kuna wale wazee wa manispaa ambao hupita usiku kuwalipisha watu wote wanaolala pale stand ya mabasi.
 
Pale pale kaunda terminal but Bei za vyumba ni ghali ....Kuna vyumba kwacha 200000 hadi 300000 ambazo ni TSH 40 to 50 thousand, na hapo ni chumba kibaya sana....bongo chumba 30000 elfu unapagawa
Chumba cha kulala wageni kwacha 200000? You can't be serious mkuu. Unajua kw 200000 ni usd ngapi au shingapi ya Tz?
 
Hata Malawi napo si haba.
 
Unafikiri bongo shaba zingekuwepo hadharani ustaarabu usingekuwepo? Huu upuuzi si sababu mtu anajua anaweza akafanya uhalifu na akatoka salama kwa hongo mahakamani tu.
Labda kwa sababu wale wazee wa zamani waliokuwa wanatumiwa kuwatoa wezi vibusha wameshakufa.
 
Uaminifu ni changamoto tena kuanzia juu, angalia report za CAG inasikitisha sana yaani watu wanawaza upigaji na huku street raia wanawaza kutapeli na kupiga tuu hakuna EMPATHY.
Yani ni majanga kuanzia serikalini hadi mtaani.
 
Nadhani hata Uganda wizi wa kijinga hamna, askari wametapakaa sehem nyingi, kuna kijana alijaribu kuiba side mirror ya gari, alitandikwa shaba hapo hapo... Mwizi ni kutandikwa shaba tu
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ huku polisi wetu akimtandika shaba mwizi wa set mirror, lazima wanasiasa wetu waanze kumlaumu polisi kwa mauaji hayo, na akikaa vibaya anaweza akashtakiwa na kufungwa kwa kesi ya mauaji.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ huku polisi wetu akimtandika shaba mwizi wa set mirror, lazima wanasiasa wetu waanze kumlaumu polisi kwa mauaji hayo, na akikaa vibaya anaweza akashtakiwa na kufungwa kwa kesi ya mauaji.
Huku utaskia mambo ya haki za binadamu ila kimsingi mwizi ni mshenzi sio binadamu maana angekuwa na ubinadamu asingeiba.
 
Huku utaskia mambo ya haki za binadamu ila kimsingi mwizi ni mshenzi sio binadamu maana angekuwa na ubinadamu asingeiba.
Kweli kabisa, mwizi ni mshenzi sana. Hatakiwi kulindwa na hizi sheria uchwara za haki za binadamu, maana hata yeye wakati wa kufanya wizi wake tayari anakuwa ashavunja sheria zenyew za haki za binadam.
 
Kweli mi kuna jamaa anajifanya swala tano alinitapeli 80000
 
Kitu cha kwanza ninacho wasifu Wazambia ni binadamu wanaojaliana sana na kuheshimiana uwezi kukuta Mzambia anatukanana ovyo na mwenzie adharani, binafsi nafikiri na malezi yanachangia sana katika hili.
Si unaona chama na bwalya walivyo na heshima huwezi kuta ata mtu wa yanga anawasema vibaya kwa sababu wanajiheshimu na nidhamu
 
Uko sahihi Somalia ndio kiboko

Mtu anaenda msikitini kaacha maburungutu ya hela wazi njiani anapobadilishia na haibi mtu

Nchi Haina amani vurugu tupu lakini uaminifu wa pesa uko juu mno kuliko Sisi watanzania tuliojaa amani
Wasomali wanaiogopa sana dhambi ya dhuruma wao bora waue kuliko dhuruma yupo msomali mmoja Namanga akizidishiwa pesa atamtafuta mpaka mwenyewe ampate hata avuke awe Nairobi ukirudi utakutana na hela yako na hata ajali iwe kiasi chochote..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…