Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Zambia ni sahihi tunatoka na magari SA hakuna uporaji sehemu yeyote ipo miaka ya kati majambazi wakawa wanavamia pale Nkushi walipotea wote wale jamaa kesi ya kuiba kwa kutumia siraha lazima uuawe...wapo vijana kutoka Mbeya waliwahi jaribu kufanya hiyo kazi Lusaka watatu walirudishwa maiti huyo mmoja aliponea kwenye tundu la sindano hakurudi tena Zambia...
 
Duh hiyo kali.
 
Wasomali wanaiogopa sana dhambi ya dhuruma wao bora waue kuliko dhuruma yupo msomali mmoja Namanga akizidishiwa pesa atamtafuta mpaka mwenyewe ampate hata avuke awe Nairobi ukirudi utakutana na hela yako na hata ajali iwe kiasi chochote..
Duh huyo kweli ana hofu ya Mungu
 
Japo mi mkristo ila unachosema nu kweli

Jamii za kiislamu zina ustaarabu sana kwenye biashara na mambo ya wizi wizi sio mkubwa kuliko jamii za kikristo.

Huo ni ukweli kabisa
Sio kwel unajua nn sabab ya Somalia , Iraq , Syria , Nigeria , Libyia , Msumbiji nk hazijatulia mpk leo ? mali wanazoiba kwa wananch ndo zinawapa uhai kuendeleza harakat zao
 
Usijidanganye eti askari washindwe kuvuka boda upande wa pili wapo Majambazi kipindi cha miaka ya nyuma walikua wanaishi upande wa Zambia wanakuja Tunduma kufanya matukio kwa ushirikiano na polisi wa Zambia wale wahuni walikamatwa watu wakaambiwa wakatambue ndugu zao hapo Hospital ya Rufaa Mbeya.
 
Kwa kaburu matukio yake wengi wanayasikia kwenye Radio mbao ndio maana wanaweza kufananisha na Nchi yeyote...Dunian SA inakimbizana na Mexico au USA pana matukio ya hatari na ajabu kuwahi kutokea popote pale...
 
Sio kwel unajua nn sabab ya Somalia , Iraq , Syria , Nigeria , Libyia , Msumbiji nk hazijatulia mpk leo ? mali wanazoiba kwa wananch ndo zinawapa uhai kuendeleza harakat zao
Libya waliibiwa nini? Wao walichotaka ni kumtoa Col. Gaddafi madarakani na pumzi ya moto wanaiona. Hili jambo la uadilifu haliendani na dini bali mila na desturi ya taifa fulani na hali ya kiuchumi kama watu wanapata kazi na pesa automatically hata criminal activities zinapungua pia.
 
Hajui value ya Kwacha huyu, kwasasa wanasema Zambian Kwacha inafanya vizuri kuliko Rand ya South Africa
Sio kwa sasa mkuu, toka 2014 mi napita Zambia kutokea South Africa nimekuta kwach ipo juu ya rand ya South Africa. So nahisi ndugu yetu ana bahatisha tu hajui thaman ya hii hela. Nahisi anazungumzia Malawian kwacha huyu.
 
Wale walifuta 000 zile ile hela haina thamani hata kuizidi Tsh ila kuelewa hapo kwa watu wengine mtakesha...
Mkuu hii hoja yako imekaa kijiweni jiweni haina fact yoyote. Hivi inawezekana vp uamke tu asubuhi utoe hizo sifuri afu hapo hapo hela yako iwe juu ya hela ambazo zilikuwa na nguvu hapa afrika kama rand nk, vyakula viwe bei ile ile inayofanana na thaman ya hela, na dola ishuke dhidi ya kwacha? Kama ingekuwa ni rahisi hivyo basi wangeanza Zimbabwe, Congo, Uganda na nchi nyingine kufanya hivyo. Leo hii Kw 30 ya Zambia unakula msosi hadi unaacha mezani, afu uje na majibu mepesi hivo!
 
Mkuu hivi unaelewa kweli unachoandika. Wewe ushasema majambazi wa upande wa Zambia walikuwa wanavuka boda kuja kufanya ujambazi upande wa Tanzania. Sasa kama jambazi ashavuka boda kuja upande wa Tanzania kufanya uhalifu unategemea sheria za Tanzania zingemkataza askari wa Tanzania kuchukua hatua waliyochukua dhidi ya majambazi hao. Mi nilifikiri unataka kusema kwamba maaskari wa Tanzania walivuka boda kwenda kuwapiga risasi hao majambazi kule Zambia, kumbe unasema waliwapigia Tanzania baada ya majambazi hao kuingia katika ardhi ya Tanzania. Hapo hamna kosa kijana. Kwa sabab wamekuja kufanya uhalifu katika ardhi yetu. Je ulisikia juzi kati kuna askar wa Tanzania walifukuzwa kazi baada ya kuvuka boda kuwafuata wahalifu nchini Malawi? Unajua sabab iliyotolewa kwa wale askari kusimamishwa na kufukuzwa kazi kwa sabab ya kuingia Malawi? Mimi nasema hivi kwa sababu najua sheria za kimataifa mkuu.
 
Kwa kaburu matukio yake wengi wanayasikia kwenye Radio mbao ndio maana wanaweza kufananisha na Nchi yeyote...Dunian SA inakimbizana na Mexico au USA pana matukio ya hatari na ajabu kuwahi kutokea popote pale...
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ya kweli mkuu wengi wanaongea kwa kubahatisha, na wakati sisi tuliopo huku tunaona uhalisia.
 
duu wale jamaa kosa lao kuvuka mpaka au kuna siasa ndani yake???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…