Sikio la Kufa halisikii dawa - Wakataa ndoa wote

Usitumie nguvu kwa watoto wa afumbili wanaishi kwa double chance
Ni kweli. lakini ukweli waambiwe. Wapo wanaojielewa na wanamaendeleo mazuri sana! wale wanaojifanya bangi ndio hao hasara tupu
 
Kwenye equation ya ndoa za zamani variable muhimu iliyokiwa ikiishikilia ndoa ni UPENDO,kwani upendo huvumilia,upendo ndani yake unahuruma,unamatumaini nk.Siku hizi hamna mabinti wenye sifa kama wanawake wa zamani unawatafuta kwa tochi.

Siku hizi ndoa nyingi zimeshikiliwa na fedha,uchumi ukiteteleka ndoa hamna. Hiyo haitoshi hata wanawake tunao waoa hawana usichana wao wamefungamana na roho nyingi, ndio maana anapokutana na magumu yoyote anaaza kuwakumbuka Maex wake na ndio maana Ulaya ndoa nyingi kwa asilimia zaidi ya sabini huvunjwa na wanawake. Juzi mwananchi wameripoti kwa hata hapa TZ ndoa nyingi huvunjwa na wanawake.

Ndio maana siku hizi hata wanaume wameanza kuwa na vitega uchumi vya vya siri, ujue zamani wazee walikuwa wanawaficha watoto wa nje,ila mali zake mke na watoto watazijua.Ila siku hizi wanaume wanaficha vitega uchumi vyao,sababu wanaamini hela ndio itakayo Walea baadae na si wanawake au watoto. Hii yote imesababishwa na ubinafsi wa wanawake chao chao cha mmewe chake.

Yaani siku hizi kupata mke mwaminifu, atakaye kuheshimu katika vipindi vyote vya hali yako ya kiuchumi, atakaye kuonesha upendo bila kuangalia fedha ulizo nazo bila kusahau hofu ya Mungu ndani yao ni ngumu kumpata na tena siku hizi hamna watu wanaongoza kuvunja ndoa kama Maex,ndio maana hata Mungu alituambia tusijuane kabla ya ndoa aliyajua hayn.Ndio maana siku hizi utasikia anabwawa,kibamia,kimoja chali,hana pumzi,K imekaa kama utumbo wa ng'ombe nk vurugu tupu,ila kama msingejuana huko msingefika. Ukija tena usawa wa kijinsia na 50/50 ambao unawapa viburi wanawake ,heshima hawana watu siku hizi wanaamua kupiga na kusepa.

Haafu kingine dada zangu mnaamini sana kwenye fedha,ila hamna kitu kilicho rahisisha upatikanaji wa ngono kama fedha,inafikia kipindi mpaka inawazalilisha,fedha imewaweka kwenye grade,hata yule anayejishaua kwamba yy anahongwa laki kesho nae atahongwa Msimbazi,siku hizi ngono inapatikana hata kwa buku,buku tano au kumi unapata binti ana kila kitu na tamaa yenu ya fedha imesababisha ndoa kuonekana haina maana. Halafu siku hizi wengi wa mabinti mnakuja kukumbuka ndoa wakati umri ushawatupa,mshatumika sana na wengine mpaka kuzalishwa wakati mda huo soko mnakuwa hamna.

Mimi siku hizi si mlaumu mtu kutokuoa au kuchelewa kuoa. Ila hamna kitu kinauma kama kuona ndoa imevunjika hasa ile iliyo barikiwa kupata watoto, halafu ukija kusikia sababu utagundua ndoa ilikuwa haina upendo ndani yake na ndio maana wameshindwa kuvumiliana.
 
Kwa nini unaingilia uhuru wa watu kuamua kuwa single?

Kwani kuna aliyeingilia uhuru wako wa kuingia ndoani?
 
S
Ijasoma yote nimeishia kwenye " kwanini uishi peke ysko" kwani kukataa ndoa kuna uhusiano gani na kuishi peke yako kwani nikiishi na watoto wangu na ndugu zangu na wafanyakazi wangu kuna shida ni wangapi wana wake na wana waume mmoja kafariki amebaki mjane au mgane je kuwa mjane au mgane ni kuishi peke yako
 
Ngoja akanyee debe
 
hao ndugu zako wao hawaoi wala kuolewa? na wanao je? hujui kuna siku watoto wote wataenda anza maisha yao? au ndo itabidi uwang'ang'anie wabaki hapo home? Isuue ya ugane na ujane haiingi kwenye kataa ndoa.
 
Ni kweli kabisa
 
Kwa hiyo walioko kwenye ndoa huwa wanakufa vizuri sio?!
 
Unazungumzia wanawake wapi wewe? Tena hawa wa sasa atabaki na wewe ukifilisika wakati wengi wenu mnafuata hela? Hata hawa wanawake walio kwenye ndoa wakiwa na kipato wengi wanafanya mambo yao kwa siri. Kwa hiyo kuoa sio guarantee ya hayo uliyosema
 
Kuzaa kupo kuishi nao kupo tunachokataa ni ule mkataba wa kitapeli



KATAA NDOA
NDOA NI UTAPELI
NDO NI MKATABA WA MATESO
 
Kataa ndoa haina mahusiano na kuzaa.

Adam na Eva walituzaa nje ya Ndoa, hawakutaka Stress..

Ronaldo CR7 Ana Familia ila hana ndoa.

Ogopa sana mkataba wa kutenganishwa na KIFO...
Sasa CR 7 hata akiachana na huyo alienae leo wale wanae unadhani watahangaika??

Kataa ndoa ni ubinafsi wa wanaume walio wengi, yaani unataka uchovye kutimiza haja zako, mtoto akizaliwa alelewe na mama bila uwepo wako kabisa.
 
hao ndugu zako wao hawaoi wala kuolewa? na wanao je? hujui kuna siku watoto wote wataenda anza maisha yao? au ndo itabidi uwang'ang'anie wabaki hapo home? Isuue ya ugane na ujane haiingi kwenye kataa ndoa.
Ukiwa mwema uwezi kukosa wa kukaa nao hata wajukuu...mwisho wa siku hata mwenye mke ufiwa mna mkewe pia na kubaki kama kataa ndoa
 
Hauwezi kumshawishi mwanaume yeyote asietaka ndoa atake ndoa. Tunao wajomba wengi wana miaka 50 wanaranda randa bar hawana ndoa masenior bachelor, wengi wanaishia kufa kwajili ya matumizi mabovu ya pombe (figo) au magonjwa ya zinaa. Wakataa ndoa mwisho wao wote ni mmoja, wakiumwa wakiishiwa hamna familia kuwajali. Waache ndio maisha waliochagua, bado sijaona mwanaume aliefanikiwa kimaisha na yupo mwenyewe. Ukweli ni kwamba hamna jamii inaamini mwanaume asie na majukumu ya kifamilia kama ni cheo hutapata wala
Heshima eneo lolote. Utabali hivo hivo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…