Hamisi ananyongwa kisa ni NDOA.
""Nilikutana na wewe mke wangu ukiwa ni mwanachuo katika chuo cha Mwalimu Nyerere kigamboni.
Tukaanzisha mahusiano ya kimapenzi.
Mimi ni muislamu
Lakini mwaka 2008 nikaamua kukuoa kwa ndoa ya kikistru kanisa la Assemblies of God Upanga
Bila ya shaka nimefanya hivi kwa kuwa nakupenda sana mke wangu.
Tunaishi maisha mazuri, tunafanikiwa kumiliki nyumba kadhaa na magari manne.
Ninakufungulia biashara ya duka la kuuza madawa huku mimi nikiendelea na biashara yangu ya kununua na kuuza viwanja.
Tunapata mtoto mmoja aitwaye Gracious
Mke wangu unabadilika.
Unaanza kuninyima haki yangu ya ndoa bila sababu za msingi.
Hali inaendelea hadi inafikia hatua tunalala vyumba tofauti katika nyumba yetu ya ghorofa mimi chumba cha juu wewe cha chini.
Inafikia hatua mimi naanzisha mahusiano nje na wewe unaanzisha ya kwako.
Unaweza kulala nje bila taarifa na mimi vivyohivyo.
I and you deny each other conjugal rights (horizontal engagement)
Jambo hili linajulikana kwa wazazi wa pande mbili.
Hata majirani wanajua mambo unayonifanyia kama kunimwagia maji machafu, kunipiga na fagio na hata kunivuta makende yangu mbele ya mama yangu mzazi.
Mke wangu,
Kuna siku ulinichoma na kisu mkononi
Nikaenda Polisi lakini wakanirudisha kuwa tumalizane wenyewe.
Yote nilivumilia.
Kila wakati unani provoke kuwa nikupige nikuue lakini sifanyi hivyo.
Nilishakuomba twende mahakamani tuvunje hii ndoa yetu lakini ukakataa.
Ikafikia hatua sili wala siogi nyumbani kwangu kwani naogopa usije niwekea sumu.
Ndipo kuna siku niliondoka nyumbani bila kurudi kwa muda wa siku tano.""
Story juu, imepatikana kwenye maelezo ya onyo (Cautioned statement) ya Hamisi Saidi Luwongo
Maelezo haya aliyatoa mbele ya mpelelezi kituo cha polisi Temeke
NA HIZI NDIO NDOA ZENU.
View attachment 3251653View attachment 3251654
#YNWA
#YANGA_BINGWA