Sikio la Kufa halisikii dawa - Wakataa ndoa wote

Sikio la Kufa halisikii dawa - Wakataa ndoa wote

Kataa ndoa haina mahusiano na kuzaa.

Adam na Eva walituzaa nje ya Ndoa, hawakutaka Stress..

Ronaldo CR7 Ana Familia ila hana ndoa.

Ogopa sana mkataba wa kutenganishwa na KIFO...
Wewe unaweza jifananisha na Adam au CR7 😃😃
 
Vijana acheni kusikiliza watu wasio na hoja.Hivi kuna KATAA NDOA kasema mtu asichape ukuni???Atuonyeshe wapi kwenye katiba yetu tumekataza watu kuwa na watoto???

Vijana mnaojielewa jipendeni nyie kwanza achaneni na hawa wazee mufilisi wamerogwa na kupigwa malimbwata na wake zao.

Wazee wa namna hii ndo unawakuta wako rafu hawajipendi hawavai wakapendeza siku ya siku wanagongewa wake zao kisa kutokuwa smart au kuwapa wake zao muda,unawakuta segerea au wameji-RIP.
 
Wakati unashawishika na watu waliovuta bangi zao, waliojikatia tamaa ya kuishi, wasiotaka ndoa kwa kuwa wao si wanaume wala si wanawake... hawajielewi, waliotingishika akili baada ya kutendwa kwenye mapenzi; waliolelewa nje ya famili na wakachukia familia; kaa chini utafakari. Hapa si quote mstari wowote wa vitabu vitakatifu, hapa nakupa makali live.

Jaribu kufikiria, ulilelewa na familia na sasa unajitegemea. Kwa nini uishi peke yako? Wakati ukiwa na familia yako ndio waliokuwa wakipa huduma zote ulizohitaji wakati wa furaha na wakati wa magumu sasa iweje leo uwe mwenyewe? Huo ubinafsi wa kuishi peke yako unautoa wapi? kwa nini usioe? kwa nini nawe usisimame kama baba ukiienjoy na mke na watoto wako?

Hivi kesho ukihitaji huduma za kuhospitali nani atakuogesha? nani atakufariji? Najua una ndugu zako, nao watakuwa bize na familia zao; utashirikiana nao katika mambo ya nje na si ya ndani. Hivi usiku unajikumbatia peke yako kama mchawi na hata wachawi wanaoa! Hata kama utanunua wanawake... utachoka... hutapata amani na faraja ambayo ungeipata kwa mke. Kwani nini uishi kiunyongee?

Jaribu kuangalia walioishi peke yao..... hakuna aliyekuwa na furaha ya dhati, waliishia kuwa walevi na wanunua papuchi mwisho walifia ndani na kukutwa wamepasuka. Ndoa ni muhimu kwa binadamu. Changamoto za ndoa zinaweza kuwa solved lakini ukiwa na upweke si vya kukimbilia. Najua kuna wanaojifariji eti nitazalisha huko nje na kuchukuwa watoto wangu.

AMKA jipange kutafuta familia uitunze ikutunze. Hao wanaokudanganya humu hutakuwa nao na utakufa kibudu.

Ndo nshasema.. wakataa ndoa wote hawajielewi... wakajicheki afya ya akili na kama ukitaka kuwaiga usithubutu.

Mapovu ruksa.... ndoa zidumu na zitadumu milele na milele.
Nina ushuhuda na hili teacher mmoja hakuoa alikufa ovyo sana cos hakupata huduma ya karibu walimu wenzake wameenda kupiga gongo mtaani yeye anakabiliana na kutokwa roho wanataarifiwa wanafika mwamba hana dk 20 mbele yaani wanambeba mita 200 tu wanarudi kwamba kashadead
Siutaki ubachela kamwe hata nikiachana na niliyenaye sasa nitatafuta mwingine nioe ili anifariji tu no way out
Unakufa kwa njaa na pesa unayo
 
Ndoa ni kitu chema Kwa mtu mwenye akili timamu
Vyovyote itavokuwa ilaa wataoa sahiz ni mudwao kupiga kelele wengi ni vijanawadogo na hawana ela na hawajui umuhimu wa familia

Kwa kipind kidogo nilichoish bila baba nimeelewa familia ni muhimu sana kusema mtu akisema nitazaa ila sioni nawaonea huruma sana wanae hata wanaotalikiana Mungu awasaidie
Rafiki yangu material yako ni mazuri, tatizo utamuoa nani. Unachoeleza ni inavyotakiwa kuwa, lakini unakutana na hali tofauti kabisa. Bahati mbaya hata mwenye maono kama yako anaweza kushindwa kuyasimamia akawa kituko tu.
 
Sidhani kama watu wote wanazeeka na wenza wao. Na.mara nyingi ulizeeka unahitaji msaada wa ndugu jamaa. Hakuna mtu anaweza kujitunza au kutunzwa na mwenza pekee anapozeeka au kuwa mgonjwa mahtuti.
Leteni hoja zenye mantiki.Yaani unaingia kwenye ndoa kisa ukizeeka upate mtu wa kukuvalisha pampers are you nuts!!!

Hivi unashindwa nini kujitengea hela like a trust fund kiasi kwamba ukizeeka beyond huwezi kujihudumia unawalipa watu tena professionals wakutunze.Manesi kibao huko wanataka hizo kazi za kulea wazee.Nyie mazezeta badilikeni dunia inaenda kasi acheni kulala.
 
Ndoa ni kitu chema Kwa mtu mwenye akili timamu
Vyovyote itavokuwa ilaa wataoa sahiz ni mudwao kupiga kelele wengi ni vijanawadogo na hawana ela na hawajui umuhimu wa familia

Kwa kipind kidogo nilichoish bila baba nimeelewa familia ni muhimu sana kusema mtu akisema nitazaa ila sioni nawaonea huruma sana wanae hata wanaotalikiana Mungu awasaidie
Ndoa ina uhusiano gani na hela, viko direct proportional?...kama ndio hivyo kwanini the wealthiest wako single ?....
 
Nina ushuhuda na hili teacher mmoja hakuoa alikufa ovyo sana cos hakupata huduma ya karibu walimu wenzake wameenda kupiga gongo mtaani yeye anakabiliana na kutokwa roho wanataarifiwa wanafika mwamba hana dk 20 mbele yaani wanambeba mita 200 tu wanarudi kwamba kashadead
Siutaki ubachela kamwe hata nikiachana na niliyenaye sasa nitatafuta mwingine nioe ili anifariji tu no way out
Unakufa kwa njaa na pesa unayo
Kwahiyo hali aliyekuwa nayo unahisi angekuwa na mke angezuia kifo chake.

Hivi huwa mnafikiri na kuwazua kabla hamjacomment.Kwa akili hizi wewe lazima mwanamke akusumbue.Pona pona yako KATAA NDOA!!!!
 
Nina ushuhuda na hili teacher mmoja hakuoa alikufa ovyo sana cos hakupata huduma ya karibu walimu wenzake wameenda kupiga gongo mtaani yeye anakabiliana na kutokwa roho wanataarifiwa wanafika mwamba hana dk 20 mbele yaani wanambeba mita 200 tu wanarudi kwamba kashadead
Siutaki ubachela kamwe hata nikiachana na niliyenaye sasa nitatafuta mwingine nioe ili anifariji tu no way out
Unakufa kwa njaa na pesa unayo

Tena anabahati alikufa akionekana na watu. Wengine hufia ndani na kugundulika baada ya zaidi ya siku tatu! mbaya sana... kisa upweke! Tuoane tu kwa faida yetu wenyewe
 
Back
Top Bottom