Siku Dkt. Bashiru, Prof. Kabudi au Balozi Polepole wakisimama dhidi ya CCM nitaogopa sana lakini Lissu, Lema na Mbowe hawana maajabu

Siku Dkt. Bashiru, Prof. Kabudi au Balozi Polepole wakisimama dhidi ya CCM nitaogopa sana lakini Lissu, Lema na Mbowe hawana maajabu

Hapa nayazungumzia magijwi hodari wa kujenga na kutetea hoja. Ni watu ambao kwa mfanano wamebeba taswira za Baba wa taifa kimaono, Dkt. Magufuli kiutendaji na Dkt. Kikwete kiuzungumzaji. 'Combination' ya watu hao kwa hakika ndio itakayeleta upinzani wa kweli kwa CCM.

Siku ambayo hao watatu wakiungana kuna uwezekana CCM itapata tabu kwa kiasi fulani lakini kama sio hao kizazi hiki hakina mtu nje ya hao wa kuitetemesha CCM.

Sio Lissu, Lema au Mbowe wataweza kuiondoa CCM madarakani wala kizazi kinachotokana na wao.
Wamekusikia ila subiri Mwl wa sheria aje tarehe 25 ndio utaelewa kwa nini tuliiba wimbo wa taifa mahali fulani
 
Alikula matapishi, hadi makamba anasema wazuri hawafi na yeye anakubali na kupiga makofi.?

Hivi Bashiru ana steategies gani? Za kuzuia mikutano na kuzima internet siku ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu, au strategies za kuengua wagombea wa upinzani.

Uchaguzi ungekuwa clean na wakashinda kwa haki hapo ningefikiria kidogo.
Siku zote matokeo ya kushindwa kwenye siasa yanaumiza sana na maumivu yake ni kama yale ya mechi kufungwa inafikia mahali wengine wanashindwa kuyavumilia.

Kituko kinakuja pale wanaposhinda wanasema tume ni huru na wanaposhindwa ndio wanapiga kelele tume sio huru. Hiki wanachofanywa ni kushindwa kuvumilia maumivu ya kushindwa kabisa.
 
Hao pamoja na wengine wengi wanaungana ndani ya chama kuimarisha chama na kujenga serikali yenye nguvu.

Hawawezi fanana na walioamua kuwa wakimbizi na kwenda kuishi ughaibuni huku wakitaka madaraka Tanzania

Chama chetu Cha Mapinduzi chajenga nchi
Ndiyo nchi hii haiendelei, Chama kilichopo madarakani haina uwezo wa kujenga nchi.
 
Hapa nayazungumzia magijwi hodari wa kujenga na kutetea hoja. Ni watu ambao kwa mfanano wamebeba taswira za Baba wa taifa kimaono, Dkt. Magufuli kiutendaji na Dkt. Kikwete kiuzungumzaji. 'Combination' ya watu hao kwa hakika ndio itakayeleta upinzani wa kweli kwa CCM.

Siku ambayo hao watatu wakiungana kuna uwezekana CCM itapata tabu kwa kiasi fulani lakini kama sio hao kizazi hiki hakina mtu nje ya hao wa kuitetemesha CCM.

Sio Lissu, Lema au Mbowe wataweza kuiondoa CCM madarakani wala kizazi kinachotokana na wao.
Mjenga hoja ndiye yule alisema watatumia dola kibaki madarakani? Au mimi pia sijaelewa?
 
Hao pamoja na wengine wengi wanaungana ndani ya chama kuimarisha chama na kujenga serikali yenye nguvu.

Hawawezi fanana na walioamua kuwa wakimbizi na kwenda kuishi ughaibuni huku wakitaka madaraka Tanzania

Chama chetu Cha Mapinduzi chajenga nchi
Unaweza kuta kuna watu au mtu anakuita na wewe mama
 
Upinzani unahitaji watu wenye kariba ya hao niliowataja usonge mbele ,kizazi Cha lema ,lissu na Mbowe kinaurudisha nyuma sana upinzani
Sasa kwanini usiende wew kuwa mpinzani au wewe unawashwa wapi kama wew siyo mpinzani?
 
Hapa nayazungumzia magijwi hodari wa kujenga na kutetea hoja. Ni watu ambao kwa mfanano wamebeba taswira za Baba wa taifa kimaono, Dkt. Magufuli kiutendaji na Dkt. Kikwete kiuzungumzaji. 'Combination' ya watu hao kwa hakika ndio itakayeleta upinzani wa kweli kwa CCM.

Siku ambayo hao watatu wakiungana kuna uwezekana CCM itapata tabu kwa kiasi fulani lakini kama sio hao kizazi hiki hakina mtu nje ya hao wa kuitetemesha CCM.

Sio Lissu, Lema au Mbowe wataweza kuiondoa CCM madarakani wala kizazi kinachotokana na wao.
Yani wakikataa kulea familia zao ndiyo utawaamini.Great Fool Of All Times!
 
Alishindwaga lowasa basi hakuna wakuitetemesha CCM, jamani CCM ni limbuyu likubwa.
 
Sukuma gang hawana nafasi tena nchi tayari imeshapata uhuru kwa mara ya pili tangu 09/12/1961 ikaja kuwa koloni la Chato empire chini ya Jemedari Pombe Magufuri na kufurushwa vibaya 17/03/2021 na COVID 19. Baada ya hapo tukapata Rais mwanamke kiulaini Mheshimiwa Samiah Hassan Suluhu.
Safi sana hii
 
Lini ulimchagua huyo mwanamke?

Pia jua kuwa hakuna kitu inaitwa sgang Nchi hii,

Lipo tabaka la kundi dogo waliojitajirisha isivyo halali wanapambana kuwadidimiza wenye HAKI na kuwabebesha mizigo mizito.

Tuhakikishe Nchi inakuwa moja, tusikubali kugawanywa makundi makundi.

Aamen
Sukuma gang wapo, ni watu kaliba ya Bushiri, Ndungoi, Slow Slow, Kabundi na wengineo. Sukuma gang siyo kabila ni tabia. Kwani Saambaya au Ndungoi ni wasukuma? Lakini ni Sukuma gang members
 
Hao ndio masalia ya Nyerere chamani,

Nyerere hakuanzisha chama Ili viongozi walambe asali wakati wananchi wanaramba shubiri.

Wavamizi ndani ya chama ndo wafurushwe, hivyo sioni sababu ya Polepole na kabudi Kutoka ndani ya CCM!!!
Kabudi yule aliyesema katoka jalalani?
 
Baba wa taifa mwalimu Nyerere alisema upinzani wa kweli wa hii nchi utatoka ndani ya CCM.

Ccm inawatu makini wengitu ambao wakiamua kuwa wazalendo wanaweza kufanya maajabu makubwa ya kimaendeleo katika nchi yetu.

Hawa wapinzani hawana uwezo wakuingoza nchi sababu wenyewe hawajiamini.

Kumbuka uchaguzi mkuu 2015 katika nafasi ya urais ndio utajua wapinzani hawajawa na uwezo wa kuongoza.
So ccm kama ina watu makini ilikuwaje mtu kama Jiwe akapata nafasi ya kuwa Rais wa nchi? Au na yeye ni moja ya watu makini huki kwenu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Usisahau laptop kwa Walimu na 50 ml kwa kila kijiji, mwisho wa siku akaishia kuiba uchaguzi, ila tuseme ukweli hakuna Rais muovu kama Jiwe
 
Kweli chajenga nchi kwa deni kuongezeka mpaka trilioni 92

Wale chadema waliotuambia pesa ya kuendesha nchi wangeenda kuchukua ulaya sasahivi deni lingekua trillion 92×10

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hasan
 
Sukuma gang wapo, ni watu kaliba ya Bushiri, Ndungoi, Slow Slow, Kabundi na wengineo. Sukuma gang siyo kabila ni tabia. Kwani Saambaya au Ndungoi ni wasukuma? Lakini ni Sukuma gang members
Hakuna kitu kama hicho, ni IMAGINATION tu.

Kuna kundi kubwa la wananchi Kwa maelfu wenye njaa ya HAKI, wanapambana kupata mkate Kutoka kundi dogo la wevi na waovu!!!!
 
Magufuli ndio alitengeneza matabaka CCM. Usikatae.
Yalianza zamani makundi, lakini Awamu ya 004 yalikarikaribia kukizamisha chama ndo akaletwa jiwe Ili kubalance.

Umesahau wanamtandao na wapiga deal enzi zile, Ukiwa na mzigo bandarini na hutaki ulipe Kodi unaenda Kwa mtoto wa mkubwa Fulani,

Ulikuwa Bado mdogo enzi hizo au unajitoa ufahamu???
 
Back
Top Bottom