Sikubaliani na aina ya mabadiliko ya viongozi uliofanywa na Rais Samia. Washauri wake wamempoteza

Leo mtu anatolewa hapa anapelekwa kule hakai miezi anahamishwa tenaa hao hao wanajirudia rudia hao haoa najiuliza tuko watu mil 60 hawa Mawaziri tuko nao wote kabisa mimi kwa maoni yangu hakuna anaegfanya kazi yake vizuri kwa kweli hawa wote walikua wa kuwafuta kama kweli una nia ya kujenga nchi kwa mwendo mpya wa kwenda mbele zaidi....
 
Sema kumteua Professor wa Sheria tena Mzee wa Miaka 60+ kuwa waziri wa Michezo , Sanaa na Utamaduni haingii akilini kabisa

Japo Kabudi ni mzee wa hovyo na alichangia sana kwenye awamu ya tano kutunga Sheria kandamizi Ila haiingii akilini kabisa kuwa waziri wa Michezo.
 
unadhani hawajui wanachofanya? siasani mambo ni mengi muda mchache
 
Uwaziri ni kipaji jamani au ile ni platform tu ya kusemea yale uliotakiwa kusema na je usipoteuliwa kama kitu hujui nyamaza
Ndicho alichoongea mtoa mada angeteua kwa kuangalia vipaji,uzoefu au taaluma lakini hao walioteuliwa hawajazingatia vipaji.
Palamagamba ujuzi wake na kipaji chake ni sheria amewekwa kwenye sanaa wewe ulishawahi kumuona hata siku moja anafanya sanaa ya aina yoyote iwe ya kuimba au yoyote ile?
Yaani ni bora hata umteue mrisho mpoto anaweza akakupa strategies na kuleta matunda japo hajawahi kuwa kiongozi.
Kwa kifupi wanapuyanga tu.
 
Uzi ufungwe
 
Hizo sababu unazoziona hana kuteuliwa waziri wa michezo, pengine ndo kigezo cha kuteuliwa yeye kuwa waziri wa michezo. Tusichojua ni uhakika wa sbbu zipi zilizopelekea akateuliwa wizara hiyo, Ila elewa hakuna teuzi inafanywa kwa bahati mbaya kihivyo, kwani wao hawajui Prof ni mbobezi wa Sheria?! Sisi tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini jombaa
 
Waziri sio mtendaji Mkuu wa wizara kijana, kwa Mantiki hio Rais awe mtaalam wa vitu vyote?
Yes sio mtendaji, lkn yeye ndio mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya mwisho kwenye wizara yake. So kama waziri ni kichwa panzi basi na wizara itakuwa inafanya mambo ya hovyo, kinyume na kile inachotakiwa kufanywa kwa faida ya taifa.
 
Nakubaliana na wewe kwa 100% mkuu.
 
Kumbe kuna mabadiliko n hamsemi jaman
 
Raisi na kitengo chake kizima cha ushauri na uteuzi hawajui kabisa rekodi za wateuliwa. Ndomaana Leo anajaribiwa kuwekwa wizara hii, wakiona hafiti wanamuhamisha kungine, huko napo asipofit anarudishwa alipotoka nk.

Yani serikali inafanya majaribu katika mambo ya maana kitaifa. Mwisho wa siku awamu ya miaka mi5 inaisha bila lolote la maana kufanyika.
 
Noma sana aisee... Prof wa jalalani anadhalilishwa na elimu yake πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ila Slaa alikuwa anawezea jaman ile wizara, lakni kwa huyu wa sasa ni hamna kitu. Kuna ndg yangu kapata msaada kupitia huyo waziri Slaa. Mungu ambariki. Tunahitaji kurecorgnize kazi na umakini wa mtu na kumuacha aendelee kufanya kazi yake, kitengo cha kumtoa mchapakazi kumuweka mzembezembe ni kujiondolea credts wewe mwenyewe Rais,. Tuwekee Slaa jaman amesaidia wengi mmoja wapo ni ndugu yangu. Masauni mtoe jamani mpe hata wizara ya utamaduni huko
 
Yaani ni bora hata umteue mrisho mpoto anaweza akakupa strategies na kuleta matunda japo hajawahi kuwa kiongozi.
Kwa kifupi wanapuyanga tu.
Exactly mkuu, hiyo wizara angempandisha cheo mwana FA, ampe wizara kamili aisimamie.
 
Ni kama vile kocha asiejua nafasi za wachezaji wake uwanjani kiasi ya kwamba golikipa anampanga kwenye ushambuliaji, mshambuliaji anapangwa kwenye ukipa, halaf beki anapelekwa kwenye ushambuliaji, mnafikiri team hiyo itaweza kupata ushaindi kweli?!πŸ“ŒπŸ”¨
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…