Sikubaliani na aina ya mabadiliko ya viongozi uliofanywa na Rais Samia. Washauri wake wamempoteza

Sikubaliani na aina ya mabadiliko ya viongozi uliofanywa na Rais Samia. Washauri wake wamempoteza

Ila Slaa alikuwa anawezea jaman ile wizara, lakni kwa huyu wa sasa ni hamna kitu. Kuna ndg yangu kapata msaada kupitia huyo waziri Slaa. Mungu ambariki. Tunahitaji kurecorgnize kazi na umakini wa mtu na kumuacha aendelee kufanya kazi yake, kitengo cha kumtoa mchapakazi kumuweka mzembezembe ni kujiondolea credts wewe mwenyewe Rais,. Tuwekee Slaa jaman amesaidia wengi mmoja wapo ni ndugu yangu. Masauni mtoe jamani mpe hata wizara ya utamaduni huko
Huyu wa sasa ni wa hovyo kuliko mawaziri wote. Jina lake tu pekee wengi hawalijui.
 
Ni kama vile kocha asiejua nafasi za wachezaji wake uwanjani kiasi ya kwamba golikipa anampanga kwenye ushambuliaji, mshambuliaji anapangwa kwenye ukipa, halaf beki anapelekwa kwenye ushambuliaji, mnafikiri team hiyo itaweza kupata ushaindi kweli?!📌🔨
Mkuu tunahutaji busara zako, japo maneno mawili matatu tusonge mbele.
 
Niaje waungwana

Naona raisi Samia kaendelea kuvuruga serikali yake mwenyewe bila kujua madhara yanayoweza kutokea kutokana na uvurugaji wake huo.

Ni kama vile kocha asiejua nafasi za wachezaji wake uwanjani kiasi ya kwamba golikipa anampanga kwenye ushambuliaji, mshambuliaji anapangwa kwenye ukipa, halaf beki anapelekwa kwenye ushambuliaji, mnafikiri team hiyo itaweza kupata ushaindi kweli?!

Binadam tumeumbwa kila mtu na kipaji chake. Ndomaana wenzetu wazungu wakikuona wewe akili yako inaelekea kwenye elimu basi wazazi watakusomesha kwa juhudi na bidii kwa sababu wanajua kwamba huko ndiko Mungu alipoamua akili yako ielekee, hivyo wakiku force kwnye michezo au biashara itakuwa ni kupoteza pesa na muda bure, kwani result yake baadae itakuwa ni tofauti na kipaji chako.

Hiivyo watakuendeleza kwa kile wanachoona kinaendana na akili au kipaji chako. Hakunaga mambo ya kulazimishana au kujaribishana katika sehemu ambayo mtu hafiti wala hana uzoefu nayo.

Mfano UK waziri mkuu unakuta anamteua waziri wa michezo ambae anaijua vizuri michezo, ni mfuatiliaji wa michezo na pengine aliwahi kabisa kuwa mchezaji. Hivyo akipewa nafasi ya wizara ya michezo ana uwezo wa kufanya mambo makubwa katika michezo kwa sababu ya uzoefu wake na kipaji chake katika michezo.

Hivyo hivyo kwa Marekani, Canada, Ujerumani nk mtu anateuliwa katika sehemu ambayo ana uzoefu nayo ili kuondoa kuzorota kwa shughuli za wizara na serikali kwa ujumla, hivyo ni vigumu sana kukuta ujinga ujinga wizarani au mtu kuhamishwa hamishwa wizara nk.

Sasa sisi waafrika tumekuwa tukiwapa watu post ambazo hawana ujuzi wala uzoefu nazo. Tukiamini kwamba kwa vile mtu anaitwa Doctor au Professor basi popote utapomuweka atafiti, matokeo yake mtu anakaa wizarani miaka miwili, mitatu Hadi mitano bila kufanya lolote la maana, maana mtu amewekwa katika sehemu asiyoweza kuimudu na kwa utamaduni wetu mtu hauwezi kukataa post unayopewa na raisi, vile vile mtu hushindwa kumwambia raisi ukweli kwamba post aliyopewa hana uzoefu nayo au hatoweza kuimudu. Yeye atakaa kimya mpaka siku aliemteua atapoona hakuna anachofanya na kumtoa au kumhamisha. Najua kwamba kuna wengine wana vipaji vya ku handle sehemu yoyote wanayowekwa, lakini hao ni wachache sana alafu kibaya huwa hawatulizwi pale wapopaweza.

Mfano mpaka leo watanzania wengi hatuelewi sababu ya raisi Samia kumtoa mchapa kazi Slaa kutoka wizara ya ardhi na kwenda kumtupa kwenye usemaji, au Kabudi kutoka sheria kutupwa katika wizara isiyoendana na taaluma yake. Mwisho wa siku itaonekana kuwa alipopelekwa hakuna anachokifanya, kumbe tatizo na kupelekwa katika post asiyoifahamu.

Mimi ningekuwa raisi Samia basi mabadiliko haya yangemrudisha Slaa ardhi maana tayari kelele za watu kuzulumiwa nyumba, viwanja nk zishaanza kurudi tena upya, huku waziri husika mhe, Ndejembi akiwa hana mbinu yoyote ya kuwadhibiti wezi hao wa ardhi. Clinic za kushughulikia kesi za ardhi ambazo zilianzishwa na waziri Slaa zimekufa kibudu zote, huku wezi wa ardhi wakitembea vifua mbele bila hofu yoyote.

Pia Kabudi angebaki wizara ya sheria na katiba.

Masauni tupa nje na Ndejembi angepewa mambo ya ndani.

Lakini kwa aina ya uteuzi ulivyofanyika ni kama vile washauri wa raisi, raisi mwenyewe pamoja na KMK wanafanya betting katika mambo ya msingi alaf baada ya mwezi mmoja tu au miwili wakiona mambo hayaendi watengue na kuteua tena. Nchi yetu Sasa nafasi nyeti zimekuwa ni za kufanyiwa majaribio... It's very very SAD!

PIA SOMA
- Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais
Nimetaja mara kadhaa hapa JF, mfumo unoumaliza nchi yetu mfumo wa Kleptokrasia.

Ni mfumo unoshikiliwa na mafisadi na unolindwa na vyombo vya usalama.

Na hakuna kitu kibaya kama serikali kuwekwa mfukoni na mafisadi.

Hata watu walosoma nje ya nchi na wenye uzoefu au utaalam wao hawawezi kufanya kazi Tanzania bila kujiunga (kwa lazima) na mfumo wa Kleptokrasia.

Uko sahihi Slaa alipaswa kuachwa pale Ardhi ili asaidie kuondoa matatizo ya ardi ya watu kudhulumiwa ardhi yao.

Kwa jinsi mabadiliko haya yanotokea usijeshangaa kusikia wale ambao waziri Slaa aliwashughulikia kama yule Mzee Masawe au nani vile Swai? wamerudishiwa ardhi au nyumba ambazo walizipora kwa wahanga.

Pia kumpa mzee Kabudi nguli wa sheria na mwalimu wa akina Tundu Lissu, Dr Mwakyembe and Co kwanza ni udhalilishaji wa utu wa mtu na pia ni udhalilishaji wa taaluma husika.

Raisi Samia kama kweli ataka kuongoza kweli kwa dhati nchi hii ni lazima ajitambue kuwa akosea sana uongozi wake, kwani moja ya sifa kuu za uongozi ni kuwa tayari kuona udhaifu na matatizo ulo nayo weye mwenyewe kwanza kabla hata ya kuwasikiliza wale wanojiita washauri.
 
Hizo sababu unazoziona hana kuteuliwa waziri wa michezo, pengine ndo kigezo cha kuteuliwa yeye kuwa waziri wa michezo. Tusichojua ni uhakika wa sbbu zipi zilizopelekea akateuliwa wizara hiyo, Ila elewa hakuna teuzi inafanywa kwa bahati mbaya kihivyo, kwani wao hawajui Prof ni mbobezi wa Sheria?! Sisi tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini jombaa
Sasa hivyo vigezo vyao vya siri ambavyo havionekani na wananchi vina msaada gani kwa Taifa na wananchi kwa ujumla?
 
Hizi clinic ndizo zimemuondoa Jerry Slaa kwenye wizara ya ardhi. Usichokijua ni kwamba serikali hii imewekwa mfukoni na mafisadi ambayo yameteka kila nyanja na kila maamuzi, hata teuzi zinafanywa na mafisadi haya.

Kwa kifupi ni kwamba serikali hii imepigwa kopi ,na kopi ya serikali hii inaendeshwa na mafisadi ambayo yamemtanguliza Abdul mbele. Unamfahamu Abdul??

Na haya mafisadi ndiyo yanaongoza kwa uporaji wa viwanja. Yalipoona huyu Jerry Slaa anataka kuharibu ulaji wao kwa kuanzisha clinic yakaamua abadilishiwe wizara.
Mfano mzuri ni kwamba unapofanya mabadiliko kama hayo ni budi kuzingatia utaalam.

Slaa kwa taaluma amesomea masuala ya mifumo ya tehama (nadhani ni programming na software) hivyo hapo kumpeleka wizara hiyo na mawasiliano na teknolojia ni sahihi ingawa pia kumekaa kimkakati zaidi na pia kuzuga kwa ajili ya 2025.

Mtu ambae kama ni kutatua tatizo la ardhi na ameonekana afaa kwa nafasi hiyo ni Paul Makonda, kwani nae kule Arusha mapema alizindua kliniki kwa ajili ya kutatua matatizo ya ardhi na tumeona mafanikio.

Hivyo cha kufanya ni kuitisha uchaguzi mdogo jimbo la Kigamboni (kwani kupo wazi baada ya kifo cha marehemu Ndugulile) na kisha kumpigia kampeni Makonda na akishinda baadae wampa wizara hiyo kuiongoza.

Wizara ya ardhi ni moja ya wizara ngumu na nyeti hivyo yahitaji watu aina ya Makonda au Slaa kwani wana akili za ziada katika kubuni njia za kutatua matatizo.

Ila Kabudi pamoja na utaalamu wake wa sheria pia aweza kutumika kwa muda ulobaki kabla ya uchaguzi mkuu lakini ni jambo la uzuri endapo atapatikana mtu ambae wampa ubunge wa kuteuliwa kutokana na sifa zake kisha wampa wizara husika.

Nafasi za ubunge wa kuteuliwa ziwe ni nafasi za kutafuta watu wenye utaalam katika maeneo nyeti ambao si wabunge.

Wizara za Ardhi, Mambo ya Ndani, Ujenzi, ni mojawapo ya wizara ambazo mabadiliko yanotokea ulimwenguni yahitaji watu wenye ujuzi na utaalam wa kisasa zaidi.

Sio watu watekwa na kuuliwa waziri yupo kimya, au watu wasimamisha maghorofa na yadondoka baada ya muda fulani lakini waziri wa ujenzi yupoyupo tu.
 
Ila Slaa alikuwa anawezea jaman ile wizara, lakni kwa huyu wa sasa ni hamna kitu. Kuna ndg yangu kapata msaada kupitia huyo waziri Slaa. Mungu ambariki. Tunahitaji kurecorgnize kazi na umakini wa mtu na kumuacha aendelee kufanya kazi yake, kitengo cha kumtoa mchapakazi kumuweka mzembezembe ni kujiondolea credts wewe mwenyewe Rais,. Tuwekee Slaa jaman amesaidia wengi mmoja wapo ni ndugu yangu. Masauni mtoe jamani mpe hata wizara ya utamaduni huko
Masauni atolewe uwanjani akae nje ashike jezi ili wengine wachukue nafasi yake iliyomshinda kwa muda mrefu.
 
Shida kubwa ya nchi yetu viongozi wengi wazuri ndio wanapigwa vita, wale wa hovyo ndio kila siku wanasifiwa.

Angalia kwenye mawizara mpaka taasisi za Serikali, watu wenye akili nzuri na nia ya dhati ya kuisaidia nchi hawapendwi ata kidogo. Tuna safari ndefu sana kama nchi
 
Yaani wewe umeona halafu rais pamoja na taasisi zake zote hazijaona! Unaonekana una kipaji,vipi upewe nchi??

Punguza ujuaji wa kishamba!
Hoja ya kipuuzi bora ungekaa kimya, kwamba mtu akiwa Rais ndio ana akili kuliko watz wooote au
Acha kutishwa na neno Urais ni taasisi hata vilaza wamejaa humo!.
 
Km mawaziri wanatumia uchawi, basi kiboko yao ni Jenister.
Huyu mama kupewa wizara ya Afya, naamini hata Rais haelewi ka mteua vipi ila bas, uchawi wa kingoni umevuka bahari.

Mweeeeh!!
 
Shida kubwa ya nchi yetu viongozi wengi wazuri ndio wanapigwa vita, wale wa hovyo ndio kila siku wanasifiwa.

Angalia kwenye mawizara mpaka taasisi za Serikali, watu wenye akili nzuri na nia ya dhati ya kuisaidia nchi hawapendwi ata kidogo. Tuna safari ndefu sana kama nchi
Yes ni kweli.. ukitaka upendwe sana na system...
A) Achana maswala ya uzalendo.
B) Jiunge na chawa wa mama mwenye nchi.
C) Na sifia CCM kila siku.

Kinyume na hapo elimu yako, uzoefu wako na uzalendo wako havitakusaidia kupata nafasi yoyote ya uongozi nchini.
 
Hoja ya kipuuzi bora ungekaa kimya, kwamba mtu akiwa Rais ndio ana akili kuliko watz wooote au
Acha kutishwa na neno Urais ni taasisi hata vilaza wamejaa humo!.
Exactly mkuu 😂😂😂
 
Km mawaziri wanatumia uchawi, basi kiboko yao ni Jenister.
Huyu mama kupewa wizara ya Afya, naamini hata Rais haelewi ka mteua vipi ila bas, uchawi wa kingoni umevuka bahari.

Mweeeeh!!
Umemsahau na Bashungwa mkuu. Nasikia huko Bukoba kukutana na vyungu vimevunjwa kwenye vinjiapanda vya mkoa ni jambo la kawaida mkuu.
 
Back
Top Bottom