Sikubaliani na aina ya mabadiliko ya viongozi uliofanywa na Rais Samia. Washauri wake wamempoteza

Huyu wa sasa ni wa hovyo kuliko mawaziri wote. Jina lake tu pekee wengi hawalijui.
 
Mkuu tunahutaji busara zako, japo maneno mawili matatu tusonge mbele.
 
Nimetaja mara kadhaa hapa JF, mfumo unoumaliza nchi yetu mfumo wa Kleptokrasia.

Ni mfumo unoshikiliwa na mafisadi na unolindwa na vyombo vya usalama.

Na hakuna kitu kibaya kama serikali kuwekwa mfukoni na mafisadi.

Hata watu walosoma nje ya nchi na wenye uzoefu au utaalam wao hawawezi kufanya kazi Tanzania bila kujiunga (kwa lazima) na mfumo wa Kleptokrasia.

Uko sahihi Slaa alipaswa kuachwa pale Ardhi ili asaidie kuondoa matatizo ya ardi ya watu kudhulumiwa ardhi yao.

Kwa jinsi mabadiliko haya yanotokea usijeshangaa kusikia wale ambao waziri Slaa aliwashughulikia kama yule Mzee Masawe au nani vile Swai? wamerudishiwa ardhi au nyumba ambazo walizipora kwa wahanga.

Pia kumpa mzee Kabudi nguli wa sheria na mwalimu wa akina Tundu Lissu, Dr Mwakyembe and Co kwanza ni udhalilishaji wa utu wa mtu na pia ni udhalilishaji wa taaluma husika.

Raisi Samia kama kweli ataka kuongoza kweli kwa dhati nchi hii ni lazima ajitambue kuwa akosea sana uongozi wake, kwani moja ya sifa kuu za uongozi ni kuwa tayari kuona udhaifu na matatizo ulo nayo weye mwenyewe kwanza kabla hata ya kuwasikiliza wale wanojiita washauri.
 
Sasa hivyo vigezo vyao vya siri ambavyo havionekani na wananchi vina msaada gani kwa Taifa na wananchi kwa ujumla?
 
Mfano mzuri ni kwamba unapofanya mabadiliko kama hayo ni budi kuzingatia utaalam.

Slaa kwa taaluma amesomea masuala ya mifumo ya tehama (nadhani ni programming na software) hivyo hapo kumpeleka wizara hiyo na mawasiliano na teknolojia ni sahihi ingawa pia kumekaa kimkakati zaidi na pia kuzuga kwa ajili ya 2025.

Mtu ambae kama ni kutatua tatizo la ardhi na ameonekana afaa kwa nafasi hiyo ni Paul Makonda, kwani nae kule Arusha mapema alizindua kliniki kwa ajili ya kutatua matatizo ya ardhi na tumeona mafanikio.

Hivyo cha kufanya ni kuitisha uchaguzi mdogo jimbo la Kigamboni (kwani kupo wazi baada ya kifo cha marehemu Ndugulile) na kisha kumpigia kampeni Makonda na akishinda baadae wampa wizara hiyo kuiongoza.

Wizara ya ardhi ni moja ya wizara ngumu na nyeti hivyo yahitaji watu aina ya Makonda au Slaa kwani wana akili za ziada katika kubuni njia za kutatua matatizo.

Ila Kabudi pamoja na utaalamu wake wa sheria pia aweza kutumika kwa muda ulobaki kabla ya uchaguzi mkuu lakini ni jambo la uzuri endapo atapatikana mtu ambae wampa ubunge wa kuteuliwa kutokana na sifa zake kisha wampa wizara husika.

Nafasi za ubunge wa kuteuliwa ziwe ni nafasi za kutafuta watu wenye utaalam katika maeneo nyeti ambao si wabunge.

Wizara za Ardhi, Mambo ya Ndani, Ujenzi, ni mojawapo ya wizara ambazo mabadiliko yanotokea ulimwenguni yahitaji watu wenye ujuzi na utaalam wa kisasa zaidi.

Sio watu watekwa na kuuliwa waziri yupo kimya, au watu wasimamisha maghorofa na yadondoka baada ya muda fulani lakini waziri wa ujenzi yupoyupo tu.
 
Masauni atolewe uwanjani akae nje ashike jezi ili wengine wachukue nafasi yake iliyomshinda kwa muda mrefu.
 
Shida kubwa ya nchi yetu viongozi wengi wazuri ndio wanapigwa vita, wale wa hovyo ndio kila siku wanasifiwa.

Angalia kwenye mawizara mpaka taasisi za Serikali, watu wenye akili nzuri na nia ya dhati ya kuisaidia nchi hawapendwi ata kidogo. Tuna safari ndefu sana kama nchi
 
Yaani wewe umeona halafu rais pamoja na taasisi zake zote hazijaona! Unaonekana una kipaji,vipi upewe nchi??

Punguza ujuaji wa kishamba!
Hoja ya kipuuzi bora ungekaa kimya, kwamba mtu akiwa Rais ndio ana akili kuliko watz wooote au
Acha kutishwa na neno Urais ni taasisi hata vilaza wamejaa humo!.
 
Km mawaziri wanatumia uchawi, basi kiboko yao ni Jenister.
Huyu mama kupewa wizara ya Afya, naamini hata Rais haelewi ka mteua vipi ila bas, uchawi wa kingoni umevuka bahari.

Mweeeeh!!
 
Yes ni kweli.. ukitaka upendwe sana na system...
A) Achana maswala ya uzalendo.
B) Jiunge na chawa wa mama mwenye nchi.
C) Na sifia CCM kila siku.

Kinyume na hapo elimu yako, uzoefu wako na uzalendo wako havitakusaidia kupata nafasi yoyote ya uongozi nchini.
 
Hoja ya kipuuzi bora ungekaa kimya, kwamba mtu akiwa Rais ndio ana akili kuliko watz wooote au
Acha kutishwa na neno Urais ni taasisi hata vilaza wamejaa humo!.
Exactly mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Km mawaziri wanatumia uchawi, basi kiboko yao ni Jenister.
Huyu mama kupewa wizara ya Afya, naamini hata Rais haelewi ka mteua vipi ila bas, uchawi wa kingoni umevuka bahari.

Mweeeeh!!
Umemsahau na Bashungwa mkuu. Nasikia huko Bukoba kukutana na vyungu vimevunjwa kwenye vinjiapanda vya mkoa ni jambo la kawaida mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…