Timu bora kwa hapa nchini ni Yanga, hilo liko wazi.
Maamuzi ya marefa yanazibeba timu nyingi ila kwa timu kama Simba ni too much ndio maana game ikiwa fair anakandwa. Mfano kati yake na Singida na Yanga.
Simba wamjengee sanamu Karia pale mo arena. Hata kama ameshindwa lakini nia yake ya kuisaidia Simba ifike mbali hata kwa kuzishusha timu nyingine ikibidi ilikuwa dhahiri.
Ndugu zangu hata hii kanuni ya kusajiri wachezaji 10 wa kigeni kwa vitabu genesis yake ilikuwa kuisaidia Simba tu na sio timu nyingine. Mipango huu ulipitishwa na Karia wakati ule Yanga inakinga bakuli baada ya Manji kuacha kuwa mafadhili wa Yanga na Simba wamempata mo. Ndicho kipindi ambacho Simba alikuwa bingwa kwa misimu 4 mtawalia.
Kimataifa, TFF iliwapa Simba hadi viporo 11 vya kwenye ligi ili ipate muda wa kushiriki mashindano ya CAF.
Simba ilikamatwa ikiroga kule South Africa lakini TFF haikuwapa adhabu yoyote Simba Wala kalipio.
Kwenye uhamisho wa wachezaji wa ndani na nje TFF iliwapa Simba kipaumbele pale ambapo Kuna utata wa uhamisho na timu nyingine.
TFF imeruhusu Simba ifanye chochote kile ili kupata matokeo ndani na nje ya nchi
TFF inapanga ratiba ya mechi (fixtures) ambayo kama ukivaa miwani yenye lens nzuri utagundua kuwa imezingatia hali ya Simba zaidi.
TFF ya Karia imeruhusu waamuzi wafanye kila liwezekalo Simba ishinde na Yanga ishindwe.
Adhabu za bodi ya ligi ziliihurumia
Simba zaidi kuliko timu nyingine.
Kuleta waamuzi kutoka Misri lilikuwa takwa la Simba kwa Karia
Azam media kuacha kutumia VAR kwenye Ligi Kuna uhusiano na project ya TFF kuisaidia Simba.
Fungakazi ilikuwa pale Simba iliporuhusiwa na TFF/bodi ya Ligi kuahirisha Derby dakila za mwisho bila kujali kitu chochote nchini.
Na msimu ujao ndiyo itakuwa fungakazi.
Ni vizuri ujenzi wa Sanamu lake uanze Sasa.