Haya
Hizo kauli ungeongea kwa timu nyingine ila siyo simba na yanga labda kama umeanza kufuatilia mpira hivi karibuni, hizo kelele zote ni kwa sababu yanga baada ya kudondosha point kwa azam, tabora, jkt na kuona simba wamewakaribia kama kawaida yenu mkaanza zile hesabu zenu za tuki na waki kuna timu mkawa mnategemea ziifunge simba au zitoe naye draw adondoshe point ili ninyi mrahisishiwe kuchukua ubingwa, sasa mlipoona simba anazifunga hizo timu zote mlizozitegemea matokeo yake mkaanza kutafuta visababu mara marefa mara viongozi wa shirikisho na bodi ya ligi mara wachambuzi
Yani nakumbuka hata cafcc pia mlisema simba walifika fainali kwa sababu ya kubebwa na marefa mara sijui walipangwa na timu mbovu kumbe yote hayo mlikuwa hamtaki tu simba wafyeke kichaka chenu cha medali, yani kwa kifupi msimu huu mlihakikisha kila mtu mnamtupia lawama sababu ya ushindi wa simba ili mradi tu ionekane kwamba simba ni timu mbovu na inabebwa, yani haiwezekani timu moja hiyo hiyo kila ikishinda ndio inaonekana inabebwa ila nyingine ikishinda inaonekana ina uwezo na uzuri umesema mwenyewe kwamba mpira ni mchezo wa wazi kila mtu anaona
Kama kweli mlikuwa mnaangalia mechi za simba na siyo kusimuliwa basi nafikiri mlikuwa mnajionea namna wachezaji wa zile timu walivyokuwa wanacheza karate uwanjani na kupoteza muda kimakusudi, kuna wakati hadi nikawa nahisi inawezekana kuna matajiri wanaweka pesa na kuziambia hizo timu kuwa wafanye hayo kwa makusudi ili refa akiwapa simba penati au akiongeza dakika nyingi ionekane wamepata ushindi kwa kubebwa, ndio maana unakuta kuna timu zikicheza na simba wanakamia hadi wanataka kufia uwanjani tofauti na zikicheza na yanga eti mabeki wanajifanya wanapoteza mipira kizembe ndani ya box na kuwaachia kina dube na mzize wamalizie tu golini halafu mkiulizwa huko kimataifa mbona hamuoneshi huo ubora wenu mnakuwa wakali