Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Jamaa ni kocha mzuri, sema tu presha ilimzidi akaachana na falsafa yake. Azam kocha huyo kazi kwenu. Uzuri mna mawinga wazuri wa kutosha na wachezaji wenye Kasi, achana na mifaza ya Simba ile.
Maajabu ya soka la soka la Tanzania ya wajuaji, yaani kocha anafukuzwa huku akiwa na wastani mzuri za ushindi, mechi alizofungwa ni za kuhesabuka haswa. Kocha anafukuzwa kwasababu tu ya kivuli cha Yanga. Watu wanataka Simba iwe kama Yanga uwanjani pasipo kuhoji factors mbalimbali kama viwango vya wachezaji na umri. Kiufupi ubora wa Yanga ndio uliomfanya kocha atimuliwe.
 
Jinsi kalivyo kafupi na kanavyolalamuka kila saa. Kuna siku nilimuuliza oale Element hotel kabla hawajacheza na Waydad. Mgunda yupo wapi nataka niongee naye, kakanijibu huku kananungunuka. Sijui aliniogopa yule mrundi akijua mimi ni miongoni mwa staff wa WAC. Kakaanza kulalamika.
Labda hukujitambulisha vizuri
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Mmemuonea aisee..
 
Back
Top Bottom