Simuungi tena mkono Rais Samia kwa haya yanayoendelea na kadhia ya Mafuta

Aise. Wewe jamaa sijui kwann teuzi zote zinakupita maana siyo kwa uchawa huo. Halafu unatudhalilisha wanaume.
 
Tatizo wana JF Hamfiki ata robo ya idadi ya wananchi... Kumnyima mama kura hakusaidii... Dua ndio mkombozi pekee...
Jf ni kama indicator moja wapo ya watawala kujua wanakubalika au hawakubaliki mbele ya watanzania mill 60
 
Rais Samia anafaa ila nakubaliana na mtoa hoja kwenye mambo ya msingi, Rais lazima atoe sauti ya kimamlaka kwenye hili naunga mkono 100%, tabia ya lugha nawaombeni Tanzania haiendi hivyo, sisi ukisikia mtu anasema naomba unifanyie hivyo basi tunachukulia udhaifu nadhani kuna ulazima tone ibadilike. Haya na hili mkaliangalie tutafika tumechoka sana. Nchi inataka sauti ya kimamlaka lazima uwe katili kidogo.
 
Mimi binafsi sina rafiki na adui wa kudumu rais Samia watendaji wake wanamuangusha sana uenda ni makusudi hili 2025 wambandue awe making Hali ikiendelea hivi watu wataonesha kukukubali kwa maandishi tu lakini mioyoni mwao ni kinyume kabisa. Chukua dkt mshenga nafikili yupo kwenye kitengo Cha uvuvi Zanzibar mpatie kitengo hapo unishatini autojutia jamaa jembe linajua kupiga kazi
 
Sema tu hana uwezo wa kusimamia .acha kumsugarcoat
 
Kwani wewe unadhani CCM wanategemea sanduku la kura? Sanduku lao la kura ni TISS na Polisi, wewe upige, usipige, mammoja. CCMwanaamua nani awe nani, angalia walivyotengeneza bunge kibogoyo la Ndiyooooo, kwa kura za kupita bila kupingwa. Tubadilishe kwanza mfumo wa upatikanaji wa Rais na viongozi wengine kwa kubadili katiba mbovu iliyopo na kuleta mpya.
 
Mwite mwenzako The Boss na Lord denning ..

Taratibu wataelewa tu..
 
Ni jambo lisilopingika kuwa watu wasio na ufahamu na wasiojitambua ndo watasimama kumuunga mkono mbunifu wa maumivu ya taifa.

Rais anaishia kuteua na kutengua na kulalamika lalamika. Hachukui hatua kurekebisha kasoro na shida za wananchi yeye anaishia kuwashughukikia wanaomkosoa na kumpinga.

Ninaishi uraiani, walio wengi hawamuungi mkono na wameshaona kabisaa namna alivyokaa mbali na shida za wananchi. Yeye anaishi ikulu na kikundi kidogo cha watu akiamini huko nje yeye ni kinara.

Amejitwalia umungu mtu.
Amejitwalia mamlaka dhidi ya katiba
Amejikweza juu kabisa na hataki kukosolewa

Mene Mene Tekeli na Peresi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…