Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Hayo ni matatizo ya "Status Anxiety".Mpaka mkongwe umekuja hapa nisamehe mkuu kuna madogo wanaleta dharau na vilaki laki vyao 😀
Hutokea sana kwa watu ambao ndiyo kwanza wameanza kushika pesa.
Wafaransa wanawaita "Nouveau Riche". Haya ni maneno ya dharau kusema huyu ni mtu mshamba ambaye kaanza kushika pesa karibuni bado zinamzuzua, hajazizoea na kuziona kitu cha kawaida.
Johnny Come Lately. Kaja na mbio za mwenge.
Kwa watu wengi wanaojitambua na waliozikuta pesa kwao tangu wanazaliwa, wanakuwa mpaka wanasahau kuwa pesa ni kitu muhimu, kwa sababu zipo tu.
Wanatambua kuna vitu muhimu zaidi ya pesa.
Mahusiano, heshima, legacy, kutambulika.
Kuna binamu yangu mmoja alikuwa anasema matatizo ya kweli hayamalizwi kwa pesa, kinachomalizwa kwa pesa ni gharama tu, si tatizo la kweli.
Mfano, tatizo la gharama ni kukosa pesa za kukutibu ugonjwa. Tatizo la kweli lililopita gharama ni kuwa na ugonjwa usio na dawa wala kinga.
Ndiyo maana unaweza kuwa na pesa ukashindwa kuingia club ya members only, kwa sababu hapo kinachohitajika kuingia si pesa, ni membership.
Au unaweza kuwa na pesa, halafu usisikilizwe, akasikilizwa mzee mmoja tu ambaye hana pesa kama wewe ila anajulikana na kukubalika.
Kuna sehemu nyingine pesa is the bare minimum metric.