Anhaa nishaujua huu mchezo, ngoja!Shida una haraka na huyo mwanamke ndio maana unatumia gharama kubwa ila mwanamke ukiwa hauna haraka nae na ukamtengenezea mazingira mazuri ili kumfanya awe comfortable na wewe huwezi kutumia hizo gharama kubwa ni vile tu mnakaza fuvu ndio maana mnaangukia kwa wadangaji halafu mnajiita mna mademu. Mwanzoni mwa mahusiano yenu ndio yanadetermine mtaishi mahusiano ya namna gani ili lazima ujue ukimzoesha mwanamke pesa mwanzoni kabisa kuanzia date yenu mpaka kwenye mahusiano ya mwanzoni ndivyo huyo mwanamke atakuwa hivyo hivyo
Hata kuongea naye lolote siwezi😂Mwandiko wa aina hii unadogosha sana hadhi ya mtu. Hauwezi kumchukulia serious kwa jambo lolote, achilia mbali mahusiano.
Nampamba ili atume Spika yake jamvini.Unampa airtime huyo mbuzi katoliki
Unataka kuichezea bwasheeNampamba ili atume Spika yake jamvini.
Tunafunga pm ili kukwepa kutumiwa vitu watu wachache na hii ni Jamii + forum na sera yake ya kufanya mambo kwa uwazi.Unataka kuichezea bwashee
Kila mtu na namna ya utokaji wake😆Nampamba ili atume Spika yake jamvini.
Inaonyesha ww sio mtoto wa Daslam umetokea polini asee karibu nikupe code.Niaje wakuu?
Nimekaa hapa nikiwa nimeshika simu yangu mkononi, huku nikitazama screen na kushusha pumzi ndefu. Kila nikikumbuka ujumbe wa makato ya miamala na madeni niliyoyaingiza wiki chache zilizopita, nasikia maumivu mapya kabisa moyoni.
Siyo kwamba nina matatizo ya kiuchumi ya kuzaliwa, hapana! Tatizo langu lilianza pale nilipoamua kufanya majaribio ya kutongoza mtoto wa mtu mjini hapa
Zamani nilikuwa najiambia, "Mimi ni mwanaume, lazima nionyeshe msisimko wa mfuko." Nikajifanya mwamba. Nikakutana na binti mmoja mrembo ambaye picha zake za mitandaoni zinasema kabisa yeye ni wa hadhi ya juu.
Ili nionekane najiweza, nikamualika mtoko wa kwanza (first date). Kilichofuata kilikuwa ni somo la maisha ambalo sitasahau.
Siku ya miadi, binti alikuja. Lakini hakuja peke yake; alikuja na "mashoga zake wawili" ambao walikuwa na njaa kama wametoka vitani.
Tulipofika sehemu ya chakula, mimi nilitegemea tutaagiza vitu vya kawaida tu vya kueleweka. Lakini wapi! Walianza kutaja majina ya vyakula vya Kizungu ambavyo hata kuvitamka siwezi, pamoja na vinywaji vinavyoletwa vikiwa vimepambwa kwa matunda na maua juu yake.
Kila agizo lilipotua mezani, nilikuwa napiga hesabu ya haraka haraka kichwani. Jasho jembamba lilianza kunitoka chini ya kiyoyozi. Wakati bili inakuja, macho yangu yaliona ukungu. Kiasi kilichopo kwenye ile karatasi kilikuwa kirefu kuliko bajeti yangu ya mwezi mzima!
Ili kulinda heshima yangu na isionekane nimeishiwa, ilibidi nianze kufanya sarakasi za kukopa kwa dharura kwenye vikundi na App za mikopo ya haraka huku nikiwa nimejifungia chooni.
Nililipa ile bili kwa uchungu mkubwa, nikawalipia na usafiri wa kurudi kwao, kisha nami nikarudi kwangu nikiwa mnyonge kama kuku aliyenyeshewa mvua.😁
Kufika nyumbani, nikajisemea "Inatosha." Kesho yake binti akanitumia meseji: "Asante kwa jana dear,tulienjoy sana. Wikiend hii tunaenda wapi tena?" Nilichofanya ni kuifuta ile namba, kisha nikakaa chini na kutafakari maisha yangu
Niliamua kuchukua uamuzi mgumu lakini wa busara kwa usalama wa akili yangu na pochi yangu. Kuanzia leo, nimejitoa rasmi kwenye mashindano ya kutafuta mapenzi ya gharama.
Akili yangu yote sasa hivi nimeielekeza kwenye kutafuta pesa na kujenga maisha yangu kwanza.
Moja ya vijana wa mjini wanaojivunia "O" yake.Kila mtu na namna ya utokaji wake😆
Anajichimbia kaburi lake, kumbe nchi haina raisi duh🙆🏽♀️Moja ya vijana wa mjini wanaojivunia "O" yake.
Fatilia vyema atakua anatokea tabata huyoAnajichimbia kaburi lake, kumbe nchi haina raisi duh🙆🏽♀️
TemekeFatilia vyema atakua anatokea tabata huyo
Nae aanze kuendesha baiskeli uchi akidai haki zakeTemeke
WiFi imekata huyo!Nae aanze kuendesha baiskeli uchi akidai haki zake
Usikubali mwanamke aku'dictate kwenye swala la wapi mka'spend na kuwekana.Kwa maisha ya Tanzania, mahusiano ni kama hasara kwa Mwanaume
Kuanzia dinner dates, hadi faragha za hotel
Kuna jamaa niliona anakimbia bill za mrembo aliyetoka naye dinner hotel x hapa DSM
Binti wa watu akalazimika kuacha simu janja yake ili ku-cover gharama za chakula alichoagiza
Ni vizuri kuwa muwazi kwa mwenzio hasa mnapotoka out hasa eneo la bajeti yako
Mwambie kabisa baby tunatoka, ila nina kiasi cha shilingi 50,000 pekee kwaajili yetu
Yeye ndiyo apime, aje mwenyewe ama abebe timu yake 🙌
Alilipaje gharama zako kwamba alirejesha hela au?? Me nikimwambia mwanamke tutoke alafu aseme hana nauli ni bora tusionane tu! Wanawake hawana huruma na wanaume maskini hivyo na sisi wanaume tunabidi kuwa hivyo hivyo✌🏽Usivunjike moyo mkuu,,kumshawishi binti ya mtu hadi aamue kukuvulia nguo unahitaji uvumilivu wa hali ya juu..
Mimi mwenzio yalinikuta kama wewe,nilimwita mmoja wakaja 2, tena wali request bolt boda toka Goba hadi shekilango kila mmoja na yake.,
Nikalipa bila kinyongo,,walikula na kunywa..
Nilimnyatia hadi akaingia kingi..nikajilipa gharama zngu...
Usikate tamaa mkuu , wanawake wa sasa ndivyo walivyo wanapenda sn kupima level ya kina cha maji kabla hawajayaoga.