Sitokaa nitongoze mtoto wa mtu! Hili lililo Nikuta limenifunza kitu MJINI hapa

Binafsi naona huyo malaya yupo sahihi kufanya alichofanya.
Yuko vizuri huyo Demu Hana shida, kwani alishamsoma huyu Msukuma Mshamba Tu, kwa sababu mtu anapotoka mpaka anakuja ushajia anakuja Peke yake au na Marafiki, sasa inakuwaje Mtoto jamaa anashtukizwa? Demu mjanja, hizo hele alizopata posho ya Mwenye amegawana na wanyonge wa uswazi
 
Mabinti kama hao ndo wanahitajika ili kuwaweka sawa kiakili sisi wanaume tusio na akili timamu
 
Niaje wakuu?
Nimekaa hapa nikiwa nimeshika simu yangu mkononi, huku nikitazama screen na kushusha pumzi ndefu. Kila nikikumbuka ujumbe wa makato ya miamala na madeni niliyoyaingiza wiki chache zilizopita, nasikia maumivu mapya kabisa moyoni. Siyo kwamba nina matatizo ya kiuchumi ya kuzaliwa, hapana! Tatizo langu lilianza pale nilipoamua kufanya majaribio ya kutongoza mtoto wa mtu mjini hapa.
Zamani nilikuwa najiambia, "Mimi ni mwanaume, lazima nionyeshe msisimko wa mfuko." Nikajifanya mwamba. Nikakutana na binti mmoja mrembo ambaye picha zake za mitandaoni zinasema kabisa yeye ni wa hadhi ya juu. Ili nionekane najiweza, nikamualika mtoko wa kwanza (first date). Kilichofuata kilikuwa ni somo la maisha ambalo sitasahau.
Siku ya miadi, binti alikuja. Lakini hakuja peke yake; alikuja na "mashoga zake wawili" ambao walikuwa na njaa kama wametoka vitani. Tulipofika sehemu ya chakula, mimi nilitegemea tutaagiza vitu vya kawaida tu vya kueleweka. Lakini wapi! Walianza kutaja majina ya vyakula vya Kizungu ambavyo hata kuvitamka siwezi, pamoja na vinywaji vinavyoletwa vikiwa vimepambwa kwa matunda na maua juu yake.
Kila agizo lilipotua mezani, nilikuwa napiga hesabu ya haraka haraka kichwani. Jasho jembamba lilianza kunitoka chini ya kiyoyozi. Wakati bili inakuja, macho yangu yaliona ukungu. Kiasi kilichopo kwenye ile karatasi kilikuwa kirefu kuliko bajeti yangu ya mwezi mzima!
Ili kulinda heshima yangu na isionekane nimeishiwa, ilibidi nianze kufanya sarakasi za kukopa kwa dharura kwenye vikundi na App za mikopo ya haraka huku nikiwa nimejifungia chooni. Nililipa ile bili kwa uchungu mkubwa, nikawalipia na usafiri wa kurudi kwao, kisha nami nikarudi kwangu nikiwa mnyonge kama kuku aliyenyeshewa mvua.😁
Kufika nyumbani, nikajisemea "Inatosha." Kesho yake binti akanitumia meseji: "Asante kwa jana dear,tulienjoy sana. Wikiend hii tunaenda wapi tena?" Nilichofanya ni kuifuta ile namba, kisha nikakaa chini na kutafakari maisha yangu.
Niliamua kuchukua uamuzi mgumu lakini wa busara kwa usalama wa akili yangu na pochi yangu. Kuanzia leo, nimejitoa rasmi kwenye mashindano ya kutafuta mapenzi ya gharama. Akili yangu yote sasa hivi nimeielekeza kwenye kutafuta pesa na kujenga maisha yangu kwanza.
Kuna Uzi kakufungulia Jana humu utafute.Ninhekuwa mimi juo msala ninhewaachia wao.Ningeaga nenda kwa WAKALA kitoa pesa afu wasingeniona tena
 
Attachments

  • Screenshot_20260914-093510.png
    Screenshot_20260914-093510.png
    166.2 KB · Views: 10

Hivi huwa mnatuonaje na hizi story zenu za kutunga?

Uko mahala pa gharama ambapo hukutegemea kuletwa hapo...ukaingia toilet fasta ukakopa kwenye app za mtandaoni ili ulipie bili!...( kwa maelezo yako bili si chini ya 450-500k)

NOTE!!! KAMPUNI NYINGI ZA MTANDAONI TOFAUTI NA KAMPUNI ZA SIMU..HAWAWEZI KUKUKOPESHA KIASI KIKUBWA KWA MARA YA KWANZA!

Unatuonaje?!

Kampuni nyingi za mtandaoni huanzia 10,000-30,000/=
Na unatakiwa uwe na NIDA! Papo hspo!Tuseme wewe unatembea na NIDA KILA UENDAKO!
 
Ni akili za kijinga tuu, sasa kwenye maisha yako ukishakula na kunywa kwa namna hiyo unabadilije maisha yako?
Unabaki ombaomba wa kila wiki.
Kwamba? .....sasa kutongoza kila siku kuna faida gani, any way ni mawazo yako mkuu.
 
Una maana kutembea na sugar daddy kunatakiwa uwe mwanamke jasiri??
mwanamke anayetembea na mtu umri wa baba yake kwa sababu ya pesa maana yake huyo amejilipua hayuko kawaida ni potelea mbali.
Ni sawasawa na hawa vijana wa kiume wanaovizia mishangazi kutoa huduma ili wapate pesa kichwani huwa hawako sawa
 
Bora hata ungemualika nyumbani kwako Kwanza, visichana vya hivyo huwa havikatai popote vinakuja AU kama ulipendelea mtoko basi ungekuwa very clear kuwa nataka uje peke yako halafu Hata hivyo hata angekuja peke Yake bado njaa ni njaa tu still angekutia majuto

Mbona kuna wanawake wako very smart Hadi juice anaona tabu kuagiza....Ulikutana na njaa njaa halafu ww mwenyewe Huna Hela lazima uone nyota nyota, yaani siku nyingine kama mfuko mbovu nenda restaurant za kawaida but zipo class Hazina mambo mengi ya uzungu mwingi, akila Sana basi laki mbili maana hamalizi kuku mzima wala glass mbili za juisi
 
Niaje wakuu?
Nimekaa hapa nikiwa nimeshika simu yangu mkononi, huku nikitazama screen na kushusha pumzi ndefu. Kila nikikumbuka ujumbe wa makato ya miamala na madeni niliyoyaingiza wiki chache zilizopita, nasikia maumivu mapya kabisa moyoni. Siyo kwamba nina matatizo ya kiuchumi ya kuzaliwa, hapana! Tatizo langu lilianza pale nilipoamua kufanya majaribio ya kutongoza mtoto wa mtu mjini hapa.
Zamani nilikuwa najiambia, "Mimi ni mwanaume, lazima nionyeshe msisimko wa mfuko." Nikajifanya mwamba. Nikakutana na binti mmoja mrembo ambaye picha zake za mitandaoni zinasema kabisa yeye ni wa hadhi ya juu. Ili nionekane najiweza, nikamualika mtoko wa kwanza (first date). Kilichofuata kilikuwa ni somo la maisha ambalo sitasahau.
Siku ya miadi, binti alikuja. Lakini hakuja peke yake; alikuja na "mashoga zake wawili" ambao walikuwa na njaa kama wametoka vitani. Tulipofika sehemu ya chakula, mimi nilitegemea tutaagiza vitu vya kawaida tu vya kueleweka. Lakini wapi! Walianza kutaja majina ya vyakula vya Kizungu ambavyo hata kuvitamka siwezi, pamoja na vinywaji vinavyoletwa vikiwa vimepambwa kwa matunda na maua juu yake.
Kila agizo lilipotua mezani, nilikuwa napiga hesabu ya haraka haraka kichwani. Jasho jembamba lilianza kunitoka chini ya kiyoyozi. Wakati bili inakuja, macho yangu yaliona ukungu. Kiasi kilichopo kwenye ile karatasi kilikuwa kirefu kuliko bajeti yangu ya mwezi mzima!
Ili kulinda heshima yangu na isionekane nimeishiwa, ilibidi nianze kufanya sarakasi za kukopa kwa dharura kwenye vikundi na App za mikopo ya haraka huku nikiwa nimejifungia chooni. Nililipa ile bili kwa uchungu mkubwa, nikawalipia na usafiri wa kurudi kwao, kisha nami nikarudi kwangu nikiwa mnyonge kama kuku aliyenyeshewa mvua.😁
Kufika nyumbani, nikajisemea "Inatosha." Kesho yake binti akanitumia meseji: "Asante kwa jana dear,tulienjoy sana. Wikiend hii tunaenda wapi tena?" Nilichofanya ni kuifuta ile namba, kisha nikakaa chini na kutafakari maisha yangu.
Niliamua kuchukua uamuzi mgumu lakini wa busara kwa usalama wa akili yangu na pochi yangu. Kuanzia leo, nimejitoa rasmi kwenye mashindano ya kutafuta mapenzi ya gharama. Akili yangu yote sasa hivi nimeielekeza kwenye kutafuta pesa na kujenga maisha yangu kwanza.
Usipotongoza UTATONGOZWA😄😄😄😄
 
Izo mbanga tuachie sisi endelea kutafuta pesa.!!
Nmewahi kudate na pisi moja ya argentina ilikua ni flight attendant aisee ilikaa mwezi mzima nilpokuja kupiga hesabu nilzotumia zilikua zaidi ya 30m za kitanzania. Ile pisi ilikua imenyooka sana sijutii chochote
 
Usivunjike moyo mkuu,,kumshawishi binti ya mtu hadi aamue kukuvulia nguo unahitaji uvumilivu wa hali ya juu..
Mimi mwenzio yalinikuta kama wewe,nilimwita mmoja wakaja 2, tena wali request bolt boda toka Goba hadi shekilango kila mmoja na yake.,
Nikalipa bila kinyongo,,walikula na kunywa..
Nilimnyatia hadi akaingia kingi..nikajilipa gharama zngu...
Usikate tamaa mkuu , wanawake wa sasa ndivyo walivyo wanapenda sn kupima level ya kina cha maji kabla hawajayaoga.
Mwanamke anayekupenda hawezi kukufanyia hivyo hata kidogo ukiona unatumia nguvu kubwa kumpata tena kwa gharama ujue huyo sio kwaajili yako hata kama utanikiwa kuwa hautakuwa mwenyewe
 
Dwa ya kudeal na Mwanamke wa aina yoyote be it from Masaki, Obay au Tandika, sema Tu Sina bajeti kubwa, na chakula au kinywaji chagua wewe, mwanzoni utaogoa kuachwa lakini huo ndio Wanaume na utakapoweza Tu kujisimamia utauona kabisa huyo Demu hatkuach kwa sababu hiyo.

Soma Uzi wangu wa " Wanawake wanaojiita Hugh class"

Ukiona Msichana anakula mashoga zake wake watafune jasho lako bila wewe kuwaalika ujue amekudharau sana, na kabla hawajaja wameshakujadili kuna Fala mmoja mejichanganya twende kumkomesha🤣🤣
Wewe ndio umemaliza kila kitu nipe link ya huo uzi wako nipitie
 
Back
Top Bottom