Siyo siri Rais Samia alianza vizuri, sasa analikoroga

Baada ya kipindi cha Magufuli Awamu ya Tano, alipoingia mama Samia , wengi tulivuta pumzi ya uafadhali kisiasa. Pamoja na kuwa mwana CCM, Awamu ya Tano iliyokuwa a One Man Show, kila mtu alikula mboko.

Sasa tunaona mambo yanataka kujirudia tena.
Power has gone to the head, mama hasikilizi ushauri ulio wazi.

Sina haja ya kurudi kwenye saga la DP World, wamesema wengi.
Wamo wanasiasa, wataalam, wapinzani, but the lady is not for turning.

Sasa tunarudi kule kule kwenye machungu ya Awamu ya Tano.
Ubambikaji kesi nzito nzito ili kuzima mihemuko ya kisiasa umerudi.
Wasiojulikana wamerudi.
Watu sasa wanawekwa ndani kwa kesi za kufikirika.
Hii hali haiwezi kuwa endelevu kisiasa.
Katika demokrasia, hata mtu ukifanya vizuri watu watasema tu.

Kwa nini tumefikia hapa?
Inaelekea kuna makubwa zaidi nyuma ya hili sakata Dp World, lakini tutazame mbele. Wengi tunapenda uwekezaji, lakini kwa masharti ya Taifa letu.
Hilo ni bottom line.
Na niwe mkweli tu, sakata la DPW mama Samia limemuondolea umaarufu wa kisiasa.

Mama inabidi aende retreat, awe na washauri wake wa kisiasa na ni vema akajitazama kwenye kioo hicho cha kisiasa.

2025, tunataka kumpa mama Samia kura za uhakika, si kura za kubebwa kwenye rambo na viroba na wasiojulikana.

Mama Samia alianza vizuri, kwa sasa hivi analikoroga.

Kiti cha Ikulu kinawehusha
 
..kutumia POLISI ni dalili za Samia na genge lake kushindwa kujenga hoja zenye ushawishi.

..wananchi wanaelekea kusikiliza na kukubaliana zaidi na hoja za wapinga mkataba wa Dp World kuliko hoja za wanaomuunga mkono Samia.

..vilevile wanaounga mkono Dp World wanaonekana kuchoka na kukata tamaa. Hawaonekani kuwa na ari na mwamko kama wenzao wanaopinga.

..jambo lingine baya ni Samia kuruhusu watu wa hovyo-hovyo kuwa mstari wa mbele kumsemea na kumtetea.

..Haileti picha nzuri kwa kiongozi wa nchi kutetewa na watu wahuni na wasiofaa ktk jamii.
Watu wa CCM wamezunguka nchi nzima kuelezea upotoshaji

Serikali ime elezea

Wapingaji wameenda mahakamani wameshindwa.

Hapo sasa ni sawa na mtu anaeonyeshwa rangi nyeupe, yeye anakadhana anaona nyeusi; kuendelea kujibizana na mtu kama huyo ndio kukosa muda.

Bandari aina shida yoyote na awajakamatwa kwa sababu ya bandari; isipokuwa kauli zao.
 
Bandari aina shida yoyote

..sasa kama Serikali / Ccm wamewaelimisha wananchi na wameeleweka kwanini wanatumia POLISI?

..Mara nyingi CCM hutumia POLISI pale inapokuwa imezidiwa kwa hoja na vyama vya upinzani.

..Mama alikosea kutanguliza WAHUNI kutetea huu mkataba, na sasa amepoteza imani na ushawishi ktk suala hili.
 
Sawa mwana CCM....ila kila kitu kina mwisho.
 
Baada ya kipindi cha Magufuli Awamu ya Tano, alipoingia mama Samia , wengi tulivuta pumzi ya uafadhali kisiasa. Pamoja na kuwa mwana CCM, Awamu ya Tano iliyokuwa a One Man Show, kila mtu alikula mboko.

Sasa tunaona mambo yanataka kujirudia tena.
Power has gone to the head, mama hasikilizi ushauri ulio wazi.

Sina haja ya kurudi kwenye saga la DP World, wamesema wengi.
Wamo wanasiasa, wataalam, wapinzani, but the lady is not for turning.

Sasa tunarudi kule kule kwenye machungu ya Awamu ya Tano.
Ubambikaji kesi nzito nzito ili kuzima mihemuko ya kisiasa umerudi.
Wasiojulikana wamerudi.
Watu sasa wanawekwa ndani kwa kesi za kufikirika.
Hii hali haiwezi kuwa endelevu kisiasa.
Katika demokrasia, hata mtu ukifanya vizuri watu watasema tu.

Kwa nini tumefikia hapa?
Inaelekea kuna makubwa zaidi nyuma ya hili sakata Dp World, lakini tutazame mbele. Wengi tunapenda uwekezaji, lakini kwa masharti ya Taifa letu.
Hilo ni bottom line.
Na niwe mkweli tu, sakata la DPW mama Samia limemuondolea umaarufu wa kisiasa.

Mama inabidi aende retreat, awe na washauri wake wa kisiasa na ni vema akajitazama kwenye kioo hicho cha kisiasa.

2025, tunataka kumpa mama Samia kura za uhakika, si kura za kubebwa kwenye rambo na viroba na wasiojulikana.

Mama Samia alianza vizuri, kwa sasa hivi analikoroga.
Upole wa kiongozi wa nchi una mipaka yake. Ana mwili wa nyama na uvumilivu wa binadamu huwa na kikomo chake.

Unapomtusi rais au unapokuja na habari ya upotoshaji wa wazi nafsi yako na iwe ya kwanza kukusuta kuwa unachokifanya ni cha hovyo.
 
Namkataa Magufuli Kwa sababu alikuwa hajui ki handle uchumi huo ndio ugomvi wangu nae ila sio siasa uchwara.

Watu wanaleta uzushi na taharuki uwachekee wa nini?

Na nimewaambia siku nyingi kwamba political brutality Africa sio shida so long as Uchumi is doing well,mifano Iko Mingi sana na wewe unajua.

Magufuli alikuwa anagombana na Kila mtu worse enough wawekezaji na wafanyabiashara.
Kwa huyu mamako ni uchumi upi anaotengeneza?
 
..suala hili limetuonyesha UHALISIA wa Samia Suluhu Hassan.

..wakati wote alikuwa akifeki-feki sasa ndio tumemjua uwezo wake, falsafa zake, na maadili yake.

..hili suala alitakiwa ajitokeze kulitolea ufafanuzi, lakini muda wote amejificha.

..watangulizi wote walipofanya jambo kubwa kama hili walijitokeza na kulitetea na kulifafanua.
Nafikiri limemgusa kwa kuhusika by 100%.
 
Upole wa kiongozi wa nchi una mipaka yake. Ana mwili wa nyama na uvumilivu wa binadamu huwa na kikomo chake.

Unapomtusi rais au unapokuja na habari ya upotoshaji wa wazi nafsi yako na iwe ya kwanza kukusuta kuwa unachokifanya ni cha hovyo.
Ni mjinga tu anayeweza kuamini kuwa tusi ni uhaini.
Hata kusuka kitu inabidi uwe na akili!
 
Nyamaza hujui kitu. Mama anafanya vizuri kabisa. Watanzania tunamuombea adumu mpaka 2035 na ikipendeza tutabadili katiba ili atawale mpaka atakaposema kachoka mwenyewe.
FqDMpTMX0AAXivc.jpeg
 
Ulitaka wajibiwe vipi bandari zote zimeuzwa wakati sheria ipo wazi?

Kama hoja Lissu alikuwa anatamka mbele ya polisi mama yenu kauza bandari na uongo kibao mbona yupo huru.

Nimekuuliza swali nani analipia hizo gharama za kufungua kesi za kina Mwakabusi hujui? Nimekuuliza umeshawahi kuingia na kusikiliza mijadala yao ujajibu.

Nilipokwita poyoyo uelewi kwanini wamekamatwa umekasirika; jibu kwanza nani analipia gharama za kina Mwakabusi na kama umesikiliza mijadala ya hao watu.

Nimekuuliza kwanini Lissu hataki uhusiano wa karibu na kundi la kina Mwakabusi na Dr Slaa ujajibu.

Sasa kwanini tuendelee kujibizana wakati hujui hata hakina wapo nyuma ya huyo Mwakabusi wakati ni jambo la wazi kama unafuatilia siasa na kwanini uongozi wa CDM unakaa nao mbali wanaojua madhara ya kauli zao publicly.
Serikali imegundua imefanya kinyume cha sheria na ndiyo sababu imeamua kupeleka bungeni muswada wa amendment katika kikao kijacho ili kuhalalisha ufedhuli wao! Uliona wapi mkataba unasainiwa halafu Sheria ya kuhalalisha inafuata!

Kuhusu gharama za kesi Mwambukusi and co. walianza kwa fedha zao baadaye wananchi wakawaunga mkono kwa kuwachangia ingawa mahakama imeamua mlalamikiwa na mlalamika wajigharimie wenyewe!

Leo hii mawakili wenzake wa Mwambukusi wame- file request for appeal kwa gharama zao na wanaowaunga mkono. Kwa hiyo gharama za kesi siyo issue wananchi watagharimia.

Chadema haijawatenga na ndiyo sababu Mdude yupo nao bega kwa bega, ulitaka viongozi wote wa Chadema wahamie Mbeya?
 
Baada ya kipindi cha Magufuli Awamu ya Tano, alipoingia mama Samia , wengi tulivuta pumzi ya uafadhali kisiasa. Pamoja na kuwa mwana CCM, Awamu ya Tano iliyokuwa a One Man Show, kila mtu alikula mboko.

Sasa tunaona mambo yanataka kujirudia tena.
Power has gone to the head, mama hasikilizi ushauri ulio wazi.

Sina haja ya kurudi kwenye saga la DP World, wamesema wengi.
Wamo wanasiasa, wataalam, wapinzani, but the lady is not for turning.

Sasa tunarudi kule kule kwenye machungu ya Awamu ya Tano.
Ubambikaji kesi nzito nzito ili kuzima mihemuko ya kisiasa umerudi.
Wasiojulikana wamerudi.
Watu sasa wanawekwa ndani kwa kesi za kufikirika.
Hii hali haiwezi kuwa endelevu kisiasa.
Katika demokrasia, hata mtu ukifanya vizuri watu watasema tu.

Kwa nini tumefikia hapa?
Inaelekea kuna makubwa zaidi nyuma ya hili sakata Dp World, lakini tutazame mbele. Wengi tunapenda uwekezaji, lakini kwa masharti ya Taifa letu.
Hilo ni bottom line.
Na niwe mkweli tu, sakata la DPW mama Samia limemuondolea umaarufu wa kisiasa.

Mama inabidi aende retreat, awe na washauri wake wa kisiasa na ni vema akajitazama kwenye kioo hicho cha kisiasa.

2025, tunataka kumpa mama Samia kura za uhakika, si kura za kubebwa kwenye rambo na viroba na wasiojulikana.

Mama Samia alianza vizuri, kwa sasa hivi analikoroga.
Wanaolikoroga wamekaa pembeni wanasubiri alinywe limtokee puani
 
Ni mjinga tu anayeweza kuamini kuwa tusi ni uhaini.
Hata kusuka kitu inabidi uwe na akili!
Biden kule USA kauwa mwanaharakati mmoja mjuaji kama hawa wanaotukana hovyo hapa Tanzania.

Madonna aliwahi kumtukana Trump mbele ya hadhara na wazee wa FBI wakamwambia afute kauli yake na akaifuta hadharani mambo yakaisha.

Wapo unaoweza kuwatukana lakini madaraka ya rais ni lazima yaheshimiwe.
 
Kwa huyu mamako ni uchumi upi anaotengeneza?
Maelfu ya Ajira
Maelfu ya wawekezaji
Maelfu ya Kilimo chenye Tija
Maelfu ya miundombinu ya kila sekta
Maelfu ya wafanyabiashara
Mapato ya Serikali mara dufu

Kiufupi hakuna takataka yeyote wa kumzodi Samia kwenye Uchumi na social services
 
Nyamaza hujui kitu. Mama anafanya vizuri kabisa. Watanzania tunamuombea adumu mpaka 2035 na ikipendeza tutabadili katiba ili atawale mpaka atakaposema kachoka mwenyewe.
Kwamba atake asitake tutamlazimisha kuongeza muda wa kutawala au?
 
Biden kule USA kauwa mwanaharakati mmoja mjuaji kama hawa wanaotukana hovyo hapa Tanzania.

Madonna aliwahi kumtukana Trump mbele ya hadhara na wazee wa FBI wakamwambia afute kauli yake na akaifuta hadharani mambo yakaisha.

Wapo unaoweza kuwatukana lakini madaraka ya rais ni lazima yaheshimiwe.
Kwanza ieleweke wazi, siungi mkona tabia zisizo za kistaarabu za kumtukana mtu yeyote , sembuse kiongozi wa nchi.
Kutukana ni mihemuko, tabia ambazo zipo kwa binadamu na si za kistaarabu.
Kuna mwanasiasa mmoja vile vile aliwatukana wanasiasa wenziwe kuwa wanawashwa washwa.
Mwingine akawaita wanasiasa walio chini yake kwa dharau"Nonsense".
Hayo yoye ni kumpunguzia mtu hadhi yake katika jamii, lakini huo si uhaini!
 
..sasa kama Serikali / Ccm wamewaelimisha wananchi na wameeleweka kwanini wanatumia POLISI?

..Mara nyingi CCM hutumia POLISI pale inapokuwa imezidiwa kwa hoja na vyama vya upinzani.

..Mama alikosea kutanguliza WAHUNI kutetea huu mkataba, na sasa amepoteza imani na ushawishi ktk suala hili.
Tuwe na tabia ya kupenda kusikiliza, IGP Wambura ajasema wamekamatwa kwa sababu ya kupinga bandari japo washashindwa mahakamani na awataki kuheshimu maamuzi.

Na akaendelea kuelezea ata kama watu bado wanataka kupinga bandari wabaki kwenye mipaka ya hoja za siasa, unaposema utafanya njama nchi isitawalike kisa bandari hapo sasa unanunua ugomvi na polisi hiyo ndio kauli yake.
 
Kweli mama anaboronga na kwakifupi sijawahi ielewa ccm
Kwenye comment kuna izo comment za chawa wa mama🥲🥲
Safari ya kuliponya ili taifa bado ni ndefu sana
 
Nyamaza hujui kitu. Mama anafanya vizuri kabisa. Watanzania tunamuombea adumu mpaka 2035 na ikipendeza tutabadili katiba ili atawale mpaka atakaposema kachoka mwenyewe.
Kwa hili, huyu naye atapita njia ileile aliyopitia mtangulizi wake. Usishangae hata yeye akafa premature death tena yeye hata asifikishe mwaka 2025!!

Acha ndugu. Usichezee wala kukanyaga haki za watu. Usionee na kumwaga damu za watu bila makosa yoyote Kwa kiburi cha "mimi ni mtawala na mwenye mamlaka"

Yupo anayetawala juu mbinguni na hapa Duniani, Mungu wa haki. Ni mfalme wa wafalme. Mungu wa haki
 
Back
Top Bottom