Siyo siri Rais Samia alianza vizuri, sasa analikoroga



Kiti cha Ikulu kinawehusha
 
Watu wa CCM wamezunguka nchi nzima kuelezea upotoshaji

Serikali ime elezea

Wapingaji wameenda mahakamani wameshindwa.

Hapo sasa ni sawa na mtu anaeonyeshwa rangi nyeupe, yeye anakadhana anaona nyeusi; kuendelea kujibizana na mtu kama huyo ndio kukosa muda.

Bandari aina shida yoyote na awajakamatwa kwa sababu ya bandari; isipokuwa kauli zao.
 

..sasa kama Serikali / Ccm wamewaelimisha wananchi na wameeleweka kwanini wanatumia POLISI?

..Mara nyingi CCM hutumia POLISI pale inapokuwa imezidiwa kwa hoja na vyama vya upinzani.

..Mama alikosea kutanguliza WAHUNI kutetea huu mkataba, na sasa amepoteza imani na ushawishi ktk suala hili.
 
Sawa mwana CCM....ila kila kitu kina mwisho.
 
Upole wa kiongozi wa nchi una mipaka yake. Ana mwili wa nyama na uvumilivu wa binadamu huwa na kikomo chake.

Unapomtusi rais au unapokuja na habari ya upotoshaji wa wazi nafsi yako na iwe ya kwanza kukusuta kuwa unachokifanya ni cha hovyo.
 
Kwa huyu mamako ni uchumi upi anaotengeneza?
 
Nafikiri limemgusa kwa kuhusika by 100%.
 
Upole wa kiongozi wa nchi una mipaka yake. Ana mwili wa nyama na uvumilivu wa binadamu huwa na kikomo chake.

Unapomtusi rais au unapokuja na habari ya upotoshaji wa wazi nafsi yako na iwe ya kwanza kukusuta kuwa unachokifanya ni cha hovyo.
Ni mjinga tu anayeweza kuamini kuwa tusi ni uhaini.
Hata kusuka kitu inabidi uwe na akili!
 
Nyamaza hujui kitu. Mama anafanya vizuri kabisa. Watanzania tunamuombea adumu mpaka 2035 na ikipendeza tutabadili katiba ili atawale mpaka atakaposema kachoka mwenyewe.
 
Serikali imegundua imefanya kinyume cha sheria na ndiyo sababu imeamua kupeleka bungeni muswada wa amendment katika kikao kijacho ili kuhalalisha ufedhuli wao! Uliona wapi mkataba unasainiwa halafu Sheria ya kuhalalisha inafuata!

Kuhusu gharama za kesi Mwambukusi and co. walianza kwa fedha zao baadaye wananchi wakawaunga mkono kwa kuwachangia ingawa mahakama imeamua mlalamikiwa na mlalamika wajigharimie wenyewe!

Leo hii mawakili wenzake wa Mwambukusi wame- file request for appeal kwa gharama zao na wanaowaunga mkono. Kwa hiyo gharama za kesi siyo issue wananchi watagharimia.

Chadema haijawatenga na ndiyo sababu Mdude yupo nao bega kwa bega, ulitaka viongozi wote wa Chadema wahamie Mbeya?
 
Wanaolikoroga wamekaa pembeni wanasubiri alinywe limtokee puani
 
Ni mjinga tu anayeweza kuamini kuwa tusi ni uhaini.
Hata kusuka kitu inabidi uwe na akili!
Biden kule USA kauwa mwanaharakati mmoja mjuaji kama hawa wanaotukana hovyo hapa Tanzania.

Madonna aliwahi kumtukana Trump mbele ya hadhara na wazee wa FBI wakamwambia afute kauli yake na akaifuta hadharani mambo yakaisha.

Wapo unaoweza kuwatukana lakini madaraka ya rais ni lazima yaheshimiwe.
 
Kwa huyu mamako ni uchumi upi anaotengeneza?
Maelfu ya Ajira
Maelfu ya wawekezaji
Maelfu ya Kilimo chenye Tija
Maelfu ya miundombinu ya kila sekta
Maelfu ya wafanyabiashara
Mapato ya Serikali mara dufu

Kiufupi hakuna takataka yeyote wa kumzodi Samia kwenye Uchumi na social services
 
Nyamaza hujui kitu. Mama anafanya vizuri kabisa. Watanzania tunamuombea adumu mpaka 2035 na ikipendeza tutabadili katiba ili atawale mpaka atakaposema kachoka mwenyewe.
Kwamba atake asitake tutamlazimisha kuongeza muda wa kutawala au?
 
Kwanza ieleweke wazi, siungi mkona tabia zisizo za kistaarabu za kumtukana mtu yeyote , sembuse kiongozi wa nchi.
Kutukana ni mihemuko, tabia ambazo zipo kwa binadamu na si za kistaarabu.
Kuna mwanasiasa mmoja vile vile aliwatukana wanasiasa wenziwe kuwa wanawashwa washwa.
Mwingine akawaita wanasiasa walio chini yake kwa dharau"Nonsense".
Hayo yoye ni kumpunguzia mtu hadhi yake katika jamii, lakini huo si uhaini!
 
Tuwe na tabia ya kupenda kusikiliza, IGP Wambura ajasema wamekamatwa kwa sababu ya kupinga bandari japo washashindwa mahakamani na awataki kuheshimu maamuzi.

Na akaendelea kuelezea ata kama watu bado wanataka kupinga bandari wabaki kwenye mipaka ya hoja za siasa, unaposema utafanya njama nchi isitawalike kisa bandari hapo sasa unanunua ugomvi na polisi hiyo ndio kauli yake.
 
Kweli mama anaboronga na kwakifupi sijawahi ielewa ccm
Kwenye comment kuna izo comment za chawa wa mama🥲🥲
Safari ya kuliponya ili taifa bado ni ndefu sana
 
Nyamaza hujui kitu. Mama anafanya vizuri kabisa. Watanzania tunamuombea adumu mpaka 2035 na ikipendeza tutabadili katiba ili atawale mpaka atakaposema kachoka mwenyewe.
Kwa hili, huyu naye atapita njia ileile aliyopitia mtangulizi wake. Usishangae hata yeye akafa premature death tena yeye hata asifikishe mwaka 2025!!

Acha ndugu. Usichezee wala kukanyaga haki za watu. Usionee na kumwaga damu za watu bila makosa yoyote Kwa kiburi cha "mimi ni mtawala na mwenye mamlaka"

Yupo anayetawala juu mbinguni na hapa Duniani, Mungu wa haki. Ni mfalme wa wafalme. Mungu wa haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…