Vitu vingine fanya kama passion tu, havina impact yoyote kwa individual person.
Passion sio Impact au haina impact ?, Individually ukimaanisha nini yaani hata hao selected / waliocheza nao hawana faida / impact
Imagine tuseme Tanzania imefanikiwa kuingia WC na ikafika final na ikachukua kombe, wewe km wewe una nufaika vp na ushindi huo? Je inaweza kukuza uchumi wa nchi? Achana na uchumi wako tu.
Kweli hujui hili ?, Hivi unadhani bila Pele Brazil ingefahamika kama inavyofahamika, bila Brazil kucheza a Beautiful game watu wangeipenda na nchi kuweza kuuza bidhaa zao, unadhani FIFA kama FIFA inachangia kiasi gani cha pesa kwenye grassroots za nchi ? Hivi unajua kabla Senegal haijaifunga France kuna watu walikuwa hata hawajui Senegal ni nini ? Hivi unajua Vita vya kwanza vya Dunia vilisimama ili watu waangalie mpira ?
Unajua timu ikichukua Kombe la Dunia inalipwa kiasi gani na scouts wa nchi zote wataanza kuangalia hio nchi kiasi gani na wangapi watanunuliwa / kuchukuliwa sababu ya huo ushindi ? Unajua passion ya mpira itakua kiasi gani na mzunguko wa biashara kuongezeka kiasi gani ? Hivi nini kinakuza uchumi labda nikuulize ? (Watu kupenda ligi ya Bongo na Vibanda umiza kuongeza uchumi unakua au )?
Ukifuatilia sana soccer utagundua tunapigia debe kazi za watu pasipo kujijua.
Unapiga debe sababu ya passion (that is life) ukiangalia kwa jicho hilo kila kitu hakina maana..., hata unavyocheza mziki na kutoa jasho unapata faida gani ?, mimi kupoteza muda hapa kukujibu wewe napata faida gani..., nikinywa beer napata faida gani ? (ule utamu kwenye koo) ? kama ndivyo unajuaje mpiga kelele huo sio utamu wake ?
Wewe mwana simba, ubingwa mara nne mfulilizo ulikunufaishaje?
Si ni mwana Simba ? Sasa huoni mwana Simba yanga ingeshinda angepata huzuni ? and what is life kama sio happiness and feeling good ?
Je ubingwa wa yanga na hata wangekuwa unbeaten 100 games ww ingekuongezea nini?
Unamuongezea bragging rights..., to each his/her own...
Lakini utagundua inaposhinda simba/yanga kuna kundi flani la watu wanapata manufaa wewe utabaki mpiga kelele na kuchangia timu ya watu wa watu.
Manufaa ni nini ? Pesa ? Ingekuwa ni Pesa watu waliozaliwa kwenye Royal Family wangekuwa ni wenye manufaa peke yao ila utagundua kuna vitu ni priceless na simba / yanga au timu yoyote bila mashabiki ni uchafu tu..., na kwa taarifa yako hakuna owner wa timu ambaye ana-make direct money (labda kukuza brand) its a loss making business for owners
Kurudi kwenye mada hata anaeshabikia morroco hana tofauti na mtu wa mbeya anayeshabikia simba. Mpira utabaki kuwa burudani and it has nothing to do with uzalendo since ni biashara ya watu fulani.
Kila mtu anashabikia kulingana na utashi wake kuna mtu anashabikia timu ya mtaa sababu ni mtaani kwake, kuna mtu alishabikia Brazil (especially watu wa Africa) kutokana na Pele..., kuna watu wa Msumbiji wanashabikia Ureno sababu the Great Eusebio alitokea huko kuna watu hii ni burudani wanashabikia sababu kutokana na burudani inayotoka hapo....
That's why its football a beautiful game..., kwa ambaye hajui hili nadhani amepotea na atafute hobby nyingine... (maybe pottery au golf)