Sofiane Boufal: Ushindi wa Morocco ni kwa ajili ya wananchi wa Morocco, Waarabu na Waislamu

Ni kweli maana mashabiki wengi wa Afrika walisimama na timu za magharibi na Amerika ya kusini.
 
Waafrika gani unazungumzia!?..kwani waarab si waafrika!?..uafrika si rangi nyeusi ya ngozi
Hahahaha hawataki kusikia wanaitwa waafrica, inaonekana huwajui wewe, wanafikira wako more superior kuliko ngozi nyeusi, usilazimishe undugu hawataki
 
W We jamaa kichwa ni box kabisa wapi wameandika hii sio kwa waAfrica? Acha ushamba
 
Hivi kama kuna Saido, Dodo na Saidama....!

Hafu mimi nakuja na Pilau na kusema hii Pilau italiwa na Saido na Dodo....! Unahitaji uthibitisho gani kujua kwamba haumo!

Otherwise labda wewe Ostaadh.
Inategemea na jamaa alikua anaongea vipi na namna alivyo ulizwa. Shida ni kua watu mpo tayari kukumbatia habari ya uongo kisa tu inaendana na mnachowaza
 
Akitaja wanaohusika na ushindi amenukuliwa hivi:-
" This victory belongs to all the Moroccan people, to all the Arab peoples, to all the Muslim peoples of the world"
Lete sauti yake
 
Kataja wahusika watatu, Waafrika hatuhusiki
 
Shangwe zote zile nimewashangilia jana kumbe wamejitoa kwenye uafrica eboo😀
Furaha halisi unajitengenezea mwenyewe. Furaha za kutengenezewa zinaweza kukugeuka muda wowote. Ona furaha yako ya jana ilisababishwa na Waburushi, leo wamekuruka kwamba wewe sio sehemu ya ushindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…