Sometimes Huhitaji Ushauri Wala Pesa… Unahitaji Tu Mtu Mmoja Akukumbatie na Kukuambia: Everything Will Be Okay

Sometimes Huhitaji Ushauri Wala Pesa… Unahitaji Tu Mtu Mmoja Akukumbatie na Kukuambia: Everything Will Be Okay

Pole sana mama pretty wangu, mambo ya kifamilia yanazingua sana..!! Haswa hizi familia zetu za kibongo..

Jipe moyo utashinda, usifikirie kujiua. Tumekuja duniani kupambana, ndiomana mimi sitaki kuzaa naona nitaleta mtu aje kuteseka kwa starehe zangu binafsi..!!
 
Ndugu pole kwa unayopitia japo sijui tatizo ni nini ila machungu yoyote yale hasa yanayougusa moyo huwa yanaumiza sana. Cha kufanya usikatae tamaa wala muombe Mungu kwa imani yako kisha mshirikishe mtu ambaye ambaye unahakika ndiyo anayeweza kuwa faraja yako hapo haijalishi ni mzazi, mke au rafiki ukiwa unaamini huyu ndiye amekuwa akinipa faraja basi mshirikishe mnaweza gawana maumivu kisha akakushauri vyema.

Ni wengi tumeumizwa sana makazini, kwenye mapenzi na ndugu au watu wa karibu lakini tulivumilia tukatafakari, kuikubali hali na kuchukua uamuzi upya na sasa tunashonga mbele.
 
Pole sana Mama Pretty, kuna wakati shida za familia au changamoto za dunia zinatuelemea mpaka tunajiona hatuna thamani ya kuishi tena. Nataka ujue kwamba hisia zako ni valid kabisa, na ni sawa kabisa kulia na kuishiwa nguvu wakati mwingine.

Hata hivyo, naomba usiruhusu hayo mawazo ya kukata tamaa yashinde hii vita, wewe ni mtu wa thamani sana, na kuna watu wengi wanaokupenda na wanaohitaji uwepo wako hapa duniani, shusha presha yako sasa hivi, usijihukumu kwa unavyojisikia, na uweke akilini kwamba you are stronger than you think. Hii hali ngumu unayopitia ni ya mpito tu na itapita, nina uhakika utakuwa sawa kabisa, please don't lose hope kabisa.
Pole sana Mama pretty kila kitu kitakuwa sawa, muombe na umtegemee Mungu pekee ndie mweza wa kila kitu
 
Dada, najua kuna maumivu ambayo hakuna mtu anaweza kuyabeba kwa niaba yako. Lakini usikubali nyakati ngumu za muda mfupi zikufanye uharibu maisha yako yote. Pambana hata kama ni kwa hatua ndogo, lia, pumzika, na tafuta msaada unapohitaji lakini usikate tamaa. Umefika hapo ukiwa na sababu ya kuishi, hata kama bado hujaiona.
 
Moja ya mtihani wa dunia hii ni kushinda nguvu ya kukata tamaa.

Usikate tamaa Mama pretty . Nyakati ngumu huja na kupotea ila watu wenye moyo ya kuvumilia hudumu. Baadaye itakuwa historia tu na utatabasamu ukikumbuka namna ulivyovuka kwenye nyakati ngumu bila kukata tamaa.
 
Kuna wakati maisha yanakupeleka sehemu mpaka unatamani usingezaliwa kwenye hiyo familia uliyopo.

Au unajikuta unajuta kuishi, imefikia hatua mpaka mtu unatamani kujiua tu ili uepukane na madhila ya dunia.

Naandika hii thread huku nikiwa natetemeka na kukata tamaa. Natamani mtu aniambie tu nitakuwa sawa. Najiskia vibaya sana na nina uchungu mkubwa sana ndani yangu.🙏
Usisubiri mtu akuambie utakua sawa...

Jiambie mwenyewe kuwa nitakua sawa, hata ukiwa peke Yako fungua mdomo na tamka kuwa nitakua sawa, unapopitia Magumu usikubari kuvunjika Moyo, hata kama ni maumivu makubwa kiasi Gani, tamka kwamba changamoto yoyote inayonitokea, inatokea Kwa sababu ninaweza kupambana nayo, then tamkaaaa "Nitakua sawa"

Unaweza kuwa hujui kuhusu mambo ya Kiroho, ila unapotamka jambo Kwa Sauti, Ulimwengu wa Roho unasikia na itakua sawa na vile unavyotamka.

Unapokata tamaa ama kutamka maneno ya kukata tamaa, Ile spiritual negative energy haiishii hapo, inazidi ku push, that's why, inaanza kidogo kidogo, utasema Maisha ni Magumu, moyo wangu umeumizwa, na wewe ukikubari, itaenda mbele zaidi, baadaye utaanza kuwaza ama kusema, siwezi kuendelea namna hii, this is too much, nawe ukakubari ndani Yako itaendelea Tena kukusukuma, itafikia siku ukienda Msibani, ukaona Marehemu ndani ya Jeneza, unaanza kumuonea Wivu....!

Mkuu usikubari, utakufa kweli, tutakula Ubwabwa na tutakusahau.... Ukisikia ndani mawazo negative usikubari, panua mdomo, tamka Positive, ukiona mawazo ya kujua yanakuja, funua mdomo, tamka kwamba Sitakufa bali nitaishi....! Ukiona kukata tamaa na Maisha na unaweza kwamba utakufa Masikini, Usikubari Mkuu, tamka Kwa Sauti kwamba Mimi sio Masikini....!

Mungu akubariki Mtu wa Mungu.
 
fake id zikukumbatie, aya sawa pokea kumbato langu everything will be okay

Dah nilisahau umesema mmoja.

Anyway i feel you, kuna kipindi maisha yanakuwa magumu sana, kwa upande wangu najiambiaga mwakani mwezi fulani nitakuwa naliona hili gumu la muda huu kama historia
 
Kuna wakati maisha yanakupeleka sehemu mpaka unatamani usingezaliwa kwenye hiyo familia uliyopo.

Au unajikuta unajuta kuishi, imefikia hatua mpaka mtu unatamani kujiua tu ili uepukane na madhila ya dunia.

Naandika hii thread huku nikiwa natetemeka na kukata tamaa. Natamani mtu aniambie tu nitakuwa sawa. Najiskia vibaya sana na nina uchungu mkubwa sana ndani yangu.🙏
Baada ya kukumbatiwa utataka pesa
 
Back
Top Bottom