Akiulizwa atupe mrejesho anauchunaTangu uingie mitini wakati unataka kuyashitaki makampuni ya simu ulionekana hovyo kweli nimeshangaa kuona umerudi au kuna chochote ulipewa ukasaliti umma?
Kwa Sheria za Tanzania, ni jukumu la mwanaume kumtunza mke wake hicho kifungu kipo kwenye Sheria ya Ndoa,
Na pia kipo kifungu Cha sheria kinachosema mume anaweza kumtunza mke na watoto walioachana.
- Sasa kama hujui Kuna mazingira ambayo mahakama inaweza ikatoa amri ya matunzo kipindi Cha Kesi ya ndoa,hadi baada ya kuvunjika ndoa i.e talaka,
- hivi unajua Kuna mazingira ambayo pia Mwanamke anaweza kumtunza mme wake?
...Naona Wanaume wamelishikia Bango Kumpongeza Mwanaume Mwenzetu bila Kufikiri!SOMO LA MALI KWA WANANDOA KWA KILICHOTOKEA KWA ACHRAF HAKIMI NA MKEWE.
Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.
Mke wa ACHRAF HAKIMI ameshindwa kupewa mali yoyote baada ya ndoa yao kuvunjika kwasababu Hakimi aliziandika mali zote jina la mama yake mzazi.
Je jambo hili linawezekana kwa Sheria za Tanzania ?.
Ndio linawezekana , ni hivi :-
Kwa wanandoa kuna mali za aina 2;-
1. Mali zilizopatikana kabla ya ndoa.
2. Mali zilizopatikana wakati wa ndoa.
MALI ZILIZOPATIKANA KABLA YA NDOA.
Hizi ni mali ambazo mtu anakuwa nazo kabla hajaoa ama kuolewa. Yumkini akiingia kwenye ndoa anaingia nazo.
Hata hivyo Sheria ya ndoa inasema mali hizi zinahesabika si za ndoa kwa maana ya kuwa huyo mwenye nazo ni zake peke yake bila mwenza wake. Ndoa ikivunjika haziwezi kugawiwa.
Pamoja na hayo, mali hizo pia zinaweza kubadilika na kuwa za ndoa ikiwa mambo mawili yatafanyika.
KWANZA, ikiwa mwenza mwenye hizo mali ataingia makubaliano na mwenza wake kuwa ziwe za ndoa basi zitakuwa za ndoa na itakapovunjika basi zitagawiwa
PILI, iwapo mali umeingia nayo kwenye ndoa lakini kipindi cha ndoa imeendelezwa.
Mfano, Umeingia kwenye ndoa na kiwanja chako lakini kipindi cha ndoa ndo kimejengwa, AU kilikuwa kimejengwa lakini ni pagala tu, kipindi cha ndoa ndo mmemalizia na kuwa nyumba kamili.
Hapa ndoa ikivunjika mtagawana na hautasema alinikuta na Pagala langu au kiwanja changu. Kitendo cha kuendeleza mkiwa wote kinampa haki mwingine na kuwa mali ya wote.
Lakini kama mali ameingia nayo kwenye ndoa na hakuna maendelezo yoyote yaliyofanyika kipindi cha ndoa basi hiyo mali haiwezi kugawiwa ndoa ikivunjika na inabaki mali ya mwenza huyo pekee.
MALI ZILIZOPATIKANA WAKATI WA NDOA.
Hizi huhesabika moja kwa moja kuwa ni za wanandoa wote mpaka isemwe vinginevyo.
Na haijalishi zipo kwenye jina la mke au mme, madhali zilipatikana kipindi cha ndoa basi zinahesabika ni za wanandoa na zinastahili kugawiwa ndoa inapovunjika.
Hata hivyo, ili ziweze kugawiwa ni lazima kila mwanandoa athibitishe mchango wake katika upatikanaji wa hizo mali.
Tafsiri ya mchango ni pamoja na pesa, vifaa, lakini hata kazi za nyumban nao ni mchango katika kupatikana kwa mali.
Mke au mme anayebaki nyumbani kwa ajili ya shughuli za nyumbani anahesabika amechangia kwa kile kinachopatikana kutoka kwa yule aliyeingia mtaani kutafuta.
Kwahiyo wakati wa kuthibitisha mchango hayo yote yanazingatiwa.
JE MGAWANYO WA MALI NI NUSU KWA NUSU.
Hapana, mgawanyo mali za ndoa inapovunjika sio lazima kuwa nusu kwa nusu. Inaweza kuwa 20%/80%, 70%/30%, 90%/10%, nk nk. Kwa ufupi hakuna kiwango maalum, hata kukosa kabisa kupo.
Kikubwa ni kuwa utapata fungu lako kutokana kiwango cha mchango wako kama tulivyoona hapo juu. Na kama huna mchango kabisa basi waweza kutoka kapa pia.
MALI AMBAZO ZIKO KWENYE MAJINA YA WATOTO.
Mali hizi hamuwezi kuzigawa ndoa inapovunjika. Hii ni kwasababu kitendo cha kuandika majina ya watoto ni sawa na kuwa mlikubaliana kuwapa zawadi watoto.
Ukitoa zawadi maana yake maslahi(ownership interest) yenu katika hiyo mali yalishahama kwenda kwa watoto kwa njia ya zawadi nanyi hamna maslahi tena katika hiyo mali.
MALI ZILIZOANDIKWA MAJINA YA WATU WENGINE.
Mali ambayo haina jina la mke au mme sio rahisi kuigawa ndoa inapovunjika.
Huyu HACHRAF HAKIMI aliandika majina ya mama yake. Mali ya namna hii ni vigumu kuigawa kama mali ya ndoa kwasababu inaonekana inamilikiwa na mtu mwingine.
Kwa msingi huu huwezi kugawa mali ambayo haihusiki. Wengine huandika majina ya ndugu zao, marafiki nk.
Ndio, akifanya hivi basi ni vigumu hiyo mali kuigawa ndoa ikivunjika hata kama una uhakika wa 100% kuwa ni yenu.
Hii ni kwasababu ushahidi wa nani mmiliki wa mali ni nyaraka au usajili. Nyaraka na usajili unaonesha mtu mwingine ni vigumu useme hii mali ni yetu.
MALI INAYOBADILISHWA UMILIKI.
Kama mali imeanza ikiwa ni ya ndoa halaf ikabadilishwa majina hiyo unaweza kuidai na ikagawiwa.
Wapo wanandoa wakiona mambo yameanza kubadilika basi ama huanza kubadili majina ya mali au huuza.
Ikiwa tarehe zitaonesha mali ilibadilishwa au kuuzwa kipindi cha ndoa na ni mali ya wanandoa,na mwenza hakuwa ameridhia, basi ubadilishwaji huo ama uuzaji huo ni batili na hiyo mali itarudishwa kwenye mali za wanandoa ili igawiwe.
WANANDOA WANAWEZA KUFANYA NINI KUHUSU MALI.
KWANZA, yafaa ikiwa mtakubaliana basi mali iwe na majina ya wote mke na mme. Iwe ni gari, kiwanja, nyumba,akaunti benki, nk. Sheria inaruhusu.
Hii husaidia sana hata kipindi cha kifo ambapo mjane au mgane hawezi kusumbuliwa.
PILI, mnaweza kuwa na makubaliano kuhusu kila mali,kuanzia zile ambazo mlikuwa nazo kabla hamjaoana, mpaka zile mtakazopata wakati wa ndoa. Mtakubaliana ipi iwe ya pamoja na ipi iwe ya mmoja.
Japo hili ni gumu kwa maisha yetu sababu ukilianzisha hili utaambiwa HUNA MAPENZI YA KWELI.
TATU, muwe na utaratibu wa kucheki mara kwa mara hadhi(status ) ya mali. Pitia pitia huko Ardhi, TRA, Serikali ya mtaa ujue. Msilale sana.
Huenda ukagundua kitu mapema kabla mambo hayajaharibika.
NNE, msajili/andika mali kwa majina ya watoto, maana yake muwape zawadi watoto. Hata kama mnatumia nyie lakini ikijulikana ni za watoto.
Ila lazima iwe imesajiliwa na sio kusema tu kwa mdomo kuwa hizi ni mali ni za watoto.
Ukisema mali ni za watoto na hakuna usajili rasmi hiyo hukataliwa sababu watoto hawana mali bali mali ni za wazazi na majina zitakuwa zinasoma wazazi.
TANO, kama hamuwezi kufanya lolote mapema kati ya hayo manne juu basi mmoja awe tayari kupoteza au msubiri mahakama iwaamue.
REJEA ya maandiko haya ni :-
Sheria ya ndoa R:E 2019 hasa vifungu vya 58,59,,60, na114.
NA
Shauri la Bi Hawa Mohammed vs Ally Sefu(Rufaa Na.9/1983) TZCA 12.
...Naona Wanaume wamelishikia Bango Kumpongeza Mwanaume Mwenzetu bila Kufikiri!
Kitakachotokea Sasa... Jamaa Bado Ataktakiwa kutoa matunzo Kwa ajili Mtoto/Watoto wake, atajua Mwenyewe wapi atakozitoa Mwenyewe! SI anacheza mpira na analipwa Hela nzuri TU?
Tusubiri tuone Hakimu atampangia atoe Shilingi ngapi za matunzo...ama aende Jela!
Tusubiri pia Mke wake apate Wakili Mzuri wakati Dunia' nzima inajua Hela zake Hakimu 'amezificha' Kwa kumpa Mama yake!
Tungoje tuone SHERIA za huko kuhusu Watoto zinavyofanya Kazi....Sio SHERIA za Wizara yetu ya Ustawi wa Jamii ! [emoji1][emoji1]
....Kweli ! Kama Kahaba Mwenyewe ni yule niliemuona kwenye Picha wako pamoja na Hakimu, na Kiuno Chore Kiko Nje !...kweli Bora ametolewaKapa ! [emoji1][emoji1][emoji1]Huyu jamaa alie kuandikisha mama yake ni dume la mbegu ikitokea akafa mamake alithi mali na ndugu zake bora kuliko mali yake kuliwa na huyo kahaba angeishia kuhonga tu
Mahakama za kitanzania zimekulemaza,hayo maswali ni mepesi sana na sidhani hata kama kwenye situation kama hiyo ya jamaa yalipaswa kuulizwa.
- Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
- Hapo Hakimi ametumia false pretense.
Vipi kuhusu pesa za wanandoa zilizopo akaunti za wanandoa kwa majina yao binafsi nazo zinatakiwa zigawanywe?SOMO LA MALI KWA WANANDOA KWA KILICHOTOKEA KWA ACHRAF HAKIMI NA MKEWE.
Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.
Mke wa ACHRAF HAKIMI ameshindwa kupewa mali yoyote baada ya ndoa yao kuvunjika kwasababu Hakimi aliziandika mali zote jina la mama yake mzazi.
Je jambo hili linawezekana kwa Sheria za Tanzania ?.
Ndio linawezekana , ni hivi :-
Kwa wanandoa kuna mali za aina 2;-
1. Mali zilizopatikana kabla ya ndoa.
2. Mali zilizopatikana wakati wa ndoa.
MALI ZILIZOPATIKANA KABLA YA NDOA.
Hizi ni mali ambazo mtu anakuwa nazo kabla hajaoa ama kuolewa. Yumkini akiingia kwenye ndoa anaingia nazo.
Hata hivyo Sheria ya ndoa inasema mali hizi zinahesabika si za ndoa kwa maana ya kuwa huyo mwenye nazo ni zake peke yake bila mwenza wake. Ndoa ikivunjika haziwezi kugawiwa.
Pamoja na hayo, mali hizo pia zinaweza kubadilika na kuwa za ndoa ikiwa mambo mawili yatafanyika.
KWANZA, ikiwa mwenza mwenye hizo mali ataingia makubaliano na mwenza wake kuwa ziwe za ndoa basi zitakuwa za ndoa na itakapovunjika basi zitagawiwa
PILI, iwapo mali umeingia nayo kwenye ndoa lakini kipindi cha ndoa imeendelezwa.
Mfano, Umeingia kwenye ndoa na kiwanja chako lakini kipindi cha ndoa ndo kimejengwa, AU kilikuwa kimejengwa lakini ni pagala tu, kipindi cha ndoa ndo mmemalizia na kuwa nyumba kamili.
Hapa ndoa ikivunjika mtagawana na hautasema alinikuta na Pagala langu au kiwanja changu. Kitendo cha kuendeleza mkiwa wote kinampa haki mwingine na kuwa mali ya wote.
Lakini kama mali ameingia nayo kwenye ndoa na hakuna maendelezo yoyote yaliyofanyika kipindi cha ndoa basi hiyo mali haiwezi kugawiwa ndoa ikivunjika na inabaki mali ya mwenza huyo pekee.
MALI ZILIZOPATIKANA WAKATI WA NDOA.
Hizi huhesabika moja kwa moja kuwa ni za wanandoa wote mpaka isemwe vinginevyo.
Na haijalishi zipo kwenye jina la mke au mme, madhali zilipatikana kipindi cha ndoa basi zinahesabika ni za wanandoa na zinastahili kugawiwa ndoa inapovunjika.
Hata hivyo, ili ziweze kugawiwa ni lazima kila mwanandoa athibitishe mchango wake katika upatikanaji wa hizo mali.
Tafsiri ya mchango ni pamoja na pesa, vifaa, lakini hata kazi za nyumban nao ni mchango katika kupatikana kwa mali.
Mke au mme anayebaki nyumbani kwa ajili ya shughuli za nyumbani anahesabika amechangia kwa kile kinachopatikana kutoka kwa yule aliyeingia mtaani kutafuta.
Kwahiyo wakati wa kuthibitisha mchango hayo yote yanazingatiwa.
JE MGAWANYO WA MALI NI NUSU KWA NUSU.
Hapana, mgawanyo mali za ndoa inapovunjika sio lazima kuwa nusu kwa nusu. Inaweza kuwa 20%/80%, 70%/30%, 90%/10%, nk nk. Kwa ufupi hakuna kiwango maalum, hata kukosa kabisa kupo.
Kikubwa ni kuwa utapata fungu lako kutokana kiwango cha mchango wako kama tulivyoona hapo juu. Na kama huna mchango kabisa basi waweza kutoka kapa pia.
MALI AMBAZO ZIKO KWENYE MAJINA YA WATOTO.
Mali hizi hamuwezi kuzigawa ndoa inapovunjika. Hii ni kwasababu kitendo cha kuandika majina ya watoto ni sawa na kuwa mlikubaliana kuwapa zawadi watoto.
Ukitoa zawadi maana yake maslahi(ownership interest) yenu katika hiyo mali yalishahama kwenda kwa watoto kwa njia ya zawadi nanyi hamna maslahi tena katika hiyo mali.
MALI ZILIZOANDIKWA MAJINA YA WATU WENGINE.
Mali ambayo haina jina la mke au mme sio rahisi kuigawa ndoa inapovunjika.
Huyu HACHRAF HAKIMI aliandika majina ya mama yake. Mali ya namna hii ni vigumu kuigawa kama mali ya ndoa kwasababu inaonekana inamilikiwa na mtu mwingine.
Kwa msingi huu huwezi kugawa mali ambayo haihusiki. Wengine huandika majina ya ndugu zao, marafiki nk.
Ndio, akifanya hivi basi ni vigumu hiyo mali kuigawa ndoa ikivunjika hata kama una uhakika wa 100% kuwa ni yenu.
Hii ni kwasababu ushahidi wa nani mmiliki wa mali ni nyaraka au usajili. Nyaraka na usajili unaonesha mtu mwingine ni vigumu useme hii mali ni yetu.
MALI INAYOBADILISHWA UMILIKI.
Kama mali imeanza ikiwa ni ya ndoa halaf ikabadilishwa majina hiyo unaweza kuidai na ikagawiwa.
Wapo wanandoa wakiona mambo yameanza kubadilika basi ama huanza kubadili majina ya mali au huuza.
Ikiwa tarehe zitaonesha mali ilibadilishwa au kuuzwa kipindi cha ndoa na ni mali ya wanandoa,na mwenza hakuwa ameridhia, basi ubadilishwaji huo ama uuzaji huo ni batili na hiyo mali itarudishwa kwenye mali za wanandoa ili igawiwe.
WANANDOA WANAWEZA KUFANYA NINI KUHUSU MALI.
KWANZA, yafaa ikiwa mtakubaliana basi mali iwe na majina ya wote mke na mme. Iwe ni gari, kiwanja, nyumba,akaunti benki, nk. Sheria inaruhusu.
Hii husaidia sana hata kipindi cha kifo ambapo mjane au mgane hawezi kusumbuliwa.
PILI, mnaweza kuwa na makubaliano kuhusu kila mali,kuanzia zile ambazo mlikuwa nazo kabla hamjaoana, mpaka zile mtakazopata wakati wa ndoa. Mtakubaliana ipi iwe ya pamoja na ipi iwe ya mmoja.
Japo hili ni gumu kwa maisha yetu sababu ukilianzisha hili utaambiwa HUNA MAPENZI YA KWELI.
TATU, muwe na utaratibu wa kucheki mara kwa mara hadhi(status ) ya mali. Pitia pitia huko Ardhi, TRA, Serikali ya mtaa ujue. Msilale sana.
Huenda ukagundua kitu mapema kabla mambo hayajaharibika.
NNE, msajili/andika mali kwa majina ya watoto, maana yake muwape zawadi watoto. Hata kama mnatumia nyie lakini ikijulikana ni za watoto.
Ila lazima iwe imesajiliwa na sio kusema tu kwa mdomo kuwa hizi ni mali ni za watoto.
Ukisema mali ni za watoto na hakuna usajili rasmi hiyo hukataliwa sababu watoto hawana mali bali mali ni za wazazi na majina zitakuwa zinasoma wazazi.
TANO, kama hamuwezi kufanya lolote mapema kati ya hayo manne juu basi mmoja awe tayari kupoteza au msubiri mahakama iwaamue.
REJEA ya maandiko haya ni :-
Sheria ya ndoa R:E 2019 hasa vifungu vya 58,59,,60, na114.
NA
Shauri la Bi Hawa Mohammed vs Ally Sefu(Rufaa Na.9/1983) TZCA 12.
...Naona Wanaume wamelishikia Bango Kumpongeza Mwanaume Mwenzetu bila Kufikiri!
Kitakachotokea Sasa... Jamaa Bado Ataktakiwa kutoa matunzo Kwa ajili Mtoto/Watoto wake, atajua Mwenyewe wapi atakozitoa Mwenyewe! SI anacheza mpira na analipwa Hela nzuri TU?
Tusubiri tuone Hakimu atampangia atoe Shilingi ngapi za matunzo...ama aende Jela!
Tusubiri pia Mke wake apate Wakili Mzuri wakati Dunia' nzima inajua Hela zake Hakimu 'amezificha' Kwa kumpa Mama yake!
Tungoje tuone SHERIA za huko kuhusu Watoto zinavyofanya Kazi....Sio SHERIA za Wizara yetu ya Ustawi wa Jamii ! [emoji1][emoji1]
Kasome Sheria ya ndoa.Mwenzako anazungumzia watu walioachans, wewe unazungumzia waliopo kwenye Ndoa.
Unafanya Makusudi au haujamuelewa?
Kasome Sheria ya ndoa.
Kasome Sheria ya ndoa.
Wewe ndio hujui sheria ya ndoa, sheria ya ndoa imesema kuwa mahakama ' inaweza ' kutoa amri ya matunzo Kwa mke au kwa mke wa zamani, Wakati wa kesi ya ndoa na baada ya kutolewa talaka hiyo, hiyo Sheria ya Ndoa imesema kuwa mahakama inaweza kutoa amri ya matunzo, sio Lazima yani inaweza kutoa au isitoe amri ya matunzo kwa mke au mke wa zamani, kasome kifungu Cha 115 Cha sheria ya NdoaAu hujui maana ya Ndoa, na pia hujui maana ya Talaka.
Ukishampa talaka hakuna hayo mambo ya kuhudumiana, ishu inayobaki ni Watoto.
Huduma yoyote italenga Watoto na sio mzazi anayewatunza hao Watoto(iwe Baba au Mama)
Power of court to order maintenance for spouse (1) The court may order a man to pay maintenance to his wife or former wife– (a) (b) (c) (d) (e) (f) (g)Hakuna sheria yoyote Duniani ya Aina Hiyo.
Kama Ipo hata nchi yoyote iweke hapa.
Anayehudumiwa ni MKE wa Ndoa, mkishaachana hakuna kitu kama hicho,
Wewe ndio hujui sheria ya ndoa, sheria ya ndoa imesema kuwa mahakama ' inaweza ' kutoa amri ya matunzo Kwa mke au kwa mke wa zamani, Wakati wa kesi ya ndoa na baada ya kutolewa talaka hiyo, hiyo Sheria ya Ndoa imesema kuwa mahakama inaweza kutoa amri ya matunzo, sio Lazima yani inaweza kutoa au isitoe amri ya matunzo kwa mke au mke wa zamani, kasome kifungu Cha 115 Cha sheria ya Ndoa
-unajua maana ya neno Mali za Wana ndoa?Mahakama za kitanzania zimekulemaza,hayo maswali ni mepesi sana na sidhani hata kama kwenye situation kama hiyo ya jamaa yalipaswa kuulizwa.
Ndiyo alikuwa anatumia zote kwani kuna siku watoto au huyo mtalaka wake waliwahi kulia njaa kwamba jamaa hawahudumii?source hasa ya kuvunjika hiyo ndoa je kulikuwa na lalamiko lolote la matunzo?kama hapana then hizo pesa alizoonekana hana ndiyo alikuwa anazitumia kwa njia hiyo.
La mama yake kuwa na ukwasi kama alivyoeleza mwanasheria hapo juu nadhani mahakama haina uwezo wa kuhoji as long as wao wanasubiri mamlaka za kichunguzi zilete mashtaka kwao kwamba wamemchunguza mama Achraf wakamkuta anauza cocaine etc ndo wata-deal nae na hata akisema mwanae ameamua kumpa zawadi kila alicho nacho kwa sababu alimzaa hakuna wa kumuuliza maana huyo mwanae hajamuibia mtu wala haijawahi kuthibitika kwamba kuna siku huyo mama alimshikia mwanae bunduki akimshinikiza amwandikishie mali zake.
Sasa sheria ya Ndoa imetumia maneno former wifeHakuna kitu kinachoitwa MKE wa zamani, embu inukuu hiyo sheria hapa, Acha habari za vijiweni.
Hata Lugha yenyewe inakataa, hakuna kitu kinaitwa MKE au Mume wa zamani kisheria.
Embu weka hiyo sheria, ugumu uko wapi?
MKE au Mume ni pale mnapokuwa ndani ya Ndoa, nje ya Ndoa atajulikana kama Baba au Mama, au Mwanaume au Mwanamke.
Sheria inatambua MKE wa Kwanza, wapili, watatu au wake wengi. Lakini haitambui MKE wa zamani.
Umesoma sheria Kwa kukariri Mkuu
Power of court to order maintenance for spouse (1) The court may order a man to pay maintenance to his wife or former wife– (a) (b) (c) (d) (e) (f) (g)
-during the course of any matrimonial proceedings;
- if he has refused or neglected to provide for her as required by section 63;
- if he has deserted her, for so long as the desertion continues;
-when granting or subsequent to the grant of a decree of separation; -when granting or sebsequent to the grant of a decree of divorce
Sasa sheria ya Ndoa imetumia maneno former wife