Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Awapige pesa, kuwa na adabu huyo ni Wakili, na kazi ya uwakili ni kazi yenye heshima kabisa, na ndio maana Uwakili unapewa/ unaapishwa na Jaji Mkuu, kama Rais anavyoapishwa na Jaji Mkuu
Ni nani asiyejua hilo sasa?! Usipende kukurupuka kujitia smart kwa kila mtu usiyemjua na unayemjua. Lengo ni nini kuweka namba hapo?! Najua watakaomtafuta wengi ni wanawake, na tunakoelekea ni "tuma kiasi kadhaa humu kwenye namba hii nikusaidie...."

Wakili anatoaga mawasiliano yake kirahisirahisi?! 😃
 
Wote mnaoshabikia UBINAFSI NA UPUMBAVU WA HAKIMI NI BROKE NIGGAS! TAFUTENI PESA WAPUMBAVU NYIE
 
Ni nani asiyejua hilo sasa?! Usipende kukurupuka kujitia smart kwa kila mtu usiyemjua na unayemjua. Lengo ni nini kuweka namba hapo?! Najua watakaomtafuta wengi ni wanawake, na tunakoelekea ni "tuma kiasi kadhaa humu kwenye namba hii nikusaidie...."

Wakili anatoaga mawasiliano yake kirahisirahisi?! 😃
- uwe na heshima, ulikuwa unajua kuwa uwakili ni taaluma ya heshima? Huwezi kutumia Lugha za hovyo hovyo humu, ungekuwa unajua uwakili unaapishwa na Jaji Mkuu usingeandika huo Utopolo,hata sisi Wahasibu tunawaheshimu sana,
-huyo WAKILI Bashir, ni Mtu Mwenye heshima zake, usifikiri Kila Mtu ni tapeli kama wewe,
- kwani Wakili kutoa number zake za simu ni kosa?
 
SOMO LA MALI KWA WANANDOA KWA KILICHOTOKEA KWA ACHRAF HAKIMI NA MKEWE.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.

Mke wa ACHRAF HAKIMI ameshindwa kupewa mali yoyote baada ya ndoa yao kuvunjika kwasababu Hakimi aliziandika mali zote jina la mama yake mzazi.

Je jambo hili linawezekana kwa Sheria za Tanzania ?.

Ndio linawezekana , ni hivi :-

Kwa wanandoa kuna mali za aina 2;-

1. Mali zilizopatikana kabla ya ndoa.
2. Mali zilizopatikana wakati wa ndoa.

MALI ZILIZOPATIKANA KABLA YA NDOA.

Hizi ni mali ambazo mtu anakuwa nazo kabla hajaoa ama kuolewa. Yumkini akiingia kwenye ndoa anaingia nazo.

Hata hivyo Sheria ya ndoa inasema mali hizi zinahesabika si za ndoa kwa maana ya kuwa huyo mwenye nazo ni zake peke yake bila mwenza wake. Ndoa ikivunjika haziwezi kugawiwa.

Pamoja na hayo, mali hizo pia zinaweza kubadilika na kuwa za ndoa ikiwa mambo mawili yatafanyika.

KWANZA, ikiwa mwenza mwenye hizo mali ataingia makubaliano na mwenza wake kuwa ziwe za ndoa basi zitakuwa za ndoa na itakapovunjika basi zitagawiwa

PILI, iwapo mali umeingia nayo kwenye ndoa lakini kipindi cha ndoa imeendelezwa.

Mfano, Umeingia kwenye ndoa na kiwanja chako lakini kipindi cha ndoa ndo kimejengwa, AU kilikuwa kimejengwa lakini ni pagala tu, kipindi cha ndoa ndo mmemalizia na kuwa nyumba kamili.

Hapa ndoa ikivunjika mtagawana na hautasema alinikuta na Pagala langu au kiwanja changu. Kitendo cha kuendeleza mkiwa wote kinampa haki mwingine na kuwa mali ya wote.

Lakini kama mali ameingia nayo kwenye ndoa na hakuna maendelezo yoyote yaliyofanyika kipindi cha ndoa basi hiyo mali haiwezi kugawiwa ndoa ikivunjika na inabaki mali ya mwenza huyo pekee.

MALI ZILIZOPATIKANA WAKATI WA NDOA.

Hizi huhesabika moja kwa moja kuwa ni za wanandoa wote mpaka isemwe vinginevyo.

Na haijalishi zipo kwenye jina la mke au mme, madhali zilipatikana kipindi cha ndoa basi zinahesabika ni za wanandoa na zinastahili kugawiwa ndoa inapovunjika.

Hata hivyo, ili ziweze kugawiwa ni lazima kila mwanandoa athibitishe mchango wake katika upatikanaji wa hizo mali.

Tafsiri ya mchango ni pamoja na pesa, vifaa, lakini hata kazi za nyumban nao ni mchango katika kupatikana kwa mali.

Mke au mme anayebaki nyumbani kwa ajili ya shughuli za nyumbani anahesabika amechangia kwa kile kinachopatikana kutoka kwa yule aliyeingia mtaani kutafuta.

Kwahiyo wakati wa kuthibitisha mchango hayo yote yanazingatiwa.

JE MGAWANYO WA MALI NI NUSU KWA NUSU.

Hapana, mgawanyo mali za ndoa inapovunjika sio lazima kuwa nusu kwa nusu. Inaweza kuwa 20%/80%, 70%/30%, 90%/10%, nk nk. Kwa ufupi hakuna kiwango maalum, hata kukosa kabisa kupo.

Kikubwa ni kuwa utapata fungu lako kutokana kiwango cha mchango wako kama tulivyoona hapo juu. Na kama huna mchango kabisa basi waweza kutoka kapa pia.

MALI AMBAZO ZIKO KWENYE MAJINA YA WATOTO.

Mali hizi hamuwezi kuzigawa ndoa inapovunjika. Hii ni kwasababu kitendo cha kuandika majina ya watoto ni sawa na kuwa mlikubaliana kuwapa zawadi watoto.

Ukitoa zawadi maana yake maslahi(ownership interest) yenu katika hiyo mali yalishahama kwenda kwa watoto kwa njia ya zawadi nanyi hamna maslahi tena katika hiyo mali.

MALI ZILIZOANDIKWA MAJINA YA WATU WENGINE.

Mali ambayo haina jina la mke au mme sio rahisi kuigawa ndoa inapovunjika.

Huyu HACHRAF HAKIMI aliandika majina ya mama yake. Mali ya namna hii ni vigumu kuigawa kama mali ya ndoa kwasababu inaonekana inamilikiwa na mtu mwingine.

Kwa msingi huu huwezi kugawa mali ambayo haihusiki. Wengine huandika majina ya ndugu zao, marafiki nk.

Ndio, akifanya hivi basi ni vigumu hiyo mali kuigawa ndoa ikivunjika hata kama una uhakika wa 100% kuwa ni yenu.

Hii ni kwasababu ushahidi wa nani mmiliki wa mali ni nyaraka au usajili. Nyaraka na usajili unaonesha mtu mwingine ni vigumu useme hii mali ni yetu.

MALI INAYOBADILISHWA UMILIKI.

Kama mali imeanza ikiwa ni ya ndoa halaf ikabadilishwa majina hiyo unaweza kuidai na ikagawiwa.

Wapo wanandoa wakiona mambo yameanza kubadilika basi ama huanza kubadili majina ya mali au huuza.

Ikiwa tarehe zitaonesha mali ilibadilishwa au kuuzwa kipindi cha ndoa na ni mali ya wanandoa,na mwenza hakuwa ameridhia, basi ubadilishwaji huo ama uuzaji huo ni batili na hiyo mali itarudishwa kwenye mali za wanandoa ili igawiwe.

WANANDOA WANAWEZA KUFANYA NINI KUHUSU MALI.

KWANZA, yafaa ikiwa mtakubaliana basi mali iwe na majina ya wote mke na mme. Iwe ni gari, kiwanja, nyumba,akaunti benki, nk. Sheria inaruhusu.

Hii husaidia sana hata kipindi cha kifo ambapo mjane au mgane hawezi kusumbuliwa.

PILI, mnaweza kuwa na makubaliano kuhusu kila mali,kuanzia zile ambazo mlikuwa nazo kabla hamjaoana, mpaka zile mtakazopata wakati wa ndoa. Mtakubaliana ipi iwe ya pamoja na ipi iwe ya mmoja.

Japo hili ni gumu kwa maisha yetu sababu ukilianzisha hili utaambiwa HUNA MAPENZI YA KWELI.

TATU, muwe na utaratibu wa kucheki mara kwa mara hadhi(status ) ya mali. Pitia pitia huko Ardhi, TRA, Serikali ya mtaa ujue. Msilale sana.

Huenda ukagundua kitu mapema kabla mambo hayajaharibika.

NNE, msajili/andika mali kwa majina ya watoto, maana yake muwape zawadi watoto. Hata kama mnatumia nyie lakini ikijulikana ni za watoto.

Ila lazima iwe imesajiliwa na sio kusema tu kwa mdomo kuwa hizi ni mali ni za watoto.

Ukisema mali ni za watoto na hakuna usajili rasmi hiyo hukataliwa sababu watoto hawana mali bali mali ni za wazazi na majina zitakuwa zinasoma wazazi.

TANO, kama hamuwezi kufanya lolote mapema kati ya hayo manne juu basi mmoja awe tayari kupoteza au msubiri mahakama iwaamue.

REJEA ya maandiko haya ni :-

Sheria ya ndoa R:E 2019 hasa vifungu vya 58,59,,60, na114.

NA

Shauri la Bi Hawa Mohammed vs Ally Sefu(Rufaa Na.9/1983) TZCA 12.
Mateso yote ya nini haya?? Sifungi ndoa, acha nilee watoto wangu tu
 
  • Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
  • Hapo Hakimi ametumia false pretense.
Hiyo haiwahusu mahakama.., mali sio ya ndoa. Ilipaswa mke awe anauliza mshahara upo wapi?
 
  • Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
  • Hapo Hakimi ametumia false pretense.
Sheria wakati mwingine ni kama mtego fulani. Yeye mkewe atakua responsible kutoa matunzo kwa mtoto, kwanini awe responsible kutoa matunzo kwa mwanamke ambaye wamekwisha achana? Na bado anaweza kujitetea kwamba kwa sababu hana kipato anaomba mkewe atoe child support kwa zaidi ya 50% kisha yeye atajaribu kuomba mama yake amsaidie asilimia zilizobaki. Mama akikataa maana yake ahudumie kwa asilimia zote watoto mwanamama.
 
SOMO LA MALI KWA WANANDOA KWA KILICHOTOKEA KWA ACHRAF HAKIMI NA MKEWE.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.

Mke wa ACHRAF HAKIMI ameshindwa kupewa mali yoyote baada ya ndoa yao kuvunjika kwasababu Hakimi aliziandika mali zote jina la mama yake mzazi.

Je jambo hili linawezekana kwa Sheria za Tanzania ?.

Ndio linawezekana , ni hivi :-

Kwa wanandoa kuna mali za aina 2;-

1. Mali zilizopatikana kabla ya ndoa.
2. Mali zilizopatikana wakati wa ndoa.

MALI ZILIZOPATIKANA KABLA YA NDOA.

Hizi ni mali ambazo mtu anakuwa nazo kabla hajaoa ama kuolewa. Yumkini akiingia kwenye ndoa anaingia nazo.

Hata hivyo Sheria ya ndoa inasema mali hizi zinahesabika si za ndoa kwa maana ya kuwa huyo mwenye nazo ni zake peke yake bila mwenza wake. Ndoa ikivunjika haziwezi kugawiwa.

Pamoja na hayo, mali hizo pia zinaweza kubadilika na kuwa za ndoa ikiwa mambo mawili yatafanyika.

KWANZA, ikiwa mwenza mwenye hizo mali ataingia makubaliano na mwenza wake kuwa ziwe za ndoa basi zitakuwa za ndoa na itakapovunjika basi zitagawiwa

PILI, iwapo mali umeingia nayo kwenye ndoa lakini kipindi cha ndoa imeendelezwa.

Mfano, Umeingia kwenye ndoa na kiwanja chako lakini kipindi cha ndoa ndo kimejengwa, AU kilikuwa kimejengwa lakini ni pagala tu, kipindi cha ndoa ndo mmemalizia na kuwa nyumba kamili.

Hapa ndoa ikivunjika mtagawana na hautasema alinikuta na Pagala langu au kiwanja changu. Kitendo cha kuendeleza mkiwa wote kinampa haki mwingine na kuwa mali ya wote.

Lakini kama mali ameingia nayo kwenye ndoa na hakuna maendelezo yoyote yaliyofanyika kipindi cha ndoa basi hiyo mali haiwezi kugawiwa ndoa ikivunjika na inabaki mali ya mwenza huyo pekee.

MALI ZILIZOPATIKANA WAKATI WA NDOA.

Hizi huhesabika moja kwa moja kuwa ni za wanandoa wote mpaka isemwe vinginevyo.

Na haijalishi zipo kwenye jina la mke au mme, madhali zilipatikana kipindi cha ndoa basi zinahesabika ni za wanandoa na zinastahili kugawiwa ndoa inapovunjika.

Hata hivyo, ili ziweze kugawiwa ni lazima kila mwanandoa athibitishe mchango wake katika upatikanaji wa hizo mali.

Tafsiri ya mchango ni pamoja na pesa, vifaa, lakini hata kazi za nyumban nao ni mchango katika kupatikana kwa mali.

Mke au mme anayebaki nyumbani kwa ajili ya shughuli za nyumbani anahesabika amechangia kwa kile kinachopatikana kutoka kwa yule aliyeingia mtaani kutafuta.

Kwahiyo wakati wa kuthibitisha mchango hayo yote yanazingatiwa.

JE MGAWANYO WA MALI NI NUSU KWA NUSU.

Hapana, mgawanyo mali za ndoa inapovunjika sio lazima kuwa nusu kwa nusu. Inaweza kuwa 20%/80%, 70%/30%, 90%/10%, nk nk. Kwa ufupi hakuna kiwango maalum, hata kukosa kabisa kupo.

Kikubwa ni kuwa utapata fungu lako kutokana kiwango cha mchango wako kama tulivyoona hapo juu. Na kama huna mchango kabisa basi waweza kutoka kapa pia.

MALI AMBAZO ZIKO KWENYE MAJINA YA WATOTO.

Mali hizi hamuwezi kuzigawa ndoa inapovunjika. Hii ni kwasababu kitendo cha kuandika majina ya watoto ni sawa na kuwa mlikubaliana kuwapa zawadi watoto.

Ukitoa zawadi maana yake maslahi(ownership interest) yenu katika hiyo mali yalishahama kwenda kwa watoto kwa njia ya zawadi nanyi hamna maslahi tena katika hiyo mali.

MALI ZILIZOANDIKWA MAJINA YA WATU WENGINE.

Mali ambayo haina jina la mke au mme sio rahisi kuigawa ndoa inapovunjika.

Huyu HACHRAF HAKIMI aliandika majina ya mama yake. Mali ya namna hii ni vigumu kuigawa kama mali ya ndoa kwasababu inaonekana inamilikiwa na mtu mwingine.

Kwa msingi huu huwezi kugawa mali ambayo haihusiki. Wengine huandika majina ya ndugu zao, marafiki nk.

Ndio, akifanya hivi basi ni vigumu hiyo mali kuigawa ndoa ikivunjika hata kama una uhakika wa 100% kuwa ni yenu.

Hii ni kwasababu ushahidi wa nani mmiliki wa mali ni nyaraka au usajili. Nyaraka na usajili unaonesha mtu mwingine ni vigumu useme hii mali ni yetu.

MALI INAYOBADILISHWA UMILIKI.

Kama mali imeanza ikiwa ni ya ndoa halaf ikabadilishwa majina hiyo unaweza kuidai na ikagawiwa.

Wapo wanandoa wakiona mambo yameanza kubadilika basi ama huanza kubadili majina ya mali au huuza.

Ikiwa tarehe zitaonesha mali ilibadilishwa au kuuzwa kipindi cha ndoa na ni mali ya wanandoa,na mwenza hakuwa ameridhia, basi ubadilishwaji huo ama uuzaji huo ni batili na hiyo mali itarudishwa kwenye mali za wanandoa ili igawiwe.

WANANDOA WANAWEZA KUFANYA NINI KUHUSU MALI.

KWANZA, yafaa ikiwa mtakubaliana basi mali iwe na majina ya wote mke na mme. Iwe ni gari, kiwanja, nyumba,akaunti benki, nk. Sheria inaruhusu.

Hii husaidia sana hata kipindi cha kifo ambapo mjane au mgane hawezi kusumbuliwa.

PILI, mnaweza kuwa na makubaliano kuhusu kila mali,kuanzia zile ambazo mlikuwa nazo kabla hamjaoana, mpaka zile mtakazopata wakati wa ndoa. Mtakubaliana ipi iwe ya pamoja na ipi iwe ya mmoja.

Japo hili ni gumu kwa maisha yetu sababu ukilianzisha hili utaambiwa HUNA MAPENZI YA KWELI.

TATU, muwe na utaratibu wa kucheki mara kwa mara hadhi(status ) ya mali. Pitia pitia huko Ardhi, TRA, Serikali ya mtaa ujue. Msilale sana.

Huenda ukagundua kitu mapema kabla mambo hayajaharibika.

NNE, msajili/andika mali kwa majina ya watoto, maana yake muwape zawadi watoto. Hata kama mnatumia nyie lakini ikijulikana ni za watoto.

Ila lazima iwe imesajiliwa na sio kusema tu kwa mdomo kuwa hizi ni mali ni za watoto.

Ukisema mali ni za watoto na hakuna usajili rasmi hiyo hukataliwa sababu watoto hawana mali bali mali ni za wazazi na majina zitakuwa zinasoma wazazi.

TANO, kama hamuwezi kufanya lolote mapema kati ya hayo manne juu basi mmoja awe tayari kupoteza au msubiri mahakama iwaamue.

REJEA ya maandiko haya ni :-

Sheria ya ndoa R:E 2019 hasa vifungu vya 58,59,,60, na114.

NA

Shauri la Bi Hawa Mohammed vs Ally Sefu(Rufaa Na.9/1983) TZCA 12.
Ahsante tutaandika kwa majina ya mama inatosha sana mkuu
 
Sheria wakati mwingine ni kama mtego fulani. Yeye mkewe atakua responsible kutoa matunzo kwa mtoto, kwanini awe responsible kutoa matunzo kwa mwanamke ambaye wamekwisha achana? Na bado anaweza kujitetea kwamba kwa sababu hana kipato anaomba mkewe atoe child support kwa zaidi ya 50% kisha yeye atajaribu kuomba mama yake amsaidie asilimia zilizobaki. Mama akikataa maana yake ahudumie kwa asilimia zote watoto mwanamama.
Jamaa ni genius , aliangalia possibilities zote hizo akaona kuna win win kila sehemu
 
Mi nimeshabugi aisee kila kitu nimemuonesha na kumshikirisha huyu mke wangu na ameshaanza kuwa na jeuri sijui ntaanzia wapi
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kila mtu kasema lake, wapo waliomsifu na wapo waliomponda. Mimi nitajadili Jambo hili Kwa uchache katika mizania ya Haki, ukweli na upendo. Kama mnavyojua mambo hayo Matatu ndio ninayoyapigia debe. Hiyo ndio dini ya Watibeli.

Kwa taarifa za kesi nilivyoisikia mpaka sasa nadiriki kusema HAKIMI hakutenda HAKI. Kwa sababu zifuatazo;

1. Hakimi hakuwa mwaminifu.
Hakimi hakuwa mwaminifu katika ndoa yake katika maeneo yafuatayo;
a) Mapenzi, HAKIMI anatuhuma za kum-cheat Mkewe achilia mbali hiyo kesi ya ubakaji inayomkabili.

b) Fedha na Mali,
HAKIMI hakuwa mwaminifu katika suala la fedha na Mali katika ndoa. Kukosa uaminifu, kutokuwa mkweli kunamfanya Hakimi asiwe mwenye Haki.

2. Hakimi hakumpenda mkewe.
HAKIMI anampenda Mama yake kuliko Mkewe. Hii katika mahusiano ya ndoa sio Haki kwa Mke au Mume. Kwenye ndoa au familia ni Haki ya Mke au Mume kupendwa na Mwenza wake kuliko MTU yeyote Yule.

Haiwezekani 80% umuingizie Mama yako Wakati umeoa na unampenda Mkeo au Mumeo. Upendo wa Hakimi kwa Mama yake ni mkubwa maradufu kuliko alivyompenda Mkewe. Hiyo sio Haki.

3. Hakimi alikusudia kumtapeli Mkewe. Hakuwa anampenda.
Ndio maana aliweza kum-cheat na kumsaliti kimapenzi na muda huohuo akawa anamficha masuala ya Mapato yake. Huo ni Utapeli, na hii ni Kutokana alikuwa hampendi.

Mambo ya muhimu;
1. Kama HAKIMI angekuwa mwenye Haki angekuambia Binti wa watu tangu mwanzo kuwa Kipato changu kitakuwa kinamilikiwa Kwa sehemu kubwa na Mama. Ili binti mwenyewe aamue. Hii ni pamoja na Mali zitakazonunuliwa Kutokana na kipato chake. Kama wanavyofanya Watu wengine wenye Haki.

2. Yule Mwanamke hakuomba Talaka Kwa lengo la Kutaka Mali za Hakimi, isipokuwa ni Makosa ya Hakimi ya kutokuwa mwaminifu Kwa kumsaliti ndio kumemfanya aombe Talaka. Kwa watu waaminifu na wenye Haki Usaliti ni kosa lisilosameheka.

3. Ni kweli Mshahara wa mtu anaweza kuutumia vile atakavyo ilimradi anatekeleza majukumu ya kifamilia vizuri.
Hivyo Hakimi anaweza kuwa na Haki ya kutumia Mshahara wake atakavyo. Tatizo linakuja Kuwa matumizi ya Pesa au kipato yatatafsiri moyo wa mtu ulipo. Wanasema hazina ya mtu ilipo ndipo moyo wake ulipo.

Hakuna Mwanamke ambaye atajiona anapendwa ilhali zaidi ya 80% ya kipato cha mume wake kinatumika nje ya matumizi ya Nyumbani.

Jambo moja la kuweka Akilini hapa ni kuwa, Wanawake Hawana sababu ya kuogopa Michezo ya namna Hii Kwa sababu nao ni kina Mama wamezaa, hivyo Kile wanachokifanya wanaume ndicho watakachokifanya Watoto wao.

Hii ni kusema, ikiwa kuna mwanaume atamuiga Hakimi kuwekeza Kwa Mamaye, vivyohivyo watoto wako uliowazaa watawekeza kwa mkeo (Mama Yao) uliyemkatili. Hivyo Ngoma inakuwa droo!

Kwenye upendo kuna ukweli na Haki. Kwenye upendo mambo ya Pesa na Mali hayawezi kuwa kitu kikubwa.

Alichofanya HAKIMI ni uhuni, hasa kama ni kweli amem-cheat Mkewe mpaka akaomba Talaka. Ni uhuni ambao Watibeli hatuuungi Mkono. Na inaonekana Amekataa hata kuomba Msamaha.

Ieleweke kuwa ku-cheat Kwa wengine ni kosa lisilosameheka. Na hakuna mwenye uhalali WA ku-cheat iwe mwanaume au Mwanamke.

Wewe kama unajijua huwezi kuwa mwaminifu ni Bora usioe au kuolewa. Kwani unachoenda kufanya ni utapeli, uhuni na dhulma

Nipumzike sasa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
 
Mkuu, umeandika mambo mengi ya ukweli na ni vema na haki, lakini, talaka isiwe ni chanzo cha mapato au njia ya kumtajirisha mtu wakati hakutolea jasho hizo mali. Sheria ya Tanzania inasema mnagawana mali za familia, kwa mujibu wa mchango wa mtu katika upatikanaji wake. Japo wanasema kazi za nyumbani anazofanya mwanamke ni mchango katika upatikanaji wa mali za familia.

Bahati mbaya wanawake wengi wamekua na tamaa na ndoa zimeondoka thamani. Watu wanaogopa ndoa na ata wakioa wanaficha mali kwenye makampuni (limited by shares) au kuziweka kwenye majina ya watu wengine. Tunakoelekea ni kubaya zaidi
 
Back
Top Bottom