Songwe: Polisi wakamata walioanzisha kiwanda feki cha Sukari

Songwe: Polisi wakamata walioanzisha kiwanda feki cha Sukari

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waliokamatwa ni Oscar Chisunga, John Chisunga, Moses Mussa, Fredy Thobias na Eddy Mwashambwa ambapo wamekutwa na Kilo 440 za Sukari iliyoingizwa nchini kimagendo.

Kamanda wa Polisi ACP Alex Mukama amesema Wafanyabiashara hao wakazi wa Mlowo wilayani Mbozi walighushi Sukari na kuiweka kwenye mifuko yenye Nembo ya Kiwanda cha Sukari Kilombero.

Aidha, walikutwa na mashine 3 za kufungashia Sukari, mifuko mitupu 44 ya Kilo 20 ya Salim Sugar Co.LTD, mifuko 110 ya Kilo 50 ya Illovo Sugar ya Malawi na vifungashio vya Sukari 1,164 vya Kilo 1 kila kimoja vikiwa na nembo ya Kilombero Sugar Company.

===================

Wafanyabiashara watano wakazi wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe wanashikiliwa Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukutwa na sukari ilioghushiwa na kufanana na nembo ya Kiwanda cha Sukari cha Kampuni ya Kilombero.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ACP Alex Mukama amewataja waliokamatwa ni pamoja na Oscar Chisunga (35), John Chisunga (36), Moses Mussa (36) ,Fredy Thobias (28) na Eddy Mwashambwa (44) ambapo wamekutwa na kilo 440 za sukari zinazodaiwa kuingizwa nchini kimagendo na kuwekwa kwenye mifuko ya sukari kutoka viwanda vya ndani ya nchi.

Watuhumiwa hao pia wanadaiwa kukutwa na mashine tatu tofauti zinazotumika kufungasha bidhaa za sukari, mikasi mitatu, mifuko mitupu 110 ya sukari ya Kg50 ya kampuni ya SALIM SUGAR CO.LTD ya nchi kutoka nchi jirani.

Pia wamekutwa na mifuko mitupu 44 ya sukari kilo 20 ya Kampuni ya TSEKETSEKE ya ILLOVO SUGAR ya nchi jirani, mifuko mitupu mitatu ya sukari ya kilo 20 ya Kampuni ya KILOMBERO SUGAR COMPANY na vifungashio vya Sukari 1,164 vya ujazo wa kilo 1 kila kimoja na rola moja lenye nembo ya sukari ya KILOMBERO SUGAR COMPANY.

Kamanda Mukama amesema kuwa Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali imefanya operesheni maalumu ya Polisi iliyofanyika kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Bodi ya Sukari Tanzania na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero ndiyo imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa.

Tayari uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wengine kutoka kiwanda cha Sukari Kilombero ambao wanashirikiana na watuhumiwa kutoa nyaraka za Kampuni kama vifungashio na mifuko yakubebea Sukari.

Ametoa wito kwa wananchi wote kutokujihusisha na shughuri za kuhujumu viwanda vyetu vya ndani kwani huo ni uhujumu wa Uchumi wa viwanda na taifa kwa ujumla.

MWANANCHI
 
Kuna kitu uwa kinanikwaza nchi hii watu wabunifu kukamatwa.

Nchi hii ina upungufu wa sukari tani 200,000 kila mwaka halafu na population inaongezeka kila siku.

Wanajitokeza watu wanaanzisha kiwanda baada wachukuliwe wapewe ujuzi na wasajiliwe ili wafanye kazi zao kwa uhuru eti wanakamatwa kwa lipi?

Sukari ni pombe bangi au madawa ya kulevya ? Jiulize hao watu wangeendelezwa na kupewa njia Bora za ufanyaji kazi tungekuwa wapi leo?

Ccm na wafanyabiashara wakubwa wanaua vipaji vya wabunifu na wafanyabiashara wadogo Kuna shida gani mtu kuanzisha kiwanda kabla ya registration?

Baada tukague ubora wa bidhaa yake tunakimbilia kuwafunga watu?

Halafu Kikwazo kikubwa Cha ukuaji wa viwanda Tanzania ni wizara yenyewe ya viwanda na TBS waachieni watu wapeni elimu ili wapunguze tatizo la sukari nchini wasajiliwe walipe kodi sio kuwapeleka jela

Watu wwanashindwa kuanzisha viwanda vya mafuta, sabuni na sukari kwa sababu ya urasimu wa serikali yenyewe

Rais hawa watu waachiwe Mara moja wakafanye Kazi.

=====

Pia wamekutwa na mifuko mitupu 44 ya sukari kilo 20 ya Kampuni ya TSEKETSEKE ya ILLOVO SUGAR ya nchi jirani, mifuko mitupu mitatu ya sukari ya kilo 20 ya Kampuni ya KILOMBERO SUGAR COMPANY na vifungashio vya Sukari 1,164 vya ujazo wa kilo 1 kila kimoja na rola moja lenye nembo ya sukari ya KILOMBERO SUGAR COMPANY .

Kamanda Mukama amesema kuwa Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali imefanya operesheni maalumu ya Polisi iliyofanyika kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Bodi ya Sukari Tanzania na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero ndiyo imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa.

Tayari uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wengine kutoka kiwanda cha Sukari Kilombero ambao wanashirikiana na watuhumiwa kutoa nyaraka za Kampuni kama vifungashio na mifuko yakubebea Sukari.

Ametoa wito kwa wananchi wote kutokujihusisha na shughuri za kuhujumu viwanda vyetu vya ndani kwani huo ni uhujumu wa Uchumi wa viwanda na taifa kwa ujumla.

Chanzo: Mwananchi
 
Hao jamaa sioni kwanini walishindwa kufuata sheria na taratibu za kuanzisha kiwanda, walichofanya ni kosa bila kujali kama tuna uhaba wa sukari.
 
badala wawasaidie kufungua kampuni wanawafungall

Hiyo ni magendo ya sukari hua inapigwa zambia au malawi, inaingia kimagendo halafu inakua packed kiujanjaujanja watu wanafanya biashara enzi za jiwe hiyo ilikua uhujumu uchumi na michezo hiyo wanafanya wafanyabiashara wengi tu kwenye bidhaa nyingi
 
Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

1670442139108.jpg
 
Kabuni kiwanda cha sukari kakamatwa hii serikali ni ya hovyo sana Polisi mjitafakari
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

#ITVUpdates
1670442139108.jpg
 
Kabla ya kumtetea lazima tujue hiyo sukari inafaa kwa matumizi ya binadamu? Maana inakwenda kuingia mwilini isije kwenda kuharibu figo za watu. Watu wamevurugwa hawajali tena afya za wengine wanaangalia pesa tu. Kwanini asichukue vibali tbs /tfda kama hiyo sukari yake ni safe na haina madhara kwa binadamu
 
Kabuni kiwanda cha sukari kakamatwa hii serikali ni ya hovyo sana Polisi mjitafakari
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekamata kiwanda feki cha kutengeneza sukari katika eneo la Mlowo lililopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, pamoja na watuhumiwa 5 wakiwa na kilo 440 za sukari pamoja na vifungashio ambavyo vinadaiwa kutengenezwa nje ya nchi.

#ITVUpdatesView attachment 2439064
Serikali ituambie vipaji kama hivi vinaendelezwaje?
 
Back
Top Bottom