Sophia Mjema ateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Sophia Mjema ateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Dkt Sophia Mjema amechukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka, yeye ndiye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi.

Sophia anakuwa mwanamke wa kwanza kushika nafsi hiyo.

Wanaomfahamu wanaelewa kwamba Sophia ni mtu wa kazi, mtu wa siasa. Mwaka 2020 alionesha vizuri uwezo wake kwenye siasa za chama alipotaka Ubunge wa Ilala na kuleta upinzani mkubwa kwa Zungu.
akiwa Mkuu wa Wilaya katika maeneo yote aliyopita nako hakuwa mtu wa kupoa.

Wakati huu ambapo Mikutano ya Siasa itafanyika, wapinzani watarajie mtu makini zaidi na mtata kuliko Shaka.
 

Attachments

  • img-20190427-wa0054-833054946.jpg
    img-20190427-wa0054-833054946.jpg
    34.6 KB · Views: 9
Huko CCM ni kama wamevurugana baada ya kujua sasa yanayokwenda kutokea ni balaa la gharika ya kisiasa. Walikuwa wanapambana na bondia aliyefungwa miguu sasa kakata kamba hivyo Ata fly like a butterfly and sting like a bee! Ni kipigo tuu. Na kapiteni anatua 25/1

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
FB_IMG_1672921103951.jpg
 
Anachukua nafasi ya Shaka Hamdu

Bado haijafahamika kama Hamdu Shaka atapangiwa majukumu mengine au ndio Kabwagwa jumla.

===

Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kimemteua Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema kuchukua ya Shaka Hamdu Shaka

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Mohamed Said Mohamed Dimwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar

---

Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Taifa Leo imekutana na kufanya UTEUZI wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo,

====
1. Daniel Chongolo - Katibu Mkuu

2. Anamringi Macha - Naibu Katibu Mkuu Bara

3. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Said Mohamed Dimwa

4. Ndugu Sophia Mjema
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi

5. Dkt. Frank Haule
Katibu wa Uchumi na Fedha

6. Mbarouk Nassor Mbarouk
Mkuu wa Idara ya Kimataifa

7. Issa Haji Gavu
Idara ya Organaizeisheni
Naiombea CCM amani na furaha...Maana bila CCM imara nchi itayumba...Mkachape kazi comreds, taifa linawategemea
 
Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Taifa Leo imekutana na kufanya UTEUZI wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo,

====
1. Daniel Chongolo - Katibu Mkuu

2. Anamringi Macha - Naibu Katibu Mkuu Bara

3. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Said Mohamed Dimwa

4. Ndugu Sophia Mjema
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi

5. Dkt. Frank Haule
Katibu wa Uchumi na Fedha

6. Mbarouk Nassor Mbarouk
Mkuu wa Idara ya Kimataifa

7. Issa Haji Gavu
Idara ya Organaizeisheni
Duuh hawa ni wachanga kisiasa wote kabisa
 
Mataga enzi zenu zimeisha, kaa kimya tu.
Hii ni tetesi till habari rasmi itakapotangazwa na credible source!

Na kama ni hivyo....

CCM watakuwa wameingia choo cha kike,sababu huyo Sophia mjema alikwisha prove failure kwenye teuzi ile ya kwanza.

Hawezi kuendana na kasi inayokuka ya siasa za majukwaani kwenye uhuru wa vyama vyote.

Labda Samia anataka taifa hili liwe la "KE" territory na inayoenda kuangukia Pua.
 
Back
Top Bottom