Special thread: Kutana na waagizaji wa magari kutoka Japan
Huo utaratibu wa kulipa kidogo ukoje na unachukua muda gani..?? Haya magari tunayapenda na tuna mahitaji nayo mwanawane lakini hizo hela za kulipa kwa mkupuo ndio hatuna aisee..!!

~~Kitakachokupa ushindi ni juhudi zako~~
 
Rav 4 kill Time zilitoka miaka ya 2000 mpaka 2005, ni Toleo la Toyota la muundo
Wa SUV, ambalo ni gumu, rahisi kuhudumia kuanzia matengenezo na mafuta. Zipo zenye injini kubwa ya kawaida ambayo ni Cc 2000 na pia zipo za Cc 1800, zipo zenye 4wheel drive na ambazo hazina. Kwa ujumla ni gari nzuri sana na bei yake imeshuka kutoka 18m mpaka 15.5m
Kwa hiyo mkuu nikiwa na 15.5m nikija kwenye ofisi yenu mnanipatia hiyo gari ikiwa na vibali vyote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hujaamua aina ya gari na lini unataka kumiliki gari ya kwa mala ya kwanza basi muhim ukafaham haya yafuatayo.

1. Tengeneza Bajeti. Baadhi ya watu katika Jamii zetu, wamekua na kawaida ya kununua gari bila kuzingatia bajeti ya vitu kama matengenezo, mafuta, malipo ya maegesho, Vibali, n.k jambo linalopelekea kushindwa kufanya mambo mengine ya msingi iwapo kipato ni cha kati na aina ya gari unalomiliki linahitaji bajeti kubwa.

2. Amua utatumia utaratibu gani wa malipo. Kuna njia za kulipia gari yako kama vile kulipia kwa awamu, kupewa mkopo na taasisi za fedha, au kuhifadhi we mwenyewe na kilipia yote kwa mara moja. Ni muhim kuangalia hili ili kujiepusha na hali ya kujiumiza kiuchumi pindi unapoamua kumiliki gari kwa mara ya kwanza. Iwapo kipato ni cha kati unaweza kuzungumza na muuzaji husika ukalipia kidogo kidogo na mwishowe ukamalizia na kupewa gari yako, hii itakuepusha kumaliza mpaka akiba ambayo ingeweza kukusaidia wakati wa dharula.

3. Angalia unataka nini kwenye gari yako. Usinunue gari kwa sababu umemuona jilani yako ana gari. Ni vizuri sana uangalie mambo mbali mbali kabla hujaamua kuchukua aina flani ya gari, vitu vya msingi kijiuliza ni kama vile (unataka gari yenyewe 4WD, 2WD, ya juu juu au chini, yenye sun roof, yenye camera ya nyima, inayotumua upepo kwenye shock up au za kawaida, itakua inapita njia mbovu zaidi au ya lami, iwe ya aina gani ya mafuta, iwe imetembea kilomita ngapi, aina ya injini na ukubwa wake n.k ukiacha kununua gari kwa ushabiki utakua kwenye nafasi nzuri ya kukipenda chombo chako na kupatq kilicho sahihi ambacho hakitakupa tabu moyoni.

4. Chunguza bei za kuimiliki hiyo gari ya ndoto yako. Hapa usifike kwa muuzaji au muagizaji mmoja ukamalizana nae halafu baada ya siku 2 unakutana na gari kama hiyo inauzwa kwa bei chini zaidi na ambayo ina ubora kuliko hiyo uliyouziwa bila kutafiti bei kwanza. Hii itakusaidia kuokoa kiasi cha pesa na pia kupata kilicho bora zaidi.

5. Chagua aina tofauti zinazofanana ili kuzilinganisha. Unapopenda aina flani ya gari na kuamua kuchukua hiyo hiyo wakati mwingine hua inaleta maumivu pale unapogundua aina flani ya gari ni bora zaidi kuliko hiyo na uzuri zote zinalingana bei na mwonekano hazitofautiani sana. Hapa nazungumzia gari kama Toyota Allion Vs Premio, Toyota Allex Vs Run X, Alteza Vs Lexus IS 200, n.k

6. Chunguzq gari husika itakua ikigharim kiasi gani kwa mwezi na kwa mwaka. Kununua gari hua ni jambo jepesi, lakini wakati mwingine kuihudumia gari hua ni jambo gumu kidogo haswa kama huitumii vizuri gari hiyo kukuingizia pesa zitakazokua zikiwesha uihudumie na pia uweze kutekeleza majuk yako mengine. Hapa angalia gharama za Bima, Mkopo, Vibali, Usajili, Ushuru, Mafuta, Matengenezo, Dharula n.k

Zifuatazo ni baadhi ya aina za magari ambazo zinawafaa sana vijana au watu wa kipato cha kati.

Gari hizo ni Vitz, Raum, IST, Passo, Platz, Ractis, Fun Cargo, Porte, Bb, Sienta, Duet, Nissan Note, Nissan March, Honda Fit, Spacio, Carina T.I, Cami, Allex/ Run X, Allion, Premio n.k

Gari hizo hapo juu hutumia mafuta kidogo, matengenezo yake ni rahisi na vifaa vyake ni vingi hapa Tanzania.

Wasalaam

Kimomwe Motors Tanzania Limited- Waagizaji wa Magari toka Japan

0746267740
Mkuu nataka Toyota liteace au Suzuki carry zinaweza kuwa bei gani
 
Huo utaratibu wa kulipa kidogo ukoje na unachukua muda gani..?? Haya magari tunayapenda na tuna mahitaji nayo mwanawane lakini hizo hela za kulipa kwa mkupuo ndio hatuna aisee..!!

~~Kitakachokupa ushindi ni juhudi zako~~

Huu ni utaratibu wa kawaida kwa kuwekeza. Ni sawa na unajihifadhia kidogo kidogo mwenyewe ili uje kutimiza lengo lako, ila kwa kutambua dharula nyingi zinazotokea ndipo tukapewa wazo na baadhi ya wateja kwamba waweke pesa kwenye akaunti yetu maalumu mpaka kitakapotimia kiasi cha kumuwezesha kuagiza gari flani.

Tunapenda anayewekeza asizidishe miezi 24 na asiwe chini ya miezi 3. Hii ni sawa na wamama wengi wanavyofanya kwamba, wanaenda kwa muuza Friji wanalipa kidogo kidogo then kiasi kikitimia anachukua friji yake.
 
Mkuu Noah old model mnauzaji happy kwenu, je kwa mtu wa kipato cha kati inaweza kumfaa?
 
Hizi ni baadhi tu kutoka katika stock washirika. Gharama zimejumuisha Manunuzi, Usafiri, Ushuru na Gharama za Bandari.

Kimomwe Motors (T) Ltd waagizaji wa Magari kutoka Japan, Singapore, Ulaya Dubai na Korea tunaokoa Mda na Tunaokoa Pesa

7AFF5967-AB7F-44A8-9772-7F080F0D7685.png
EAA0AD7C-00A2-4643-9042-F16654919CA0.png
D6042536-7501-4904-813D-B4AC38E35105.png
EDD94FA1-D99B-472B-A887-38D8F8276D6A.png
9B379795-C73E-487A-BBEC-4D0E7B72276E.png
7A1B7326-CDED-4A77-819E-D010AE883B0D.png
F46156AA-40DB-4125-9935-5D39EEC5ECA9.jpeg
1BBAEFD0-2F9C-4E71-9715-BA7FE947A959.jpeg
CA5695EB-4FBF-4632-8D0B-D3C839154743.jpeg
7C48FE6E-ED9F-4CEC-B567-21CDFCE1DDA4.jpeg
55C02A95-77A4-455A-BBA5-6D2044EB7275.jpeg
D383EB97-57C4-4E21-AF9C-042E467C9CD0.jpeg


Zaidi piga 0746267740 Au tembelea Ofisi zetu za Dar es Salaam na Mbeya.

HERI YA MWAKA MPYA KWETU SOTE
 
Back
Top Bottom