KIMOMWEMOTORS
JF-Expert Member
- May 17, 2018
- 358
- 675
- Thread starter
- #141
Si kweli kwamba hatuna staff na hatulipi kodi boss. Staff tunao wa kutosha kuhudumia umma wa watanzania ndio mana ukifatilia mitandaoni utaona posts nyingi kuhusu huduma zetu kutoka kwa watu tofauti wa kampuni. Na kuhusu kodi iko wazi kwamba ni ngumu sana kufanya biashara kwa uwazi na kujitangaza halafu tuwe hatulipii kodi.
Sababu nyingine kwa nini hatukuongeza bei hiyo gari ni hii ya kwamba mwanzo tulipoiagiza tayari hesabu zake zilishaingia kwenye makadirio ya kodi hivyo isingekua busara kuitangaza bei ya juu zaidi wakati lengo la kuiuza ni kurudisha pesa tuliyotumia kumuagizia huyu mteja wetu aliyepatwa na matatizo akiwa nje ya nchi na hivyo kushindwa kuilipia kwa wakati huu.