Salam ndugu wadau.
Nissan Dualis katika mataifa mengine hujulikana kama Nissan Qashqai isipokua katika soko la Japan na Autralia. Gari hii ndogo ya juu juu ilianza kuundwa kuanzia mwaka 2006.
INJINI na MAFUTA
Kwa upande wa injini, zipo Nissan Dualis chache zenye injini ya Cc 1600 wakati injini inayofahamika zaidi ni MR20DE yenye Cc 2000 ambayo hii ni ya kisasa na hupatikana pia kwenye Nissan Xtrail kuanzia model ya 2007 (New Model). Injini hiyo ikiwa kwenye Dualis hukadiriwa kutumia mpaka kilomita 14 kwa lita iwapo kwenye barabara kuu.
Kuna Dualis zenye 2WD pekee na zipo zenye Option ya 2WD na 4WD.
UIMARA KATIKA MWENDO
Inaelezwa kua gari hii inapokua katika mwendo hua imetulia barabarani japo sio sana kwa wale waliozinyanyua juu kidogo.
VIPULI VYAKE
Wateja watu waliozitumia gari hizi kwa mda sasa wanaelezea kwamba vifaa au vipuli vyake vinakufa baada ya matumizi ya mda mrefu ikilinganishwa na gari za juu juu za Toyota. Upatikanaji wa vifaa vyake ni mkubwa kwa miji mikubwa kama Dar, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Iringa, na Kilimanjaro...vifaa hivyo hupatikana kwa gharama za juu kiasi ingawa sifa yake ni kwamba hutabadirisha mara kwa mara.
ILI UFURAHIE GARI HII
Ili uweze kufahia vizuri gari hii inashauriwa kuhakikisha unatumia oil inayoshauriwa kwa Nissan, lakini pia kufanya service kila inapohitajika bila kupitisha kwa mda mrefu kama ilivyozoeleka kwa gari za Toyota.
Uzalishwaji kwa jina la Dualis ulidumu mpaka 2014, ambapo models mpya zilizotoka baada ya mda huo ziliitwa Nissan Qashqai badala ya Nissan Dualis.
GHARAMA ZA KUAGIZA GARI HIZI
Kwa wastani kuagiza gari hizi hugharim kuanzia 14.5m mpaka 15.8m kutegemea na muuzaji huko nje na mwaka husika wa gari ambao huamua ushuru kua juu au chini kidogo.
Pichani ni baadhi ya Nissan Dualis tulizokabidhi kwa wateja wetu hivi karibuni