IFAHAM MITSUBISHI PAJERO (1999-2006)
Na KIMOMWE MOTORS (T) LTD- Waagizaji Magari
Utangulizi
Iliundwa kati ya mwaka 1999 mpaka 2006 na katika mataifa mengine inafahamika kama Mitsubishi Montero au Mitsubishi shogun ikiwa imeboreshwa zaidi kwenye chasis inayoifanya itulie zaidi barabarani.
Injini
Diesel: Cc 2800 na nyingine ina Cc 3200. Inayopatikana zaidi ni ya Cc 3200 ikiweza kwenda mpaka km 11 kwa lita.
Petrol: kuna ya Cc 3000 na Cc 3500, inayoshauriwa zaidi ni ya Cc 3000 sababu ya matumizi ya afadhari ya mafuta ya kiasi cha mpaka kilomita 8 kwa lita.
Vifaa
Vinapatikana zaidi katika miji ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam kwa gharama za juu kiasi ingawa uzuri ni kwamba vifaa vyake vinadumu mda mrefu
Utulivu na Uimara
Katika mwendo mkali gari imetulia sana, kinachoisaidia zaidi ni mgawanyo mzuri wa uzito baada ya tanki lake kuwekwa kati kati na pia kuchanua kwa tairi za nyuma kunaokoongeza balance.
Katika Vumbi pia inafanya vizuri haswa kwa kua ipo juu juu na muundo wake chini unaiwezesha kukimbia haswa ikiwa na mzigo ndani.
Maoni/ Ushauri
Kutegemea na bajeti ya mteja, kama itakuruhusu tunashauri zaidi upate ya Diesel sababu ya kudum kwake, matumizi mazuri ya mafuta na kutengenezeka kirahisi. Ikiwa bajeti inaruhusu kupata ya petrol basi ni vizuri upate ya Cc 3000 ili kupunguza matumizi ya mafuta
Gharama
Gari ya Diesel inagharim kati ya 26m mpaka 28m wakati ya Petrol hugharim kati ya 20m mpaka 22m
Mawasiliano
0746 267740 au 0719 989 222 au fika ofisi zetu za Mbeya- Mwanjelwa Soko Jipya au Dar- Magomeni Mapipa