Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Hahahahhaha,kweli Dunia ina mambo na Mungu sio mnafiki,yule anaeimbwa mgonjwa anadunda tuu mtaani yule wanaemnadi mzima ndio anafloat.

Usicheke mkuu ,huzunika na wanao huzunika ,,hakika thawabu yako itakua kubwa Mbinguni
 
He never used to such long talks and speech giving, and so kukaukiwa sauti ni jambo la kawaida sana, it's not an issue.
Ila kuhusu afya yake naomba nisitie neno.
 
Kwenye taarifa ya habari saa mbili nimeshangaa kuona maandamano ya magufuri kuelekea uwanjani.polisi walipiga marufuku maandamano nchi nzima lakini leo sijaona polisi wakipiga mabomu haya maandamano yasio na kibali
1.jpg


Anachekelea nini sasa? Mbona hao anaowapungia mikono wamemnyoshea vidole viwili juuuuuuuu? Kweli CCM kifo cha mende
 
Tutaanza kesho Jangwani kufanya comparison, then ukweli tutaupata kuhusu nani kweli mwenye asili ya mafuriko..
Japo kumbukumbu zangu sijawahi ona kwenye siasa za tz MTU aliyewahi kumfunika Lowassa kwenye mikutano
 
Kila la heri ndugu na rafiki yangu MwanaDiwani.
Uwezo wa kujieleza na afya ya mtu watapima wapiga kura.
Ndugu MIGNON

Heri iwe pia nawe na Mungu akuangazie ili ufahamu vizuri hatma ya taifa letu.
 
Kwa kujikumbusha tu, hii ilikuwa ni taarifa kutoka Dodoma mwezi wa nne mwaka huu;

Thursday said:
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kufikishwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Naibu Spika wa Bunge, Bw Job Ndugai, alitoa taarifa hiyo muda mfupi kabla ya kuahirisha Bunge jana mchana ambapo wabunge walishikwa na taharuki baada ya kusikia taarifa hiyo.

Alisema hadi jana afya ya Waziri Magufuli ilikuwa inaendelea vizuri kutokana na matibabu aliyopewa na kuwaomba watanzania waendelee kumuombea ili apone haraka. " asubuhi zililetwa taarifa hapa, kwamba mwenzetu Dk. Magufuli anaumwa na amekimbizwa katika Hospitali ya Mkoa Dodoma kwa matibabu," alisema Bw Ndugai.

"Taarifa nilizonazo ni kwamba, alipofikishwa hospitalini na kupimwa, ilionekana ‘pressure' (shinikizo la damu) lilikuwa juu. Alisema kuwa tayari Waziri Mkuu,Mizengo Pinda alikwenda kumjulia hali hospitalini na kueleza kuwa hali yake inaendelea vizuri, preasure imeshuka ila bado anaendelea kusumbuliwa na vichomi.

Pamoja na kumuombea apone haraka mgombea uraisi kutoka CCM, John Pombe Magufuli, nataka pia nichukue nafasi hii kuwaomba wote wanaobeza hali ya afya ya mgombea wa UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa, kuacha mara moja dhihaka zao...Mungu hadhihakiwi. Pamoja tutafika.
 
Nimeshangaa nilipoona na kusikia mh.Magufuli alipokuwa akinadi sera huko mbeya alisema:

"Nimeamua kutembea kwa gari ili nione matatizo na changamoto za barabara japo wengine watakuja kwa ndege na helkopta hawawezi kujua changamoto za barabara"

Najiuliza hivi katika miaka 20 aliyohudumu kama waziri miaka 20 amehudumu kama waziri wa Ujenzi sasa leo anasema ndiyo anatembea kwa gari ili kujua changamoto za barabara ataweza kuzijua chanhamoto hizo kwa siku za kampeni wakati ameshindwa kwa miaka 20?

Bungeni alikuwa akitoa takwimu za barabara na kilomita nyingi,kumbe zilikuwa za uongo?alizitoa wapi hizo takwimu wakati hata changamoto hazijui?

Wananchi yeye amesema anashangaa wanafunzi kukaa chini? Anashangaa kuona kina mama wanajifungulia chini? Anashangaa kuona dawa hazionekani na hazipo hospitalini?

Je wananchi nyie hammshangai?

Hivi anashangaa hayo au anaishangaa ccm kuongoza miaka hamsini na nne bila hzo huduma?

Mshangaeni! Chukueni hatua.

Wagombea wengine kama akina magufuli ni kichefuchefu tu,nilichogundua wananchi wana akili sana kuliko wanaojiita viongozi,hiv unaposema unatembelea gari ili ujue matatizo ya wananchi huu ndio usanii uliokomaa kabisa hv miaka yote we Magufuli hukuona umuhimu wa kujua matatizo ya wananchi isipokuwa kwenye kampeni za kuusaka urais.Vilevile Magufuli eti anashangaa kwa nini mahospitalini hakuna madawa,yaani ukisikia kejeli ndio hiz,mgambea gani huyu hata kampeni hajui kupiga,Sentensi ya kusema nitafanya mkinipa waachieni UKAWA, ninyi mmeshapewa mmeshindwa.
 
Katika hali isiyo ya kawaida Magufuli ameugua ghafla akiwa jukwaani na kushindwa kuongea akiwa kwenye mkutano wa hadhara mbeya
Lazima afya za wagombea zikapimwe magufuli si mzima
Source:Chanel 10

Uongo huo.
 
Mbona picha hazipo?,peleka ukuda huko maana UMEJAA MAHABA YA KIJANI.
Weka ushahidi wa picha au unaogopa coz ni mpya zote au?!!.
SIMBILISI WEE!.
 
Sauti imekatika siku ya tano tuu.zikifika siku ishirini pumzi nayo si inaweza kuwa imerud ilikotoka?
 
Back
Top Bottom