Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Wewe unafikiri katika zama hizi za digital mwl mkuu angetunia zumari kuwaalika wenzake kwenye mkutano. Kuna sheria imevunjwa hapo.

Wasanii 200 wa kampeni fanyeni mtunge wimbo wenye miondoko ya 'yerusalem' kwa ajili ya JPM na CCM. Changanye na baadhi ya sets za kwata za wajaluo wa musoma.
 
Mgombea wa Urais wa CCM ndg John Pombe Magufuli, leo mchana alikuwa Shinyanga mjini. Baada ya hapo kesho tarehe 4/9/2020 atakuwa Simiyu akipitia Maswa.

Rafiki na ndugu yangu mmoja ni mwalimu. Yuko Maswa. Leo kapokea text message toka kwa mwalimu mkuu wake wa shule ikimtaka kuwahimiza walimu wake kuhudhuria kampeni. Ujumbe unasomeka hivi (nimeuambatanisha na andiko hili hapo chini);

"....waalike walimu wako wote kesho kuhudhuria kampeni za Urais Maswa, Mheshimiwa Rais Magufuli atakuwepo..."

Huyo mwalimu mkuu amesema naye kapokea ujumbe huo toka kwa mkuu wa idara (Afisa Elimu - Wilaya). Naye kapewa order na DED na DED kapewa order toka kwa DC na DC naye kapokea amri toka kwa RC...

Hiki ndicho wanachokifanya CCM. Wanatumia "ujinga" wa baadhi ya watumishi kulazimisha mambo yao. Ukicheki hii, ni kama mwaliko wa kawaida lakini nyuma ya pazia kuna amri.

Bahati njema rafiki yangu kasema hana taimu chafu kama hiyo unless wagawe "mshiko" yaani ingalau "night" moja hapo wanaweza kwenda ingalau kuwazuga.

View attachment 1557512
Mbona ni mualiko, kuna tatizo gani sasa
 
Wakati kampeni hazijaanza alikuwa mwenyewe kujiimarisha, cha kushangaza jinsi siku zinavyoenda amezidi kuporomoka na watu kumwona hana jipya kwenye kampeni zake.

Sera anazoongea hazina mashiko amebaki na sera za kukejeli na vijembe ambavyo wananchi wanaona hana kipya.

Amekaa miaka yote 5 kapunguza ajira halafu leo anakuja tena kusema ataleta ajira mil 8,mara mimi sitoki nje ya nchi ni mzalendo,ajira elfu 8 kashindwa ataweza mil 8 kama siyo kutuletea comedy, vile vile kutokwenda nje ya nchi haionyeshi kwamba we ni mzalendo ni hofu yake tu.

Kusema Lissu siyo mzalendo kisa amekaa nje ya nchi haina mashiko ni kuropoka tu maana hakuna asiye jua alienda kwa matibabu.

Magufuli anaenda kuwa Rais wa awamu moja dalili zote zinaonyesha ,wafanyakazi wamemchoka ,wastaafu wamemchoka ,vijana wamemchoka, wazee wamemchoka na kila mtu anamwona vyote anavyoongea ni usanii tu
Wapigaji wamemchoka wale waliozoea kula pesa ya mabango wakati wa kampeni.

Wazalendo wa kweli hawawezi kumchoka, wanatambua maono aliyonayo yalivyo na uhusiano na maisha yao.

Wenye kujua maana ya upanuzi wa bandari na uboreshaji wa viwanja vya ndege hawawezi kumchoka.
 
Nikiangalia sura za waliopo kwenye kampeni naona ni sura za vijana wa mtaani wakiburudika na jembe lao Magufuli .....hivi mkoa wa shinyanga unaweza kuwa na walimu wangapi??
 
Wakati kampeni hazijaanza alikuwa mwenyewe kujiimarisha, cha kushangaza jinsi siku zinavyoenda amezidi kuporomoka na watu kumwona hana jipya kwenye kampeni zake.

Sera anazoongea hazina mashiko amebaki na sera za kukejeli na vijembe ambavyo wananchi wanaona hana kipya.

Amekaa miaka yote 5 kapunguza ajira halafu leo anakuja tena kusema ataleta ajira mil 8,mara mimi sitoki nje ya nchi ni mzalendo,ajira elfu 8 kashindwa ataweza mil 8 kama siyo kutuletea comedy, vile vile kutokwenda nje ya nchi haionyeshi kwamba we ni mzalendo ni hofu yake tu.

Kusema Lissu siyo mzalendo kisa amekaa nje ya nchi haina mashiko ni kuropoka tu maana hakuna asiye jua alienda kwa matibabu.

Magufuli anaenda kuwa Rais wa awamu moja dalili zote zinaonyesha ,wafanyakazi wamemchoka ,wastaafu wamemchoka ,vijana wamemchoka, wazee wamemchoka na kila mtu anamwona vyote anavyoongea ni usanii tu
Huyu naye amevutiwa na nini kama JPM amepoteza mvuto?
IMG-20200903-WA0050.jpg
 
nimetazama mkutano wake wa leo Shinyanga ni kama anawakaripia wananchi 🤣 🤣 🤣
 
Si ni mualiko , Chadema wao wanapiga overall wanasema watu wote mnaalikwa kwenye mkutano , CCM wanaspecify kila group linaalikwa , sion kosa hapo unless kama ni shuruti
 
Chadema mwambieni Robertson wa Amsterdam, lissu ni Rais [emoji3]
 
Kwani kibaya kitugani? Nini maan ya mualiko? Hakuna mtu aliyelazimishwa kwenda kwenye kampeni ila wao tuu wamealikwa wanamawili kukubali au kutokwenda.vita ni vita, mbona chadema wanawanunulia boda mafuta ya buku mbili hakuna mwana ccm aliyekuja kulalama.
Alichosahau tu ni kwamba canter na mafuso ya kuwabeba hayana mafuta!
 
Juzi tu mheshimiwa Sana na mtetezi wa haki za binadamu na zile zisizofaa Kwa tamaduni zetu" aliwahimiza watu wote kutoka sehemu zote za nchi yetu kumsindikiza kwenda kuchukua fomu za kuteuliwa kuwa mgombea wa uraisi! Je alikosea?
 
Kumbe ni "waalike". Hii haimshurutishi mwalim kuhudhuria mkutano husika.
 
Kwani serikali bado inaongozwa na chama gani kwa sasa? Kama wapinzani wana sera nzuri na mgombea anaefaa mafuriko mbona yapo tuu, hofu ya nini??? Mimi mikutano yote ya Lowasa Mbeya 2015 nilihudhuria na wala sikuambiwa na mtu tishirt nilinunua elf 15 kofia 15 wala haikuniuma,kwa hiyo upinzani mwaka huu mbona kutetemeka kwingi, Kwani kuna wasiwasi nawagombea waliosimamishwa? Mara Magufuli katoa rushwa kununua kuku.. Leo katumia waalimu sms Kwani waalim ni watumishi wa serikali ya chama gani??????
 
Si bora hiyo inasoma ni mwaliko

msg yetu walimu inasema hivi nanukuu

Walimu wote wa darasa la 1.2,3,5,6 na wale ambao hamtakuwa na vipindi darasa la 4 mnatakiwa kuja kwenye mkutano wa ugombea urais wa chama cha mapinduzi.
 
Back
Top Bottom