Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Wewe sio mfuatiliaji. CCm technologia inawaumbua sana safari hii, haujaona barua ya VC wa UDOM akilazimisha wafanyakazi kwenda kwenye ufunguzi wa kampeni za ccm? Robert Amstadarm kasema ana compile ushahidi...... unadhani watu hawajui maouvu yenu? mtakoma
U sound stupid eti tutakoma[emoji23][emoji23] yani kama vile huyo mume wenu beberu ndo anayemiliki oxygen yote ya tanzania.
 
Wanaalika watu ulitaka waalike Mbuzi... kuna chama kinachofanya kampeni bila ya kuita au kualika watu?
 
Nimejaribu kufanya tathimini na kuangalia namna kampeni za kugombea nafasi za urais,ubunge na urais hapa Tanzania. Nnimeg'amua on face it mgombea wa Ccm ndugu JPM ameshapata ushindi na Mungu akipenda ni kama anafanya kampeni kama formalities tu ili kukamilisha taratibu.

Kitendo cha wapinzani kujiliza kama watoto kuwa walizuiwa kufanya siasa ndio sababu ya kushindwa hazina mashiko. Wapinzani walikuwa na nafasi ya kuuza na kunadi sera zao majimboni,lakini walipuuzia.

Nimegundua watanzania wanataka matokeo chanya. Jambo hili limefanya mgombea wa Ccm kwa urais apate ushindi mapema. Kama ni kwenye ndondi pambano limeisha round ya kwanza. Najiuliza hata kama wangekuja majimboni kumwaga sumu dhidi ya Ccm wangetuambia nini? Maana watanzania tumeona kilichofanyika ndani ya hii miaka minne na nusu. Na mpaka sasa tunajiuliza haya yangefanyika miaka thelathini iliyopita mfulilizo Tanzania ingekuwa vipi?

Wapinzani wanapanda majukwaani hawana hoja wala sera za kuwaambia wananchi. Hii imekuwa Dalili kuwa wameshakubali kipigo mapema. Mtu unayetaka kuwa rais wa JMT huwezi kusimama jukwaani na kusema eti hata wakoloni walijenga Shule na barabara. Ina maana unapoteza muda na pesa za hao unaowachangisha kwenye mabeseni. Maana ipo wazi kabisa mkoloni alikuwa anajenga hivyo vitu ili kutunyonya na kujenga kwao. Na kwa kusema eti uhuru na haki za watu vinaminywa. Vinaminywa kwa namna gani? Kama rais anatawala kwa kufuata misingi ya katiba na sheria haya yanatokea wapi?

Hii ni dalili kuwa wapinzani wameshindwa mapema. Kama kiongozi wa chama cha upinzani unasimama jukwaani na kulaumu eti kwa nini mradi wa kuchimba gas haujafanyika bila kujali maslahi ya taifa lako, wewe na chama chako mnafaa? Mnapoteza muda na pesa za walalahoi!

Mgombea wa Ccm anajihakikishia ushindi mapema kabla hata siku kumi za kampeni kuanza. Mfano ni kuahidi kutekeleza ununuzi wa meli tano za uvuvi kanda ya pwani na kufufua shirika la uvuvi Tanzania hii ni nyundo ambayo itawamaliza wapinzani.

Na kwa sababu watanzania wanajua ana uwezo mkubwa wa kutekeleza, maana amefufua Atcl na meli za Mscl Lazima watampa tena mitano na hili limejidhihirisha kila eneo ambapo kampeni za mgombea wa Ccm au kampeni za Ccm zinapofanyika.
 
Tume ya uchaguzi wako wapi kuhusu kanuni?

Huyu mgombea:

1. Wanalazimisha watu kuhudhuria mikutano.
2. Mgombea usukumani anaongea kisukuma.
3. Dodoma aliahidi barabara 112km kupendezesha jiji iwapo tu watamchagua - hii ni rushwa.
4. Ikungi alijinasibu kuwa mgombea Lissu hatashinda Kwamba yeye ni rais anayeendelea.
5. Mgombea huyu taarifa zake tu ndiyo zinazotangazwa muda wote na radio za taifa na pia za kijamii pamoja na TVs.
6. Taarifa zingine za vyama zinaminywa kwa mkono wa serikali ya hiki chama tawala.
7. Mgombea huyu anahimiza wagombea wake tu wachaguliwe hata kama wa upinzani ni bora zaidi.
8. Nk nk

Tume kanuni zao zinasema nini kuhusu haya?
 
Mgombea wa Urais wa CCM ndg John Pombe Magufuli, leo mchana alikuwa Shinyanga mjini. Baada ya hapo kesho tarehe 4/9/2020 atakuwa Simiyu akipitia Maswa....
Lazima waende ,kumbuka wakati wa corona imepamba moto, na shule kufungwa, aliendelea kuwalipa walimu mishahara bila ya wao kufundisha,

Uganda hawalipwi mpaka sasa ,wanachoma mahindi tu barabarani
 
Lazima waende ,kumbuka wakati wa corona imepamba moto, na shule kufungwa, aliendelea kuwalipa walimu mishahara bila ya wao kufundisha,

Uganda hawalipwi mpaka sasa ,wanachoma mahindi tu barabarani

You are very ignorant and stupid at the same time...!

Eti "...wakati wa corona aliendelea kuwalipa mishahara walimu mishahara bila wao kufundisha..."

Hebu tuambie, Magufuli atoe wapi hela ya kulipa walimu wote maana unaandika kana kwamba anatoa hela kwa mama yake Chato kuja kulipa mishahara ya watu hawa...

Na yeye alikuwa analipwa na nani maana na yeye alikuwa kajifungia tu chumbani kwa mama yake Chato bila kuwepo kazini?
 
Kwani kibaya kitugani? Nini maan ya mualiko? Hakuna mtu aliyelazimishwa kwenda kwenye kampeni ila wao tuu wamealikwa wanamawili kukubali au kutokwenda.vita ni vita, mbona chadema wanawanunulia boda mafuta ya buku mbili hakuna mwana ccm aliyekuja kulalama.
Kweli wewe ni uporo wa nguna
 
Mgombea wa Urais wa CCM ndg John Pombe Magufuli, leo mchana alikuwa Shinyanga mjini. Baada ya hapo kesho tarehe 4/9/2020 atakuwa Simiyu akipitia Maswa...
Sasa inakuuma au mwambie na Msaliti Lissu afanye hivyo kama watamkubalia.
 
Sasa si ungeofuyta hiyo namba,waalkiamua kuifustilia si watampata?

Hakuna namba inayoonekana hapo zaidi +255754629......

Hii siyo namba kamili ya simu...

Shaka yako ilikuwa very much considered before posting this post...

Tunawafahamu CCM are very selfish and stupid ...
 
Sasa inakuuma au mwambie na Msaliti Lissu afanye hivyo kama watamkubalia.

Hainiumi chohote.

Nimi nimetekeleza wajibu wangu tu wa kutoa taarifa kwenu na kwako hata wewe ukawa na guts za ku - respond hivi japo bila kutumia akili.
 
Kwani kibaya kitugani? Nini maan ya mualiko? Hakuna mtu aliyelazimishwa kwenda kwenye kampeni ila wao tuu wamealikwa wanamawili kukubali au kutokwenda.vita ni vita, mbona chadema wanawanunulia boda mafuta ya buku mbili hakuna mwana ccm aliyekuja kulalama.
Acha ujinga kama hujui vitu ni bora uulize,ukipata ujumbe kama huo umetoka kwa Mkuu wako wa kazi maana yake ni lazima kuwepo ujumbe hauwezi kukulazimisha moja kwa moja kutokana na mazingira lakini uhalisia wake ni lazima kuwepo lasivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yako.
 
Rais Magufuli aliichezea bahati kwa miaka 5 leo anapata wakati mgumu kujinadi.

Haiingii akilini leo kuanza kuahidi kuboresha maslahi ya wafanyakazi, kuwaletea maji, kuwajali wachimbaji wadogo wadogo, muda wote huo wa miaka 5 alikuwa anafanya nini hadi aombe kuongezewa.

Kuna vitu vingine havihitaji muda kuongezewa masuala kama nyongeza ya mishahara na kupandisha madaraja, huwezi kuomba miaka mingine 5 ili uongeze mishahara.

Angeutumia vizuri muda wake leo asingekuwa na wakati mgumu kwenye kampeni, yaani analazimika kujieleza kama hakuwahi kuwa rais.
 
Mimi nimefanikiwa kupanda flyover ya Ubungo nikiwa kwenye mwendokasi kwa nauli ya Sh 650 tu. Sijawahi kupanda ndege yeyote wala bombadia ya Magufuli.

Sijui wangapi mmepanda flyover na bombadia za Magufuli?

Maendeleo hayana chama
 
Back
Top Bottom