Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Kwa hiyo baada ya miaka 5 kama bado hajamaliza miradi (kumbuka ataanzisha mingine), tutengue katiba ili tumpe mitano tena au tuondoe ukomo? Naona umejifunga goli tu.
Yaani tayari umeshajijibu mwenyewe bila kujua.
 
Kila nikiangalia, mahesabu yangu yananiambia kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 anapigwa asubuhi na mapema tu

1. Kura za Kaskazini zitamkataa vibaya mno
2. Kura za kusini zitamkataa katakata
3. Kura za Waislamu ndiyo kabisaa maana teuzi zake nyingi wamezilalamikia
4.Kura za mji mikubwa kama Mbeya na Dar es salaam atazisikia katika bomba
5.Kura za Singida kwa Tundu Lissu na Nyalandu hizo asahau
6.Kura za wafanyakazi ambao hajawaongezea nyongeza za mishahara atazisikia katika bomba
7. Kura za Vijana wasio na ajira, Vijana wa vyuoni wanamwangalia wanasema hiiiiiii etc
8.Kura za Watanzania walioko kwenye social media wengi hawamkubali
9. Iringa atapigwa asubuhi na mapema tu
10.Kagera ndiyo kabisa wanasubiri wapitishe hukumu
11. Kule Kigoma kwa Mwami Zitto ndo asahau kabisa
12. Wafanyabiashara wanaosumbuliwa kodi na TRA wamenyuti hawana maneno mengi wanamsubiri kwa hamu wamsulubu
13. Wenye Magari waliogeuzwa ng'ombe wa kukamuliwa pesa na Matrafiki hawa wanamgojea kwa hamu kubwa wamuonyeshe kilichomnyoa kanga manyoya
 
Hakika kazi zilizosimamiwa na Dk. Magufuli kwa maendeleo yaliyofanywa nchini ndani ya miaka mitano ni kubwa sana.Ilani ya CCM ya uchaguzi 2015-2020 imetekelezwa ipasavyo kwa kishindo.

Tusibeze maendeleo haya. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni huyu mzee.
 
Nimewaza sana na hii ni baada ya kuangalia hotuba nyingi sana za baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Swali langu la dhati kabisa. Je, leo angekuwa hai angemuunga mkono ndugu Magufuli?

Angeacha kweli kuusemea ukandamizaji uliofanywa na ndugu Magufuli?

Angesimama na nani leo ndani ya CCM?

Kiukweli CCM chini ya ndugu Magufuli imepoteza misingi yake yote. Ndugu Magufuli hasafishiki kwa yaliyotokea ndani ya nchi kwa miaka yake mitano ya uongozi.

OLE kwa wanaomuunga mkono kwakuwa tu wanataka chochote kitu. Nasema OLE! Kilio cha watakaokosa na waliokosa haki ki juu yao.
 
Kamwe Nyerere asingeunga mkono ukandamizwaji wa watu unaoendelea leo hii kisa tu wamegoma kuunga mkono juhudi
 
NDIYO ANGEMUUNGA MKONO MAGUFULI - Ni ingeshindikana asingewapa uongozi Chadema. Kama ambavyo alirudia rudia mpaka CCM ipasuke ndio upinzani utakuwepo nchi hii.

Hali hii ya vyama vya upinzani Tanzania ilitokea marekani na ndio Thamani ya System inapokuja hapa.

Baada ya upinzani kukosa kukua kwa muda mrefu nchini Marekani, system iliamua kukipasua chama kilichokuwa kikitawala bila upinzani kwa muda mrefu Cha Republican. Na kikapasuliwa na kupata vyama vya Democratic Party na Republican Party.

Hili jambo lilifanyika ili Marekani iwe na ushindani wa kutosha kwa faida na maslahi ya Marekani. kwa kuwa taifa liliamua kufanya siasa ya vyama vingi. Hali hiyo hiyo iliyokuwa Marekani wakati huo tusishangae system ikatengeneza hali hiyo hapa kwetu Tanzania.

Muda sahihi ukifika hiyo system mnayo ilaani sana leo hii itawasaidia kupata chama cha upinzani imara chenye credibility, integrity, Capacity na capability ya kupokezana madaraka na CCM kwa kuaminika.
 
Kamwe Nyerere asingeunga mkono ukandamizwaji wa watu unaoendelea leo hii kisa tu wamegoma kuunga mkono juhudi
Enzi zake hakuwa mkandamizaji ?

Sisi wadogo kiumri huwa tunaambiwa Magufuli anafanana sana na Nyerere, sema tu magufuli hana speech sensible kama za nyerere
 
Nyerere hawezi kuunga mkono mambo ya aina hii hata kidogo pitia clip za mwalimu utaelewa yule mzee muacheni apumzike kwa amani.
 
Nyerere aliheshimu uhai alitetea Uhuru the highest punishment nyerere could have given ni house arrest imagine magufuli ndio angekuwa nyerere wale waliotaka kumpindua wangebaki hai? Wala mwinyi asingewakuta .
 
Kaisikilize sauti ya mwalimu juu ya wanasiasa malayamalaya ndio utapata majibu
 
Nimewaza sana na hii ni baada ya kuangalia hotuba nyingi sana za baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Swali langu la dhati kabisa. Je, leo angekuwa hai angemuunga mkono ndugu Magufuli?

Angeacha kweli kuusemea ukandamizaji uliofanywa na ndugu Magufuli?

Angesimama na nani leo ndani ya CCM?

Kiukweli CCM chini ya ndugu Magufuli imepoteza misingi yake yote. Ndugu Magufuli hasafishiki kwa yaliyotokea ndani ya nchi kwa miaka yake mitano ya uongozi.

OLE kwa wanaomuunga mkono kwakuwa tu wanataka chochote kitu. Nasema OLE! Kilio cha watakaokosa na waliokosa haki ki juu yao.
Alichofanya madaraka nyerere Kwa Lissu a lipo kuwa Mara ndo angekifanya Nyerere angekuwa hai.

Case closed
 
Back
Top Bottom